Dom Down Click(DDC) ni jina la kikundi cha harakati za muziki wa Hip Hop kutoka Dodoma, nchini Tanzania. Jina la DDC lilibuniwa na Lucas Malali maarufu kakam LC. Leo tumepata fursa ya kufanya mahojiano nae ili kumtambua yeye, DDC na shughuli zao.
Utambulisho: Tupe majina yako kamili
Lucas Langford Ehud Malali.
Unapatikana sehemu gani, na una shughuli gani?
Mimi napatikana jijini Dodoma mitaa ya Mnadani, Capital. Ni mwanaharakati tu wa huu utamaduni( Hip Hop).
Tunajua wewe ni mtu muhimu sana katika muziki wa Handaki, ilikuwaje mpaka ukajikuta upande huu?
Mapenzi ya muziki wa Hip Hop ndo yalinifanya nijijumuishe katika huu utamaduni pia na influence kibao nilizokuwa naziona nje ya bongo na ndani ya bongo katika makuzi yangu.
Kwa nini utamaduni(wa Hip Hop), na sio upande mwingine.
Hip Hop nilikuwa naipenda Kwa sababu nilikuwa naona kama ina asili ya ushujaa shujaa hivi, ukiume ungangari, hiyo wakati mdogo na ma bro wangu tuliokuwa tukiishi nao home na kitaa baadaye nikajikuta naanza kujiona mhusika wa Hip Hop kabisa.
Ni watu gani hasa waliokupa ushawishi wa kujikita katika Hip hop kuanzia hapa Bongo na Ughaibuni?
Bongo wapo kibao kama HBC, Explastaz, Watengwa, Gangwe Mobb GWM, Kikosi Cha Mizinga, Diplomatz ilhali mbele NWA, Wu Tang Clan, Naughty by Nature, Daz EFX, Gang Starr , Lost Boyz ..Outlawz, M.O.P.
Unakumbuka ilikuwa miaka gani, au ulikuwa na miaka mingapi?
Miaka mingi kidogo man ila kipindi cha miaka ya tisini katikati hadi mwishoni.
Mr Lucas Malali, una mchango gani katika muziki wa Rap hasa kwa eneo la Dodoma?
Mimi bwana, nafanya harakati za ku provide skills kwa wanaopenda kurap kwa Dodoma, ushauri na mambo mengine mengine tu ambayo sipendi kuyataja hapa kwa upana wake.
Tunajua wewe ndio CEO wa DDC, tunaomba historia fupi ya DDC.
Yaani ilivyokuwa mpaka uanzishwaji wake hii kwa sababu ni ndefu naomba nilete link kutoka Wikipedia.”
Unaweza kutuelezea kwa kifupi tu baadaye ndio utuwekee hiyo link
Ni kundi la hip hop lililounganikana kama washkaji ila kabla ya kuwa DDC tulikuwa ni marafiki tu wa karibu ambao baadhi yetu urafiki huo ulitokana na wote kupenda hip Hop.
https://sw.wikipedia.org/wiki/Dom_Down_Click
Albam mpya ya DDC lini?
Mwaka huu ma project ya album ya DDC yanakuja siwezi kusema ni lini ila kwa upande wa producer kamaliza kazi yake bado wana kuingiza vocals tu so tusubiri kidogo.
Mpaka sasa DDC ina members wangapi na kundi pia hadi sasa lina albam/mixtape na EP ngapi?
Hii ni orodha kamili ya Wanachama wa DDC;
- Andre K (RIP)
- Adam Shule Kongwe
- Miracle
- Therapist
- Kanja Wizle
- Goda mc
- Javan (Chuna Ngozi)
- Sali Trejo
- Slogan
- Bad Jihidina
Project walizotoa kama kundi, bila msanii mmoja kutoka katika kundi mpaka sasa ni nne.
Nazo:
- The Element Vol. II (2014) - Mixtape
- Mechanism (2015) - Mixtape
- Fasihi Simulizi (2016) – Albam
- DIRA(2020) - Albam
Albamu za wanachama
- Chini Kabisa - Adam Shule Kongwe na Javan Chuna - Mixtape
- Elimu ya Juu EP (Andre K) -EP
- Fundikira(Miracle Noma) - Mixtape
- Kifamilia Zaidi (Javan) - Albam
- ANKO(Adam Shule Kongwe) - Albam
- Moto Umewaka(Adam Shule Kongwe) - Mixtape
- Uwanja Wa Fujo(Adam Shule Kongwe) – Albam
Dodoma kulikuwa na makundi mengi kitambo tuliyasikia lakini yamepotea baada ya kila member wake kufanya kazi mmoja mmoja na ikabaki kuwa wanataja makundi yao kwenye tungo zao, Je kwa DDC hii unaitazamaje?
