Karibu sana kaka Ksonrap hapa Micshariki Africa. Tuanze kukutambua kwanza, Ksonrap unaitwaje rasmi, unatokea wapi na unajishughulisha na nini kwenye maishani mwako na kwenye utamaduni huu wa Hip Hop?
Jina langu kamilin nii Karim Athumani Kamba, natokea Dar Es Salaam. Najishughulisha na biashara ndogo ndogo/ujasiriamali pia nipo kwenye utamaduni wa Hip Hop, najishughulisha na deejaying japokuwa kwasasa nimejikita zaidi kwenye uchanaji/emceeing.
Tueleze kuhusu historia yako kidogo; ulizaliwa wapi, ulisomea wapi, shule za msingi, upili na pengine kama uliendelea baada ya hapa. Utoto wako ulikuaje?
Nilizaliwa Dar Es Salaam, Muhimbili Hospital 1994 na makuzi yangu nimekulia Kilimanjaro/Marangu. Elimu yangu ya msingi nilisoma Marangu Mazoezi na baadae Darajani Secondary ndipo nilimaliza Form 4 pale nakurudi Dar Es Salaam nikasoma chuo Zoom Polytechnic mpaka Diploma ya (Information Technology) na baadae VETA, chuo cha ufundi stadi.
Kuhusu utoto wangu nilikuwa machachari sana na mtundu ila nilikua napenda kujua mambo mbali mbali; nilipenda sana kuskiliza muziki, kipindi kile nilikuwa napenda sana kuskiliza muziki wa Prof Jay, Sugu, Daz Nundaz, Afande Sele, Domo&Dojo, Geez Mabovu, Saigon na Hip Hop heads wengine kwa hiyo nilikuwa na record nyimbo zao kutoka redioni kwenda kwenye kanda (tape) hapo ndipo nilianza kupenda muziki
Mbona unajiita Ksonrap? Jina lilikujaje na linamaanisha nini?
Maana ya Ksonrap ni hii; hiyo K inasimama kama Karim na pia Kamba na Son ni mtoto wakiume (unaweza kusema pia mtoto wa kiume wa kamba) ilhali rap ni kile kitu napenda kufanya na ndio jina linakua Ksonrap!
Ksonrap kwa wale wameanza kukufahamu hivi majuzi, wanakufahamu kama emcee ila mie nimeanza kukufahamu kama mwanaharakati (wacha nikuite mkutubu😁 wa Hip Hop). Tueleze kuhusu upendo wako kwa Utamaduni huu ulikujaje? Turudishe nyuma ili tuweze kufahamu safari yako na Hip Hop?
Nilipenda kusikiza muziki wa Hip Hop/Rap tangu nikiwa chalii mdogo kwa hiyo old school ndio msingi wangu ni kitu napenda kuskiliza sana nimekuwa niki collect miziki mingi ya old school kwa muda mrefu na nina tape tofauti tofauti za wasanii mbali mbali kwa hiyo nikajikuta nime hifadhi kazi nyingi sana kiasi kwamba kuna baadhi ya wasanii walikuwa wamepoteza kazi zao wanani cheki na kuzipata kwenye maktaba yangu kwahiyo
"(Ain't nuthin' like the old school!”?) What more could I say? I wouldn't be here today. If the old school didn't pave the way"
Mistari hiyo kutoka kwa nguli wa rap duniani hayati 2Pac Shakur inanihusu sana kuhusu mapenzi yangu kwenye utamaduni huu, nimakubwa sana nashidwa kuelezea kwa ufupi ila napenda sana utamaduni huu napenda kujifunza mengi zaidi na nimepata maujanja na maujuzi ndani ya utamaduni.

Kaka Ksonrap nilianza kukufahamu vizuri wakati nikitafuta album ya Marehemu Ebbo Mi Maasai nikapata nakala yake pale Audiomack kwa account unayo imiliki. Kucheki freshi nikakuta una miradi ya ma emcee na makundi kibao. Hivi ulianzanje kukusanya miradi hii na kuanza kuiweka pale Audomack?
Ni kweli niliona watu wengi wanapata shida kupata hizo kazi kwa kuwa nilikuwa nazo tayari haikuwa shida kwenye maktaba yangu zipo kazi zakutosha nikawa na share pale Audiomack ili watu wanaosumbuka kupata waweze kuzipata japo mwanzo sikudhani kama italeta impact kubwa kiasi hicho na kwenda viral kiasi hicho.
