Album: Shahada ya Mtaa
Msanii: Mantiki Barz
Nyimbo: 20 na Bonus 3
Tarehe Iliyotoka: 06.11.2019
Utayarishaji: ABY MP (Multi-Purpose), De La Funky, Troo Funk, Kopollo

Shahada ya Mtaa ni album ya pili rasmi baada ya Tii Misingi Bila Shuruti(TMBS) ya msanii wa tasnia ya bongo hip hop toka Tanzania, Mantiki Barz ambae kitambo alikwenda kwa jina Logic.Albam hii imetengenezwa Digg Down Records iliopo Dar Es Saalam. Baada ya kuwachia nyimbo nyingi hapo awali, ikiwepo mixtape na EP Mantiki aliona mda umefika kujitambulisha rasmi kwa mitaa ya hip hop kwa kauachia album yake ya pili Shahada ya Mtaa.

Shahada ya mtaa ni album iliyo bobea kwa mistari na imeandikwa kwa umahiri na utunzi wa hali ya juu sana. Baada ya mwaka mmoja wa kuiskiza hii album nimeamua kutoa maoni yangu kuhusu hii album ambayo nitaichambua na kuidadavua ili tuielewe vizuri. Kama alivyo sema Fid Q, kwamba “Ielewe mitaa ikuelewe” basi hapa tutajaribu kuielewa Shahada ya Mtaa ili kumuelewa vizuri Jerry Muganda.

1. Shahada ya mtaa
Nyimbo ya kwanza kwenye hii album imebeba jina la album “Shahada Ya Mtaa”. Wimbo huu ulioundwa na producer ABY MP unaanza kuonyesha vile Mantiki Barz huanza siku yake na malengo ya kwenda mtaani kujitafutia rizki. Mantiki ni msomi mwenye shahada ila anatuonyesha kua unapokua mtaani pia lazma uhitimu upate Shahada ya Mtaa kwa kujifunza upya kuishi mtaani. Anaanza kwa kusema,

“Skia,alfajiri kumekucha/
Natupa shuka, najivuta,
Natoka kitandani tu na bukta, nainuka,/
Ghaflha kuna kitu nakumbuka/
Ya kwamba mi ni mja, nishukuru nikiamka/
Nazama kitaa, kama kichaa mweye dhiki/
Bila kutoka nyumbani mkono kinywani haufiki/
Jiko limenuna, hatukipi/
Ikumbukwe mii ni msomi ila kazi yangu muziki/
Elimu imenipiga, pigo sijiwezi,
Nguo zimechakaa, sipendezi,
Kulitafutia tumbo ndio kanuni elekezi!’

Hata baada ya kuhitumu kutoka chuo kikuu cha UDOM na Shahada ya Falsafa na Sayansi ya Siasa(Bachelors in Philosopy and Political Science), mtaa una muonyesha Mankiti kua lazma afanye juhudi ahitimu tena apate shada muhumi sana kuliko zote, “Shahada Ya Mtaa.” Mtaa unamcheka Mantiki ukimkumbusha kua elimu yake ya chuoni mtaani ni bure pale anaposema, “Elimu imenipiga, pigo sijiwezi.” Mtaa unamuonyesha Mantiki kua nadharia ya darasani haina chochote mtaani hadi imeanza kumfungua macho kua shughuli alizozidharua kama kilimo cha kupanda pembejeo ni muhimu mtaani kuliko cheti chake cha shule!

2. Yaliojiri – Imemuhusisha Meddy Molin
Mantiki barz kwa huu wimbo anatupeleka kwa safari yake ya elimu. Anatukumbusha enzi hizo alipojitoa mhanga kusoma kwa bidii ilikufikia malengo yake yakuitwa msomi. Anaanza wimbo kwa maongezi na rafiki yake wa mda mrefu na wanakumbushana walivyo soma pamoja enzi hizo wakiwa wadogo. Japo kua amesoma amebaki na majonzi maana anaona elimu yake sasa imemponza. Kazi hazipatikani, shahada yake ya chuo anaiona haina thamani na anaanza kujutia mbona hakufanya kozi ya Diploma au hata kuchukua somo linalohitaji cheti tu. Anashangaa kua rafiki yake aliefeli na aliewacha kusoma kapiga hatua kimaisha anaposema,

“Rafiki yangu habari zako zinavuma/
Mambo yako si mabaya, uko busy unajituma/
Una mke na watoto, nyumba na duka kubwa/
Pia una motokaa, kwa kifupi una fuba/
Huku ogopa maisha! Umethubutu na umeweza/
Mafanikio yako ki elimu ulipo teleza/
Sasa unafurahi, na pia unajipongeza/
Ninachoweza kukwambia mwenzako niliteleza!”
Anajutia kutokua na ujarisi wakujaribu kujiajiri na kushikilia uhahika wa elimu ulio mponza. Mstari huu, “Msomi bila pesa naonekana kituko/Mfukoni patupu sina buku, sina dusco!” pia unatoa kwa muktasahi hali ya vijani wengi waliosoma ila hawana chochote cha kuonyesha bali kupiga makasia kwenye matumbwi ya dhiki!

