Ukaguzi Wa Albam: Antidote For The Soul
Msanii: Lord Arnold
Tarehe iliyo toka: 11th July 2020
Nyimbo: 10
Ma producer/Wapiga Midundo: Lord Arnold, HR The Messenger
Mchanganya Sauti na Midudo: HR The Messenger
Studio: Philosophy Recordz

Kitu kimoja ambacho Philosophy records iliyopo kule Ngong, Nairobi, Kenya imebarikiwa nacho ni hichi; producer mkuu wa studio hii, HR The Messenger ni muunda midundo na mchanaji pamoja na CEO/Mkurugenzi mkuu wake Lord Arnold.

Lord Arnold ni emcee wa kizazi kipya anayepatikana kule Nairobi na anajulikana rasmi kama Arnold Mwakio. Lord Arnold ambaye kwa kuamini uandishi wake wa mashairi ni wa kipekee na haufanani na wa mtu yoyote aliamua kujibariki jina Lord yani mfalme na kulitumia pamoja na jina lake moja rasmi Mwakio ili kupata jina lake la usanii Lord Arnold.

Lord Arnold

Yeye pamoja na mwenzake waliungana na kuunda studio yao Philosophy Records baada ya kuona kuwa walikuwa na vipaji vya kuchana ila studio hazikuwepo za ku record ngoma zao. Baada ya kupewa usaidizi na mzazi wake aliyemuwezesha kununua vyombo kadhaa vya studio na kushirikiana vilivyo na mwenzake HR The Messenger, studio ya Philosophy Records ilizaliwa rasmi. Sasa baada ya miaka miwili ya kuhangaika jangwani kama wana wa Israel, wawili hawa walifikia Caanan yao ki mziki.

Baada ya Philosophy Recordz kufanikiwa mradi wao kwa kwanza toka kwa producer mkuu HR iitwayo Reign na kufanikisha mradi wao mkubwa wa kwanza toka kwa Fikra Teule Azania Na Wanawe mkurugenzi Mwakio naye mda ulipowadia mwaka wa 2020 akaamua avue koti la ukurugenzi na aingie booth na kutubariki na mradi wake wa kwanza rasmi Antidote For The Soul.

Mradi huu ambao upo laid back mwanzo mwisho unatuonesha ni style gani ya Hip Hop production utarajie ukiskie HR The Messenger ndio producer mkuu wa mradi huu. Style yake soulful inafuse vizuri na sauti ya Lord Arnold ambae yeye pia kuchana kwa utaratibu mashairi yake.

Levels ndio wimbo wa kwanza kwenye mradi huu ambapo Wafalme Weusi hawa kama wanavyojiita HR na Lord Arnold wanatupatia historia yao ya kimaisha na kimziki kwenye mdundo mzuka sana unaopiga aste aste. Arnold anafungua historia yake kuhusu vile ili kufika pale amefika na ilibidi ahudhurie vinasa flani (freestyle battles) ambapo alishinda na kupata zawadi. Wimbo ni ubeti mmoja ambao hauna kiitikio. Levels unaonesha hatua alizopiga Lord Arnorld zilizomuwezesha afike alipofika akisema hivi,

“After 2 and a half years me ni murdering/
One Friday tuka set freestyle battle/
Nilikua nimeteveva sikushika mistari bado/
Looser ange buy Prestige Margarine/
Sikua na any and so nika bet my mother’s ring/
Siko ready hata kuangushwa na gathering/
Nikashinda battle wakanijenga na Walkman
I was lacking confidence na bado nina uwoga/
Nikasonga nayo nayo mistari nikichora/
KBC naskiza John Karani/
Kwa show ni MC The Kalimani/
Kupelekwa break na advert ya Kimbo/
Omo-Pick-A-Box, Kasuku ama Feeble/"

Kwenye wimbo huu, LA haogopi kuonesha madhaifu yake, alipoanguka na aliposhinda.

Uwezo wa Lord Arnold wa kutamba juu ya midundo ya HR The Messenger unazidi kuonekana kwenye wimbo kama vile Blame na Night Shift. Night Shift unamkuta Lord Arnold akishirikiana na Ezra pamoja na Markus wakiwa katika hali ya kutafuta Ankara. Maudhui haya ya utafutaji yanapatikana pia kwenye wimbo mzuka sana unaofuatia uitwao Cheques akiwa na Monski na HR. Cheques upo spidi tofauti na una mdundo mzuka sana unaoashiria kuwa hakuna mda wa kupoteza kwani muda kuupoteza kuna gharama utalipa tu. Hii ni banger yaweza pigwa kwenye club na kuwafanya watu kuamka kucheza wakati wakijiachia baada ya wiki ya kutafuta

Mada ya mapenzi pia imegusiwa kwenye mradi huu hususan kwenye nyimbo mbili Vanilla na Lofi. Vanilla unapiga tofauti kidogo, kama hi Hip Hop- Ragga freshi na ma sista do definitely inaonesha hawakusahaulika kwani ni wimbo flani wa bata hivi. Lofi nao unawakuta waanzilishi wa Philosophy Recordz wakitoa hisia zao za mapenzi juu ya warembo wanaochanganya akili zao. Kwenye biti linalopita gita taratibu vijana wanaonesha kuwa kwenye mapenzi wao pia huyayuka.

Antidote ndio wimbo uliobeba jina la albam hii na ni nondo zinatemwa hapa kwenye wimbo unaopiga chombo cha harp freshi sana. Wimbo huu umekuta ma emcee wakiachia mistari akiwemo na Trabolee pia.

Mradi huu mimi binafsi niliupenda na kwa maoni yangu ulikuwa mzuri ki production kama kawa HR alisimama sana na mradi ki ujumla ulikua na ubora mzuri. Kwa upande wa mada ndio kidogo naona Lord Arnold angepanua wigo na kugusa mada nyingine zaidi tofauti na zilizoguswa. Ila hamna was kwani kama mradi wa utangulizi Lord Arnold amejitahidi sana na ameonesha kuwa anauwezo wakuandaa mradi wake mwenyewe na kuuleta sokoni kando na kumiliki na kuongoza jopo zima la Philosophy Recordz. Kama unataka kuanza kujitibu taratibu basi Antidode For The Soul ipo.

Mcheki Lord Arnold kupitia mitandao ya kijamii:

Facebook:Arnold Mwakio
Instagram: Lord Arnold
Twitter: Lordarnoldybk
YouTube:Lord Arnold