Msanii: Lugombo MaKaNTa ft Jadah MaKaNTa
Wimbo: Purify My Soul
Albam: Upendo Utuongoze
Tarehe: 13.01.2019
Mdundo: Marion Beats
Studio: MaKaNTa Jr. Records

Beti Ya Kwanza

Kilio changu cha machozi, nguvu, jasho na damu/
Pesa na muda sio kitu, gharama kwa sauti yangu na kalamu/
Maono yangu yasiote kutu, mwenye haki ashike hatamu/
Nimelelewa na mfumo butu, akili zangu bado timamu/
Na kumkomboa mwafrika sio lazima tumwage damu/
Nawasikia siwasikilizi wachungaji hata maimamu/
Samahani, sijawahi kuamini historia ya adamu/
Waliovusha dini bahari bado wanaabudu sanamu/
Waliolawiti ndugu zangu wakaleta uislamu/
Niwe mnyonge wa aina gani huu uovu kuukubali?
Umeniumba kwa mfano wako Sina budi kutafakari/
Natimiza lengo lako vingine siwezi kuvijali/
Je, uliniumba nifanye kitu gani hapa duniani?
Wanaojua nakuamini wewe wananiita mpagani/
Waumini hawajui mpinga kristo kiongozi wao/
Naamini uko ndani yangu, iweje niwasikilize wao/

Kiitikio (Jadah Makanta)

Dear lord, purify my soul
Dear lord, purify my soul
Kabla sijaongoza watu wangu, nijiongoze mimi kwanza
You Purify my soul
You purify my soul

Lugombo (Kiitikio)

Through sunshine and the rain
I feel love and I feel the pain
Purify my soul.