MaNgwair - A.K.A Mimi

A.K.A Mimi Ni Kitabu Cha Kumbukumbu Za Ngwea

Mwaka 2003 ndio mwaka ambao mtu mzima Mangwea aliingiza sokoni album yake ya kwanza "A.K.A Mimi" ikiwa chini ya Bongo Records kwa mkali P Funk.

Album ilisambazwa na "Gmc Wasanii". Hii ni miongoni mwa album kali sana kutoka kwa marehemu Ngwea. Album ilisimama sana kwa kubeba mawe 10 mazito.

Kabla ya kutoka kwa hii album marehemu Ngwea alitanguliza wimbo unaokwenda kwa jina la "Ghetto Langu", ni wimbo ambao ulifanya watu wengi wampe sikio pindi ulipotoka.

Na sababu Ngwea alianzia sehemu nzuri kwa P Funk watu wengi walijua kitakachofuatia ni album na sio kingine. Na kweli album ilifuatia ikapewa jina la "A.K.A Mimi".

Ukumbuke wasanii wengi ambao walikuwa chini ya Bongo Records walifanikiwa kutoa album kuliko ambao walikuwa chini ya label zingine.

Mawe yaliyopatikana kwenye hii album ni.

1. Mikasi ft. Mchizi Mox, Feruzi, Mkoloni, Rah P
2. Bado Nimo ft. TID
3. Dakika Moja ft. Noorah
4. Zawadi
5. She Got A Gwan ft.Dark Master
6. Weekend
7. Napokea Simu
8. Sikiliza ft. Lady Jaydee
9. Mademu Wangu
10. Ghetto Langu

"A.K.A Mimi" ni jina lililobeba hii album lakini huo wimbo ulikosekana ndani ya hii album ukaja kutoka baadaye kabisa.

Ngwair (R.I.P)

Wimbo uliompa jina na thamani ya juu Ngwea (R.I.P) ni hii "Ghetto Langu" wimbo ambao alizungumzia ghetto ambalo mpaka uhai unafika tamati sijajua kama alifanikiwa kulimiliki.

Wimbo wote alifanya yeye mwenyewe, yote ni kutaka kuonesha kwa uwezo wake yeye mwenyewe anaweza akatoa dude na likasumbua masikio ya watu.

Kibwagizo.

"Hii ni nyingine tena/
Ni Bongo Records tena/
P Funk/

Kiitikio

"Ni gheto langu tu/
Linalowachengua maduu/
Linalonipa chati ya juu/
K'nyama mpaka East Zoo/

Ni gheto langu tu/
Linalowachengua maduu/
Linalonipa chati ya juu/
K'nyama mpaka East Zoo/

Baada ya Kiitikio ndipo unakuja ubeti wa kwanza.

"Ngoja tuanze na hili la East Zoo/
Ukilicheki kwa nje liko simple tuu/
Ila ndani jirani kuna vitu flani/
Yaani, mi mwenyewe sometimes nalitamani/
Kapeti manyoya stuli meza kioo/
Kitanda nane kwa kumi
Marumaru mpaka kwenye choo/
Kimashine cha uzushi cha dry cleaner/
Chumba cha kati kuna studio ya kiaina/
Bafuni sink hakuna bali  jacuzzi/
Screen kila chumba tunacheki tu movie/
Ungo decoder mwendo wa Dstv/
Zinga la Tv na deck ya DVD/
Bonge la mziki linatwanga tu CD/
Na hakuna feni full time ni AC/
Na hilo ni la Dom tuu acha la Dar/
Home K-nyama wanachemba tunapokaa/"

Huu ubeti wa kwanza mtu mzima alivyosifia ghetto lake mpaka kufikia hatua ya yeye mwenyewe kulitamani ghetto lake mwenyewe mwishoni mwa ubeti anatukata stimu kwa kututambia hilo ni la Dom tu sio la Dar 😀😀

"Masela wanapenda kuja na mademu zao/
Nia yao waje kuwachapa nao/
Wakifika ndani wanaishia kuduwaa/
Mwishowe mida inaenda wanachemsha wanatambaa/
Mara kesho yake demu anakuja peke yake/
Eti anazuga anamtafuta mchizi wake/
ukimuelekeza kwake amfate/
Anadai eti amechoka anataka kidogo apumzike/
mkifika ndani haishi kukusifia/
Hata mchizi wake anaanza kumkandia/
Hujakaa vizuri ameshakukumbatia/
(Ooh) ndiyo maana mimi nawapigaga tu mikasi/
hata kisa cha kugombana na Evance/
ni aliponikuta ghetto na mdogo wake Nancy/"

Kwa ubora na sifa za ghetto mtu mzima kwake aliona kawaida kufanya mambo ya "katibu wa Mkandamizaji" kwa mademu wa masela bila noma.