DDC ipo itaendelea kuwepo naamini hivyo kwa sababu tumesukwa na ujamaa so labda urafiki au undugu wetu uvunjike kwa wote na sidhani kama itatokea mbeleni kama huko nyuma tumepita vyema.
Aisee kuna nini kati ya DDC na TamaduniMuzik. Binafsi huwa naona mnafanana kwa vitu vingi sana?
Siamini kabisa katika kufanana na Tamaduni kiitikadi wala kimifumo ila tamaduni ilichochea kukomaa kwa baadhi ya wanafamilia wa DDC coz members kadhaa wakati wanajifunza sanaa jamaa walikuwa on fire.
Halafu kwa nini mnapenda battles sana kwenye tungo zenu? Yaani mfumo wenu wa uwasilishaji ni ule ule lakini huu ni mtazamo wangu
Yeah ndo mfumo wa game yetu tulivyoamua iwe, ila naamini kabisa nyimbo nyingi pia ni tofauti na battle.
Tamaduni walianza game kwa battles na hapo nili note walikuja na kitu kinaitwa punchlines msisitizo waliuweka hapo.
Unazijua ngoma ngapi za DDC?.
Karibu zote man Lc, hiyo The Element na Chini Kabisa
Huwa najiuliza ni kwa sababu ya kuwa wako pamoja sasa kuna kuingiliana au kuvutiana kiuandishi na uchanaji.
Singo ya battle katika The Element ni moja, Chini Kabisa sijui kama zinazidi mbili.
DDC pia mlikuja katika mfumo huohuo wa kiuandishi na hapo ndipo nilipohisi mna uhusiano wa kimfumo na watu wa Tamadunimuzik. Nashukuru umeniweka sawa pia
Battle zilikuwepo kabla ya Tamaduni, japo uhusiano kati ya DDC na Tamaduni ulikuwepo na upo mpaka leo kiujamaa na kiharakati kwa baadhi ya watu pale Tamaduni.
Yaani ukimsikiliza Neno wa Kwanza, ukamsikiliza Dela P, ukamsikiliza Tawi, ukamsikiliza Adam hawa ni watu tofauti kwenye kila kitu. Ila ukimsikiliza Miracle, ukamsikiliza Andre K (R.I.P) unaweza usione tofauti ya moja kwa moja kuanzia uandishi mpaka uchanaji. Hata Javan mwanzo nilimfananisha na Kongwe lakini nilivyokuja kutulia nikagundua wana tofauti kidogo.
Unaijua DDC vizuri? Jaribu kuifatilia kidogo ili utoe mtazamo mzuri zaidi.
Nilihisi nimewafuatilia vyema ila ntajitahidi nizirudie tena kazi za wana kuzipa sikio. Sio mbaya kurudia mara nyingi kwa kadri inavyowezekana.
Tuendelee, changamoto za kusimamia kundi zikoje?
Changamoto hazikosekani ila kila jambo lina changamoto zake ukiona hadi leo tupo hivi ujue tunazimudu.
Dom Down Click mna mtazamo gani kuhusiana na hali ya kiuchumi lakini pia kijamii inayoendelea nchini? Je mmewahi fikiria kutoa elimu mtaani kama wafanyavyo MaKaNTa katika cypher zao bila kutoza kiingilio kwa hadhira?
Tumeendesha hizi harakati Dodoma mara kadhaa. Tushachangisha hadi pesa za maabara tukiwa na mkuu wa wilaya ya Dodoma. Pia tushakuwa na vilinge vya mtaa kwa mtaa, tulianzia kitaa cha DDC. Kwa sasa wana tupo sehemu tofauti tofauti kidogo, naamini tunapambana kujikimu kwanza binafsi ili tukitulia na kuunganisha nguvu tena tutafanya jambo kubwa kijamii na kiuchumi.
Video zimekuwa adimu sana kuliko audio, hii imekaa vipi Master hapo DDC?
Changamoto ya vichupa katika tasnia yetu ni kubwa kidogo ila inaenda kuisha soon.
Unaweza tuambia changamoto hizo ni zipi katika utengenezaji wa video?
Nadhani ma director wa Hip Hop Dom na taifa kwa ujumla ni wachache.
Unawezaje kuielezea handaki ya bongo kwa sentensi tatu? Pia katika hili changamoto zipi zipo katika handaki na vitu gani vya kuboresha ili tuweze songa mbele?
Wasanii wa Handaki wawe na malengo chanya kuifanyia Handaki sio Handaki iwafanyie nini.
Asante sana kwa muda wako, karibu tena Micshariki Africa
Wasiliana na Lucas kupitia mitandao ya kijamii:
Instagram: lucasmalali
Facebook: Lucas Malali