Mimi awali sikukufahamu kama mchanaji ila kama mwanaharakati wa Hip Hop. Wito wakuanza kuchana ulikujaje na ulipotoa kazi yako ya kwanza mapokezi yalikuaje? Ngoma hii inaitwaje?
Nilikuwa mfuasi mzuri wa wachanaji wengi ndani ya utamaduni japokuwa nilianza kuchana kitambo nikiwa secondary school Darajani ila baada yakumaliza shule nakurudi dsm miaka ile ya 2011 mwishoni ndipo nikawa muudhuriaji mzuri wa kilinge cha Tamaduni Muzik. Kilingeni kulinijenga sana nakukutana na washkaji wengi sana kama Boshoo, Maarifa, Bokonya Moh Rhymes, Syllabus, Bunch, Ommy Pah, na wana wengine wengi ila ngoma ya kwanza haikuwa na mapokezi makubwa nilisifiwa tu na watu wangu wakaribu nakuniambia naweza niendelee kukaza ninakipaji 😅💪🏾sikukata tamaa nimeendelea kufanya mpaka leo nimekuwa na mapokeo chanya kwenye jamii na mitandao mbali mbali.
Mpaka sasa una miradi mingapi, iwe ni EP, Mixtapes au albums, inaitwaje na ilitoka lini? Mapokezi ya hii miradi yako imekuaje?
Mpaka sasa nina miradi wiwili; wa kwanza unaitwa Nawakilisha Album ambayo ilitoka 2022 na ya pili inatwa ijulikane 2023 mixtape Ambayo imetoka 2023. Zinapatikana kwenye mitandao ya kuskiliza muziki.
Tueleze kuhusu harakati zenu pale Kiota. Kwanza Kiota ni nini, nani wahusika na mnajihusisha na nini? Nia malengo yenu ni yepi?
Kiota ni kichaka cha ndege ambacho hutaga mayai nakulea makinda mpaka wanapokuwa nakuanza kujitegemea ndio hivyo hivyo Kiota tumekuwa tukichukua wasanii nakuwalea kisha wakishaweza kujitegemea tunawaachia wanajitegemea.
Wahusika ni MV09 wapo pale Mbezi Beach zilipo studio za MV09 Records. Malengo nikukuza nakulea vipaji vichanga kisha kuvitambulisha kwenye Jamii.

Kiota
Hivi majuzi nimeona umekuja na chata lako We Represent Real Hip Hop. Kwanza hii "Real Hip Hop" ni nini na mtu gani anaweza kuingia kwa hili kundi la "We Represent"? Wazo wa hili chata lako lilikujaje na chata lako linamaanisha nini? Wapi linapatikana na kwa bei gani?
Hizi movement nilianza muda kidogo nishatoaga chata linaitwa Nawakilisha Swahili kitambo kile pale kilingeni. Juzi kati nimekuja na Represent The Real Hip Hop, wazo la chata halikuwa jipya kwa kuwa ni moja kati ya zile 6 elements of Hip Hop (street fashion) ipo ndani mtu yoyote wa utamaduni huu anaweza kuingia ndani na ambae anawakilisha Hip Hop ya kweli. Chata langu linapatikana kwa kunipigia mimi mwenyewe namba ya simu +255714333384 bei ni tsh 20,000 tu.

Ni ma emcee gani na watayarishaji gani hapa nyumbani na pia mamtoni wanaokuvutia na utendaji kazi wao?
Watarishaji ni P Funk, Palla Midundo, Bin Laden, OmmyPah, Texas, Duke Tachez, Chizan Brain.
Mamtoni napenda kumskiliza Nas, Dmx, 2pac, Eminem, Biggie, Sean Price, Onyx, Evidence, Jay-Z, The Game, Mobb Deep.
Watayarishaji ni DJ Premier, Dr Dre, Scott Storch, Swizz Beatz.
Kwa hapa nyumbani navutiwa sana na Salu Tee(R.I.P), Saigon, Stereo, Chid Beenz, Domo Kaya, Fid Q, Nash MC, Ghetto Ambassador, S.O.G, Khalighaph Jones, Jay Moe, Kikosi, Watengwa.