3. Mungu Wangu akimshirikisha J-Oncer
Mara kwa mara tunapopitia changamoto za maisha hua tunahisi kua pengine tumemkosea mwenyezi Mungu. Wimbo huu aliomshikirisha J-Oncer ni kama maombi ya Mantiki anapo pitia changamoto za maisha. Na J-Oncer anaonyesha unyenyekevu kwa mwenyezi Mungu kwa sauti yake anapoimba kwenye kiitikio,
“Uniepusha kwa mambo haya (Napiga magoti Mungu wangu)/
Hujanipita kwa kila jambo (Asante sana Mungu wangu)/
Hii sauti napaza isikike, napiga goti mbele zako/
Shukrani za dhati zifike, mwokozi unajua tabu zangu/
Naaminiii…”
Utunzi bado ubo juu na ndani ya mada ya Shahada ya Mtaa na bado Mantiki anatukumbushia changamoto za kuwa msomi na kuajiriwa kwa kusema,
“Najiita mfanya kazi ila ki ukweli ni mtumwa/
Namtumikia bepari nimechoka naenda nyuma! / ”
Kujiajiri kuna changa moto, kuajiriwa maji ya moto?

4. Nilipotaka kuoa akimshirikisha Yeyo
Abby MP bado anaendela kuonyesha umahiri wake wa vyombo kwenye wimbo huu ambapo Mantiki baada yaku “hustle” mtaani anaamua mda umefika kuweka jiko nyumbani.Mantiki alitaka binti mwenye vigezo hivi,

“Nilipotaka kuoa nilihakikisha nina mwenza/
Maana raha ya ndoa sio umpate unaye mpenda/
Yule aliyejitoa katika dhiki na fedha/
Hata kama una chongo yee anaona una kengeza!”

Kama chochote kile maishani maamuzi ya kuoa yalikua na changamoto zake ambapo washikaji wake wakamwambia kua ndo ni nusu ya kufa ila yeye hakufa moyo bali akaamua kuendelea na maamuzi yake. Ila kwa haya yote anatupa tahadhari kua pia mwenza ni binadamu na ana mapungufu yake pia.

5. Galacha akimshirikisha Waafrika
Mantiki kwa wimbo huu akaweka gea namba tano utunzi wake ukiandaliwa na dereva Kopollo na kuanza kutukumbushia kua yeye ni Galacha; mtu hodari na anaye jiamini ili aweze penya maisha yetu ya mtaani.

Anakua mwalimu wa historia na anaanza kutukumbusha mengi yalio tokea nyuma ili tuweze pata dira tusije potea. Tanzania ambayo ni nchi yake alipozaliwa anatukumbushia kua,

“Kwenye miaka ya tisini, nchi moja masikini/
Masikini kabisa tena wa kima cha chini/
Wenye rasilimali, mbuga nyingi na madini/
Wenye serekali iso wajali lakini/
Itikadi ya kijamaa ndio imani walio iamini! /
Muasisi makini kabla ya kufukiwa chini/
Chini kwa chini, kuna wadudu yamkini, /
Vifo vya mashujaa futi sita ardhini!”

Akiendelea kutukumbushia kua maisha ni safari anachukua chaki na kutufunza vile historia huficha mashujaa wa kweli kwenye historia zetu akichukulia Afrika Kusini kama mfano kutuonyesha vile tumemsifia sana Mandela na kusahau akina Chris Hani na Steve Biko. Kwa huu wimbo mwalimu Mantiki anakua na hasira na historia inavyo waficha watu muhimu sana na kusifia wachache!

6. Wasalaam akimshirisha Fivara
De La Funky anachukua usukani kwenye safari ya mtaani kwenye wimbo huu ambao ameshirikishwa Fivara ambae ni tuluthi moja iliobakia ya kikundi cha Ngome ya Chuma. Wanaenzi wanafamalia na marafika wao walio tutangulia mbele za haki. Tarumbete zinapiga kwenye beat kama ile wengi wanao amini wanaisubiria siku za mwisho.Anaingia Mantiki na kuanza kumkumbuka mamake akisema,

“Skia, eyo salaam, najua umepuzika/
Imepita miaka kumi tangu nilipo kuzika/
Sauti yako inaskika, hakika inafahamika/
Najua ungefurahi sana kumuona Dicta! /
Ungemuona Tina ungefurahi mama yangu/
Mngeongea mengi, vitimbi vya watoto wangu/

Vesi la Mantiki limejaa majonzi akimkumbuka mama yake alie kufa takibran miaka 11 na japo kua mama yake alikua anafanya shughuli za mama ntilitie, Mantiki anajivunia alivyokua aikijutama kwa ajili ya watoto wake.
Fivara haaachwi nyuma anapochukua doria kwenye vesi ya pili naye anamuenza kakake akisema,

“Nakusalim kaka, Tafari ndugu yangu/
Pole na safari, sijui ushafika ndugu yangu? /
Anaendelea kwa kumuuliza hali ya wazazi kule kuzimu na kumpa ripoti za mtaani na vile wanavyo parangana na maisha hapa duniani. Shahada ya Mtaa inaonyesha kua hata kuzimu mapambano yana endelea.

