Toka kwa: Mac Dar Es Salaam
Wimbo: Stress
Albam: Single
Tarehe iliyotoka: 13.02.2022
Producer: Black Ninja
Studio: Boom Bap Clinic

Mac Dar Es Salaam

Beti Ya Kwanza

Nimefukuzwa kazi mwanenu nina stress/
Unaempenda akikimbia lazima upate stress/
Magumu ukipitia utakumbana2 na stress/
Maisha ya bongo yamekaza yana wapa watu stress/
Watu wamepagawa kila kona wanaenda lesi/
Vichwa vimechachawa sababu wana nyingi stress/
Wengine wana kaba/
Mpaka wanapatwa na kesi/
Huu si uongo bali ni ukweli nauchana kwenye verse/
Maisha ya uswazi hapa bongo wanangu ni magumu/
Vijana wana stress ndo mana wana vuta ndumu/
Kila siku maakamani kwenda kusomewa ukumu/
Nime aso miaka mingi mpaka leo sina room/
Mlokole akiwa na stress anataka Mungu amumbe/
Mlevi akiwa na stress muda wote ana agiza pombe/
Wakuja akiwa na stress anakumbuka kwao njombe/
Ila mack sinaga stress labda simba wakose kombe/

Beti Ya Pili

Kuna stress za maisha na stress za mapenzi/
Ila stress zingine uwa ni stress za kindezi/
Tumboni kwako ujala unawaza umiliki benzi/
We ni ndumba na kafara kichwa kimejaa ushenzi/
Stress zimewafanya wengi watoke kwenye game/
Stress zimenifanya nishindwe fanya mid-term/
Stress zimewafanya wengi waitwe marehemu/
Na stress sio bongo all over kila sehemu/
stress ikikupata mwamba unaweza ukapagawa/
Wengine hawaitaki wamekubali kuwa chawa/
Chidi imemtesa mpaka kavuta madawa/
Imepoteza nguvu kazi imepoteza nyingi power/
Stress ni mambo kichwani yanayo kusonga ukishindwa kuya imili unaweza ata ukajinyonga/
Ndo mana mabishoo wao wanapenda kitonga/
Utawakuta Masaki wanadanga Fish Monger/
Stress sio leo toka enzi za mababu kama ukiindekeza hakika utapata tabu/
Na ukiwaza sana utafanya mambo ya ajabu/
Utaonekana waki mtu usiyekua mstaarabu/
Stress sio Africa zipo paka kwa wazungu/
Usiwaze sana mengine mwachie Mungu/
Kama tatizo kazi vaa gwanda shika kirungu/
Au fanya biashara upunguze yako machungu/
Bwana mdogo izi stress zitakupa zogo/
Kama muziki hauwezi jaribu hata kuuza miogo/