Kama mtunza Historia wa Utamaduni wa Hip Hop je hali ya Hip Hop Tanzania na Africa Mashariki ipoje kwa sasa?
Hali ya Hip Hop naona ipo vizuri maana kitambo kidogo ilikuwa inaonekana kama ni uhuni ila Hip Hop imekuwa na mchango mkubwa kwenye jamii; kuelimisha, kuburudisha pia imetoa viongozi mbali mbali kwenye jamii mpaka serikali kama vile Sugu (Jongwe) na Prof Jay ni mfano wakuigwa. Africa Mashariki, Hip Hop inaendelea kusonga na kupiga hatua kubwa siku hadi siku mapinduzi makubwa kama Micshariki Africa na wana Philosopher kama Mikila Gego Master wamekuwa na mchango wakuendelea kuimarisha harakati hizi.
Jamii yako inanufaikaje na wewe kua emcee, zipi athari chanya kwa jamii yako zinazotokana na sanaa yako?
Cha kwanza kabisa ni elimu. najitahidi kuelimisha jamii yangu pamoja na kuwaburudisha na cha msingi kidogo nachokipata nimekuwa nikikirudisha kwenye jamii. Wapo ambao pia wananitazama kama kioo, inspiration wapo wengine wananipa heshima kwasababu ya kazi zangu.
Kama msanii anaetumia hizi streaming apps, tupe maoni yako kuhusu manufaa yake kwa sanaa yako. Siri ya hizi platform ni nini ili mtu aweze kunufaika nazo vizuri? Je hii ndio njia ambayo wasanii wanatakiwa watumie au waendelee kuuza kwa wateja wao moja kwa moja?
Nimefikia watu wengi zaidi ya mwanz. Watu wengi wamekuwa wakinifuatilia huko nimekuwa nikipata feedback nyingi kwa watu tofauti tofauti ambao wamekuwa wakinifuatilia huko pia kipato kimeongezeka. Sisemi moja kwa moja kama ndio njia sahihi kwamba wasani wa underground wautumie, wanaweza kutumia zote, wapo watu bado wanahitaji CDs na flash na ni wanunuaji wazuri wakazi kwa hiyo kwenye uhitaji kunasoko tujikite kote tu.
Mwaka 2023 ndio bado mbichi ila mpaka sasa ushaachia album pamoja na single kadhaa...ndio tumemaliza hivyo au bado kuna kazi kibao unatuletea mashabiki zako?
2023 nahahisi ndio mwaka ambao nitaachia kazi nyingi zaidi maana nina kazi nyingi tayari nimeziandaa, miradi mingi inakuja mashabiki zangu mkae mkao wakula.
Ushauri gani unao kwa ma emcee chipukizi wanaotaka kukuza vipaji vyao ili viweze kuonekana?
Nawashauri wawe na nidhamu na bidi na pia wajitume na kuchimba zaidi mambo ya utamaduni pamoja na kufuatilia wale walio watangulia ili waeze kupata ujuzi zaidi katika kazi.
Kando na kuskika kwenye streaming apps je una mpango wa kuandaa matamasha kwa ajili ya mashabiki zako hata kitaani kwako tu?
Huwa naanda tamasha la cypher kila mwisho wa mwaka mtaani kwangu Kinondoni, nadhani kabla mwaka haujaisha nitakuja na taarifa wapi litafanyika na tarehe rasmi.
Tukimalizia wape tano wale ambao wakua nawe kutoka mwanzo wa safari yako na muziki hadi hapa ulipofikia.
Napenda kuwapa tano daddy & mommy na mwanangu wote wa Mp Classic, DJay P, Kiota Mv09, Bega Kwa Bega, OmmyPah, Kefa Mkombola na wanangu wa Kinondoni na pande zote walipo mafan's wangu big up🤝🙏🏽👊🏾
Neno la mwisho? Nini sijakuuliza ambacho ungependa kutuambia?
Kitu ambacho sikipendi kwenye utamaduni ni umimi, ubinafsi, dharau…tupendane, tushirikiane kuifikisha sanaa yetu mbali zaidi (upendo).
Shukran sana, tupe na anwani zako za kijamii na wapi kazi zako zinapatikana?
Email: ksonrap@gmail.com
WhatsApp: +255714333384
Napatikana kwenye mitandao ya kijamii;