Big G
BIG G.
Kama umfahamu BIG G, niruhusu nimtambulishe kwako.
BIG G anaefahamika rasmi kama George Kahingo alizaliwa na kukulia Nairobi na baadaye aliondoka akiwa na umri wa miaka 10 na kuishi Marekani.
Alikulia katika familia thabiti ya watu watano, dada mmoja mdogo na kaka mdogo, "Ninawapenda ndugu zangu hadi kifo, kimsingi kwa sababu niliwalea , na hakuna kitu kinachoingia kati yetu", Anasema BIG G.
BIG G alihudhuria chuo kikuu huko Virginia ambako alisomea udaktari na kufuzu na Shahada ya kwanza ya Biolojia na katika Biashara na Kemia.
"Bado napenda sayansi na nitamiliki biashara yangu mwishowe, lakini hadi sasa hivi, muziki ndio kipaumbele changu kikuu, ona nyote mkiwa juu"
BIG G.
Je ni kipi kilichokuskuma hadi ukajipatia jina lako la kisanii, Big G?
Sikumbuki haswa ni nini hasa kilinifanya kuchagua jina hilo lakini siku zote nimempenda Notorius BIG na ni wazi G inatokana na jina langu la kwanza halali. Siku zote niliwaambia watu waniite Big G katika shule ya upili kama mzaha lakini kimsingi nilitaka hilo liwe jina langu la utani. Chuoni niifahamika watu waliniita G, na hiki sio kitu kidogo kwangu kwa hivyo ni BIG G BABY!
Safari yako ya muziki imekuwaje? Ni nini kilikuingiza kwenye muziki wa rap?
Kilichoniingiza kwenye Rap ni rahisi; nilipata ushawishi mkubwa kutoka kwa Lil Wayne. Siku zote nimekuwa mwandishi tangu nikiwa mdogo, ilikuwa ni kitu nilichofurahia kufanya, iwe hadithi fupi, mashairi na hata mashairi ya hapa na pale kwa ajili ya kujifurahisha.
Lakini ni umahiri wa Lil Wayne wa kunadika mistari na uwezo wake wa uchanaji ndio ulionivutia na kunifanya nitake kutengeneza mashairi yanayoweza kushindana na uandishi wake. Kabla sijapata utambulisho wangu kama mwimbaji wa nyimbo, nilitaka kuwa kama Lil Wayne, na kadiri muda ulivyosonga nikaona wasanii waliona vipaji vidogo wakifanya makubwa na nikaona kama nina deni la kurap ili kurudisha uandishi wa mashairi mazuri polepole ambayo yalikua yameanza kupotea.
Muziki umekuwa sehemu ya maisha yangu kila wakati, kama watu wengi ninavyodhani. Lakini nilikua nikisikiliza sana muziki wa Kikuyu ndani nyumbani kwetu pia mziki wa aina ya pop huku na huko wakati muziki wa Michael Jackson na Whitney Houston ulipokua unavuma Kenya. Nilipokuja Marekani ndipo nilipoanza kusitawisha ladha ya namna yangu, nikichochewa na rafiki yangu mkubwa Larry, ambaye pia ni Mkenya. Alinitambulisha kwa Lil Wayne, Young Money, J Cole , The Game etc. Kuanzia hapo ilikuwa mda wa kazi umefika!
Ulitambuaje kwamba muziki ndio njia yako ya maisha?
Utambuzi kwamba muziki ni kitu ambacho nitafuata ulikuja nilipoanza kutazama maisha jinsi ningepaswa kuwa, sio jinsi tunavyofundishwa. Kama wabunifu wengi , tunapata faraja katika kazi zetu.
