Kyalo Kilonzo anayefahamika kwa jina la kisanii kama Malkolm K ni rapa chipukizi wa hivi karibuni ambaye amekuwa na mapenzi na muziki kutoka 2018 na akaamua kuwa mwanamuziki rasmi. Kwa sasa ana EP mpya iitwayo Timid Emotions ambayo in nyimbo kama Fathe na Keep It Mia .
Musiq Jared alikutana na Malkolm K ili tuweze kujua safari yake ya muziki. Alianzaje, amefanikisha nini hadi sasa na maoni yake ni yapi kuhusu matoleo yake ya hivi majuzi ya EP Timid Emotions na mipango yake ya baadaye mwaka huu.
Malkolm K anaieleza Timid Emotions, "kama mtoto wake mchanga. Anahisi kama kanda hiyo inaeleza jinsi alivyokua kama msanii kihisia na kiakili.
"Nimepitia mengi na Timid Emotions inajumlisha jinsi ninavyohisi kuhusu mapenzi, urafiki na ulimwengu kwa ujumla. Kila wimbo kwenye kanda hiyo chanzo chake ni tukio fulani katika maisha yangu na wale wanaonizunguka. Dhana nzima ya kanda hii ilitokana na maisha yangu ninayoishi". Anasema Malkom K.
Malkolm K ni nani, majina yako halisi na historia fupi kukuhusu?
Jina langu la serikali ni Kyalo Kilonzo. Mimi ni mwana, kaka na mpenzi kwa wengi. Nilizaliwa na kukulia Machakos ambapo jua huwa kali kila wakati.
Ulianzaje muziki?
Nilikuwa ninapenda sana sanaa sikujua ni muziki hadi baadaye maishani. Nilianza kuandika muziki tangu nikiwa mdogo lakini nilibahatika kukutana na rafiki yangu nikiwa chuo kikuu, ambaye aliniwezesha nikafahamu wapi ninaweza kurekodi mwaka wa 2018. Hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia studio na kurekodi. Nilihisi niko nyumbani.
Umekuwa ukifanya muziki kwa muda gani?
Niliachia rasmi ngoma yangu ya kwanza mnamo 2019 inayoitwa, Warm Turkey kwa hivyo naweza sema nimekuwa nikifanya muziki rasmi kama Malkolm K kwa angalau miaka 4.
Ni nini kilikuhimiza kufanya muziki?
Nilikuwa napenda mashairi na nilikuwa na binamu na kaka ambaye ni mpenda muziki na pia nikajikuta nikipendezwa na sanaa hiyo. Pia kusikiliza wachanaji kama Virusi Mbaya ambaye alinihamasisha sana hasa inapokuja kwa uandishi wa mistari. Huyo jamaa ni GOAT. Pia kusikiliza dancehall katika shule ya upili kuliathiri sana hamu yangu ya kufanya muziki.

Je, unaelezeaje aina ya muziki unaofanya?
Mtindo wangu wa muziki naweza kuuita Hip Hop ya kisasa(Contemporary Hip Hop). Vaibu freshi tu.
Mchakato wako wa ubunifu ukoje?
Kawaida huanza na kujiingiza kwenye hisia nzuri za wakati huo, wakati nikipiga mdundo na hapo ndipo ninapo anza kuunda muziki kichwani mwangu. Lakini muziki ninaoandika kwa kawaida huchochewa na jinsi ninavyohisi wakati huo au kile ninachopitia maishani.
Una EP mpya ambayo umeachia iendayo kwa jina la 'Timid Emotions', mchakato wa kuja na mradi huu umekuwaje?
Timid Emotions ni mtoto wangu. Ninahisi kama kanda inaelezea jinsi nilivyokua kama msanii kihisia na kiakili. Nimepitia mengi na Timid Emotions inafupisha jinsi ninavyohisi kuhusu mapenzi, urafiki na ulimwengu kwa ujumla. Kila wimbo kwenye kanda ulitiwa msukumo na tukio fulani katika maisha yangu na wale walio karibu nami. Kuja na dhana ya mkanda kimsingi ilikuwa kuishi maisha yangu.
'Timid Emotions' ina nyimbo ngapi na ni wimbo gani unaoupenda zaidi kutoka kwa albamu?
Timid Emotions ina jumla ya Nyimbo 8 huku 'Keep it Mia' ikiwa ninaipenda zaidi. Ukiisikiliza utaelewa kwa nini naupenda wimbo huo.
Kuna wimbo hapo ambao huupendi kivile?
Nyimbo zote nazipenda kwenye mradi huu wa Timid Emotions.
2023 imefika, nini tutarajie kutoka kwa Malkolm K?
Ninatarajia kufanya kazi na wasanii wengine. Ninajiandaa kufanya kazi na wasanii wengi na kitakachotoka jikoni ni kitu kizuri tu. Nitakuwa nikidondosha miradi zaidi pia…kanda kadhaa labda...huwezi jua kwa kweli.
Je, una mipango gani ya kuhakikisha unapata watu wengi zaidi kwenye muziki wako?
Kweli, ninapanga kufanya kazi na wasanii zaidi, kufanya mahojiano zaidi na maonyesho. Lo, na matangazo zaidi ya kujinadi

Rappers unaowapenda zaidi katika 254?
Virusi Mbaya, TnT & Jovi Jovv .
Neno kwa mashabiki wako?
Ninaandika kila wimbo kwa ajili yenu. Endeleeni kuwa nami na ninaahidi kuwaleteeni vaibu mzuka.
Je ungependa kumgotea nani?
Pongezi kwa Godfather wangu Dessy na watayarishaji wangu Groovy, Lemario na Kayo Rille na bila shaka mama yangu ambaye amekuwa akiniunga mkono sana.
Mitandao ya kijamii?
Facebook: Malkolm K
Instagram: malkolm_k
Twitter: @Malkolm_K
Neno la mwisho?
Upendo ni bure.