"Yani Ghetto tu watu wanavyonipa heshima/
Sijui itakuwaje kama nitanunua na bima/
Linanukia mapafyumu ya kinyamwezi/
Na ma airfresh utadhani ghetto la Mase/
Nakupa laivu wala sijisifii/
Kama hauamini kamuulize hata P/
Au kama unawezq njoo mwenyewe mpaka home/
na Ukinikosa K-Nyama basi ujue niko Dom/"

Ubeti wa tatu ukafungwa kwa mtindo huo. Wimbo mwingine uliokuja kusumbua ni wimbo flani wa kuchezeka club unaokwenda kwa jina la "She Got A Gwan" akiwa na mwanachemba mwenzake Dark master

"Tukianzia uzuri tu/
She got a gwan/
Tabia, heshima, ndiyo doo/
She got a gwan/
Mpaka kwa ma sistaduu yeah/
Nabaki tu kusema ooh/
She got a gwan/

Tukianzia uzuri tu/
She got a gwan/
Tabia, heshima, ndio  doo/
She got a gwan/
Mpaka kwa ma sista doo oh yeah/
Nabaki tu kusema ooh/
She got a gwan/"

Kiitikio kinaonesha ni wimbo flani hivi wa kimapenzi na wa kuvutia masikio ya msikilizaji.

"Mara ya kwanza mi namuona, East Zoo’ Dodoma/
Ghafla nikajihisi kama mtu mwenye homa/
Kutoa salamu tu jibu lake ni noma/
Sauti yake tu nikajihisi nimepona/
Ndefu yake shingo, mwendo wa maringo (Oh oh)/
Nilifurahi aliponiambia yuko single/
Sio siri mtoto huyu ameumbika/
Na kama akipita’ mbele ya watu kumi basi, Nane kati yao lazima watababaika/
Hata hao wawili wivu tu umewashika/
Yessir’ kwa Ngwair ndo amefika/
Nami naapa kamwe sintomwacha/
Nina imani atanizalia mapacha/
Na hata kama bahati mbaya akiwa tasa/ Mi najua sintoweza kumuacha/
Na yote ni sababu tu/
She got a gwan/"

Kwa ubeti wa kwanza imefanya nitamani mimi mwenyewe nimuone huyu mwanamke ambaye madume nane wamebabaika na wawili waliobaki kwa wivu wakala kabunyau.

"Sintosahau mara ya kwanza ameniruhusu, ni mbusu, nitomase zake chuchu (Woo!)/
Naona fahari leo mpenzi uko na mimi, na hii naahidi milele nitakuthamini/
Sintojali ashatembea na wangapi/

kuwa nawe maishani naona bahati/
Kila unapopita masela unawadatisha, babaisha, wanabaki macho juu juu/
Wakuonapo ma duu, wanakasirika, kunja ndita
Wana benua midomo juu/

Najua yote hiyo ni wivu tu/
Washakuzushia mambo mengi tu/
Ila wewe ndio ma baby girl mmoja wa pekee/
Siwezi kuwa na raha bila ya kuwa na we/
Makosa naomba unisamehe, nataka kuwa na we,milele,oh girl/
You got a gwan/"

Upendo hauna kipimo kwa mtu mzima yeye alishazama kwa mrembo wake maneno ya katembea na wangapi sio kazi kwake kazi kwake ni kuwa na mrembo wake. Kisha Dark akaja kumaliza na hii,

"Nioneshe ulichonacho, ma/
Nioneshe zaidi ya nguo zako ulizovaa/
Nioneshe zaidi ya ngozi yako ya kung’aa/
Nioneshe kile ambacho kitanipa raha/
Girl you got a gwan, you’re my number one/
Nia yangu mi ni kuwa nawe maishani/
Chochote utakachotaka mi nitakupa, weka imani/
Nami naahidi kamwe wala sitokuacha njiani/
She got a gwan (Yes, i know!)/
Mama get busy, twende kwenye dance floor/
Unapokata kiuno matozi wanapagawa, nasikia sauti zao wakisema/

Na atakaye kushobokea mi ntamtoa duniani/
Na kuwanzia leo ntakuwa na tembea mi na gun (No)/
Naona milupo mi inaanza kunitamani, basi malizia kinywaji twende zetu nyumbani/"

Kwani Katibu wa Mkandamizaji alikumbuka hii kitu ya kutembea na gun ya Dark akaona azuge kimkwawa yasije kumkuta nini?

Wimbo mwingine tunaotazama ni huu "Sikiliza". Wimbo huu yupo na Jide, dada mkuu pamoja na Binamu Fa. Ni wimbo ambao uliwapa amsha amsha wanawake waweze kujituma na sio kubweteka kukaa kindezi.

Kiitikio [ Jide ]

"Kama ni dem sikiliza (nisikilize mimi)/
Kama una swali uliza (niulize mimi)/
Kata kama sijamalizaaa uliza/" x2

Beti ya kwanza

"Madem ninyi nisikilizeni kwa makini mimi/
Nyinyi hivi kwanini nyie mnakua hamjiamini/
Mnajua nyie yaani mna nguvu zaidi ya sisi/
Mwanaume kwa dem ni kama mfupa kwa fisi/
Sina nia ya kubadili maadili (siyo)/
Ninachopinga nyie kushikwa masikio/
Sema tu hamjui umuhimu wenu/
Ila leo nitawaambia tu ila iwe siri yenu/
Mi mwenyewe naenda club kila wiki/
Haina maana huwa nafuata tu muziki/
Nikiwa Church huwa napaona hapalipi/
Hata niwe na hela vipi na lundo la marafiki/
Vijijini ni asilimia 90 masikini starehe yao ni pombe na nyinyi/
Sasa mpaka lini mtakua mna nyanyasika, na kudharaulika/
Au wenyewe mmeridhika/
Kuolewa mna haki wala msiite bahati/
Hivi we unadhani wanangu mi nitalea na nani/
Sema tu wengi wenu ni vicheche/
Japo siyo moto ukuu na siogopi cheche/"

Ukisoma ubeti wa kwanza unaona hii inaweza kuwapa hamasa mpaka wadada wadangaji wa sasa ambao wamejaa drama za ajabu kwenye mishe za maisha.