Sanaa yetu ni kama koko ambayo imetenganishwa na ulimwengu wa nje. Ndani ya kifuko changu cha muziki nilihisi kana kwamba naweza kuwa yeyote niliyetaka kuwa, kiasi cha mafanikio makubwa nikifurahia mchakato huo. Mchoro wa kawaida wa jinsi mafanikio yapasavyo kupatikana ulinizidi kupungua niliposhuhudia matokeo ya watu katika uzee wao. Ikiwa ningekufa hata hivyo, ningeishi kikamilifu, badala ya kuridhika tu na kuwa hai. Naona muziki ni uhuru, ukombozi wa kweli.
Je, unalenga kuleta mabadiliko kwa njia gani?
Siku zote nimeamini kuwa tumewekwa kwenye dunia hii ili kuleta athari nzuri. Ninataka kutumia muziki kama njia ya kujitengenezea utajiri sio mimi tu bali kwa watu wengi wasiojiweza kadri niwezavyo. Ninataka siku moja kushawishi fursa ambazo zinaweza kuwasaidia wengine katika kutafuta mafanikio. Pia nataka kuwagusa watu kwa maneno ninayozungumza. Sio kila neno ni la kinabii, lakini yale ambayo yanatoka mahali pa uaminifu wa kweli ambayo nina hakika wengi watathamini siku moja.
Je! kazi yako ya muziki inaelekea wapi, nini maono?
Katika hatua hii ya maisha yangu nataka tu kufanya maisha madhubuti na msingi wa mashabiki waliojitolea. Kuwa Drake mwingine, au Lil Wayne itakuwa nzuri, lakini ikiwa ninaweza tu kuishi kutokana na sanaa yangu, itanipa uhuru na wakati wa kufuata mawazo yangu ya biashara. Chochote zaidi ya hayo kitakuwa baraka zisizo na kipimo. Baraka za ziada unaweza ziita.
Hapa Kenya, unawakilisha eneo gani, una mipango gani ya kuathiri vyema jamii yako?
Inapohusu Kenya sisimama tu kutoka kwenye eneo fulani, 254 yote ni nyumbani kwangu. Hakika nimekulia Nairobi lakini sote ni kitu kimoja haswa kwa mtazamo wa kutokea juu. Nataka siku moja niwe sehemu ya kujenga miundombinu mipya katika masuala ya miradi ya nyumba kule nyumbani. Ninahisi kama makazi duni yanahitaji kukomeshwa kabisa. Ningependa kuwa na mkono wa kusaidia katika elimu na kupata kazi. Ikiwa mambo hayo matatu yataboreka, hakuna kitu ambacho ulimwengu wote unaweza kufanya ili kuzuia Kenya kwa maoni yangu.
Je, ni mradi gani unaoupenda zaidi kati ya ile uliyoiachia hadi kufikia sasa?
Nimetoa nyimbo pekee kwa hivyo sina mradi ninaoupenda zaidi lakini wimbo wangu ninaoupenda zaidi unapaswa kuwa Black Sheep .
Ni akina nani wana ushawishi mkubwa zaidi wa muziki wako haswa hapa Kenya, unaweza kusema unafanana nao kabisa?
Sifahamu vyema muziki wa Kenya lakini mtu ambaye nadhani ningekuwa kama ninge chana nikiwa Kenya bila shaka atakuwa Khaligraph jones. Pia napenda Sauti Sol na Meja anaua pia.
Nini kinakufanya uwe tofauti na wasanii wengine wa Rap kwenye tasnia hiyo?
Kinachonifanya nitofautishwe na wasanii wengine wa rapa ni mambo mawili: Ninajali sana ufundi wa mchezo sio pesa tu, na mimi mwenyewe ni kweli.
Je ni nani shujaa wako mkuu au mtu unaehisi mnafanana nae?
Si lazima kuwa na shujaa mkuu au mtu aliyejiona kama mtu mwingine, lakini kama ningekua na shujaa basi ningekua mimi mwenyewe baada ya kufanikiwa.
Je una tabia zozote za kijinga ambazo tunapaswa kujua?
Tabia mbaya niliyo nayo ni mimi mwenyewe kuzungumza mara kwa mara, kwa njia ya mazungumzo sana.
Je, unadhani mustakabali wa tasnia ya muziki uko wapi?
Kuhusu mustakabali wa tasnia, sijui. Ikiwa ningefanya hivyo singekuwa na shida kujaribu kujijengea jina haha .
Je, unapanga kupenya soko la Kenya vipi?
Katika suala la kupenya kwenye soko la Kenya, nataka kujumuisha Kiswahili hapa na pale ninapotengeneza nyimbo za midundo ya afro na hata katika baadhi ya rapu zangu. Baada ya yote, mimi ni Mkenya, kwa hivyo nitakapopata umaarufu fulani itakuwa Big G na Kenya inayojulikana.
Je, una mpango wa kushirikiana na marapa wa Kenya?
Kwa sasa nina hamu sana ni nani nitachagua kushirikiana naye kutokana na kile ambacho kinaweza kushikamana na picha yangu ninayojaribu kuijenga. Nikikutana na watu ninaocheza nao na vibe na muziki wao, Wakenya au la niko tayari kufanya nao kolabo.
Wewe ni rapper wa Kenya mwenye makazi yake kule America, unadhani nini kinafanya muziki wa Marekani na Kenya kuwa tofauti?
Ninachofikiria kutofautisha tasnia ya muziki wa Amerika na ile ya Kenya ni wigo. Nchini Kenya kuna talanta fulani tu katika aina fulani za muziki ambazo zinaweza kufikia mafanikio makubwa katika tasnia ya muziki, ambapo huko Marekani unaweza karibu kupata maelfu ya watu katika aina hizi zingine za mziki ambazo zina wafuasi na kukubalika kama sehemu ya muziki bila kujali aina hiyo ya muziki ina umaarufu.
Sijawahi kusikia bendi ya Kenya ya Metal au mwimbaji wa muziki toka Kenya akitengeneza muzika wa kielektroniki lakini hapa (America) nahisi kama unaweza kuja na aina yoyote ya muziki na watu wakaivutiwa. Hilo pia linawaweka watu wengi kwenye soko la muziki ambalo linaweza kukunufaisha au likaingia katika hasara kulingana na kipaji chako. Kadiri watu wanavyokuwa wengi, ndivyo unavyopaswa kujitokeza zaidi.
Nini kinafuata kwa Big G?
Nini kinafuata kwangu? Nimemaliza kutoa single kumi kwa hivyo naanza kuziskuma sasa. Nina kazi kadhaa zaa muziki ambazo watu sasa wanaweza kwenda kuisikiliza. Kwa sasa pia nafanyia kazi project ya remix ya nyimbo kumi maarufu ambazo nitazitoa mwaka huu na baada ya hapo EP itatoka. Nina maudhui mengi yanayokuja,msimu wa G upo njiani!
Neno la ushauri kwa anaetaka kujitosa kwenye muziki na amejaribu sana hadi kufikia hatua ambayo anataka kukata tamaa?
Ushauri pekee ninaoweza kutoa sasa hivi ni kujiamini. Sijui zaidi ya yule mwenye ndoto katika suala la kile unapaswa kupigania kufikia katika maisha haya, hakikisha tu kua unachokifanya ni kitu ambacho ungependa kufanya kuliko kujuta haukufanya. Jipe kipaumbele.
Mitandao yako Rasmi ya muziki/mitandao ya kijamii?
Instagram : Officialbiggmusic
Tiktok : Officialbiggmusic
Na ngoma zangu zipo YouTube na majukwaa ya muziki ya kidigitali.
Je, ungependa kuwashukuru akina nani?
Ningependa kuwashkuru familia yangu kwa kuwa msingi thabiti, pia marafiki zangu kwa kujitokeza kila wakati, na pia marafiki zangu ambao hunipa mawazo chanya pamoja na binamu zangu kwa kuwa FAMILIA HALISI kutoka nyumbani. Nawapenda wote. Na pia ninajishukuru mimi mwenyewe kwakua nimeweze kuthubutu.