Ubeti wa pili ni F.A

"Mfano mimi siamini kabisa mtungi/
Ukiacha mabinti siyo mineli siyo mirungi/
Ila nakosa imani nikiwaona mnajigonga/
Yaani hadhi yenu inashuka kimsimamo mnapo yumba
mnakosa nini kinachofanya msijiamini/
Au mwalimu wenu kipofu msemo na nyi mmeamini/
Msichimbe madini sawa, ila sio wote muwe wafanyakazi wa ndani/
Hesabu hazipandi, so ni ngumu kuwa rubani/
Ila japo karani nina imani haishindikani/
Big up kwa my mamy/
Na wote ambao computer imelala kichwani/
Sisemi mlee wanaume kama mabinti/
Ila mnapojitosheleza machaguo yanaongezeka
Hamuoni basi someni/
Kama uliishi vibaya, kwa mwanao irekebishe/
Wenye upeo mdogo ndo daima wanakua vicheche/
kuolewa siyo lazima
Japo inaongeza heshima/
Ina haja yake, hawatajali mke wa kigogo au mkulima/
na ole wenu msiopenda kutafuta vyenu/
Mnatamani tu vya wenzenu/
Ndiyo maana huwa mnamegwa na wazee wa umri wa babu zenu/
Nieleweni jikazeni/
Msipo komaa waume zenu watawaletea vicheche ndani/
Niamini Binamu B Yeah!/"

Binamu alimaliza kila kitu kwa hawa ambao kwa sasa wanaona ufahari kuwa single mama, naona hii itawaumiza sana kichwa endapo wakipita mstari kwa mstari. ubeti wa tatu anamaliza Ngwea mwenyewe.

"Kingine mnapenda sana vya kupewa/
Ndiyo maana wengi wenu mnaishia kuchezewa/
Mnamegwa mnaachwa
Na hata mkiolewa/
Ndoa inajaa visa na kuonewa/
Mfano Ngwear narudi muda ninaotaka/
Na ukiniletea kibesi tu asubuhi talaka/
Sinajua hauna kitu zaidi ya begi lako/
Ila nisingethubutu endapo nyumba ni yako/
Najua hamuwezi kwenda haja ndogo mmesimama/
Ila mnao uwezo wa kufanya kila sisi tunacho fanya/
Hata kuwa Rais mwanamke pia ana haki/
'mradi tu awe na vigezo wanaume tunapata wapi/
Kama kusoma wote ruksa kusoma/
Bado biashara hata ufundi wa kushona/
Wenzenu wachache bungeni simnawaona/
Hata kuimba imbeni tu wala msione noma/
Ka Sista P, Zay B, Stara, Ray C/
Je unataka kuendesha Prado kama Lady Jay Dee komando/
Amini wote tumezaliwa watupu/
Na kuvaa kutokana na juhudi tu za mtu/
Haaaaalllaah/

Ngwea alimaliza kila kitu na mpaka sasa tunae rais wa kwanza mwanamke.

Nyimbo nyingine ni "Mikasi". Wimbo ambao ulizua gumzo kubwa sana pindi ukiwa unaanza pale miguno ya mambo yenu inaposikika na kuna media flani zikawa zina mute ile kitu.

"Bado Nimo"

Wimbo ambao ulizungumzia gonjwa hatari la Ukimwi. Miaka ya nyuma ilikua kawaida sana kila album kukuta kuna wimbo mmoja ambao unazungumzia ugonjwa wa ukimwi.

"Dakika 1"

Wimbo ambao ulizungumzia mapenzi yani mtu anayetongoza anamuomba mdada japo dakika moja amsikilize.

"Zawadi"

Wimbo ambao unahusu ugonjwa wa ukimwi.

"Weekend"

Wimbo ambao unazungumzia bata za Weekend.

"Napokea Simu"

Wimbo ambao ulitumia biti la "Promota Ana Bipu" ambao ni wimbo wa Prof Jay Ft. Mkoloni. Hii P alitaka kuwaonesha watu kuwa biti ni mali ya producer sio msanii.

"Mademu Wangu"

Wimbo ambao ulizungumzia tabia mbalimbali za mademu na makabila yao yani tuseme Dulla Makabila kama alikopi hivi toka kwenye hii.

Kingine cha ziada humu Ngwea aliweza kurap na kuimba pia ndio kitu ambacho kilinogesha hii album na kuwa bora.