7. Mara Ya Mwisho
Mantiki anarudi tena akishirikiana tena na Abby MP wakiendelea kuenzi walotuacha kwa kukumbuka mara ya mwisho alipokua na watu hao. Anachora taswira halisia ya siku ya mwisho wakati mtu nafsi inapo mtoka anaposema,

“Mara ya mwisho alikua hoi taabani/
Amekata kauli, inamtafuna saratani/
Ndugu hatutambui, yani kama hatujui/
Amerudia utoto, haja zote kitandani kwenye bodi zake…”

Wimbo huu unatuelemisha umuhimu wa kuenzi watu tuwapendao na kukumbuka matendo mazuri ya watu waliotuacha.
Kando na haya tunajifunza kiswahili mbadala cha mtaani anaposema,” alichomoa betri” kumaanisha alifariki/aliaga dunia/ alikufa!

8. Kabla Hujalaa akimshirikisha Waafrika
Mtaani kuna wanaume na wanawake na kwa wimbo huu Mantiki anashirikiana tena na Kopollo kuongea na akina dada zetu. Sauti ya Waafrika kwenye beat alilounda apollo imenoga sana. Mantiki anampigia dada flani na kujitambulisha rasmi na kumwambia kua yeye ni MC anaye elimisha jamii. Ana anza kumpa elimu,

“Kumradhi, najua haujapenda hii simu/
Unahisi unapoteza, nakurushia stimu/
Uko resi na maisha, hivyo inakulazimu/
Kujiweka sokoni, kisa pesa taslimu…/”

Anamtia moyo dada kwa kumkumbusha japokua anapitia changa moto nyingi maishani kua “hadhi yako dada iko juu, juuu, usijishushe thamani!” Wimbo huu ni mbiu ya mgambo toka kwa Mantiki kwenda kwa akina dada kuwa, “she’s the number one!”

9. Nisamehe akimshirikisha Waafrika
Maisha ni shule na mara kwa mara kama vile mwanafunzi shule hatuna budi kukosea wakati tunapojifunza. Hivyo basi Mantiki anatukumbushia kua kuomba msamaha kunatakiwa kuwa kitu cha kawaida. Japo kua ameshamkosea mpenzi wake mda mrefu bado anamsistizia asisite kumsamehe maana mapungufu ni ya ki ubinadamu.Anasema kua kakosea hadi hajui aanze vipi kuomba msamaha ila lazma apate maneno yakujieleza,

“Umeshanisamehe mara nyingi/
I’m speechless, sijui nijitetee vipi/
Eti mnaongea kipi, nikuimbie mziki/
Na vile uko humble, nikuletee pipi?”

Kwa haya yote pia anasistiza kua pia kuna mda msamaha huja na adhabu kama anayo mpa mwanae Dicta ambae ametajwa mara kadhaa kwenye nyimbo za Mantiki.

10. Dada yake Baba akimshirikisha Yeyo
Wimbo huu ulioundwa na Kopollo umeonyesha umahiri wa Mantiki kuchukua historia ya maisha na kuandika wimbo wenye unaonyesha taswira kamili la chimbuko lake. Ni wimbo wake bora kwangu mie binafsi.

Kando na mama yake mzazi, Matiki Barz anaonyesha vile shangazi yake alicheza pakubwa kumlea. Huu wimbo hata shangazi alipo lala lazma atahisi upendo na heshima anayopata hadi sasa toka kwa Mantiki.

Mantiki anasema kilicho mfanya awe karibu na shangazi yake baada ya wazazi wake wawili kufariki. Anakumbuka,

“Mpaka mama anakufa ananikumbusha alimwambia, /
Wifi mimi naondoka ila Jerry nakuachia/
Uhai nautamania ila wakati umewadia/
Najua utamsaidia awe baba wa familia/
Anaendelea kwa kusema, “Namshukuru Mungu, shangazi akanitwaa/ Kwa afya na maradhi hajawai nikataa/.

Yeyo nae kwa kiitikio alibariki nyimbo hii kwa sauti ambayo lazma ilimfikia shangazi popote alipo.

11. Nyota Tano akimshikirikisha Stereo
Funky producer De La anarudi tena hapa kwa nyimbo ambayo Mantiki anamshirikisha mtoto wa Africa (African Son) Stereo (Singa Singa). Huu wimbo unakutanisha ma Mc wawili ambao wanataka kujionyesha wako mahiri na makini na uchanaji wao. Wote wanataka kuonyesha nani ana mistari.

Kwa heshima na taadhimba Mantiki ana muachi bro Stereo aanze na hachelewi kuonyesha kwanini amedumu kwenye gemu anaposema,

“Oya mwana kaa kichwani hauja settle, basi pole(sana)/ Unachoweza basi niku battle na Shilole (Shissy baby)!”
Mantiki nae hawachwi nyuma anaposhika kipaza nakusema, “Bars na flow nazishusha bila deadline/Kichwani timamu sina ganja wala red wine!”
Producer De La Funky, Stereo na Mantiki wote walisimama kwa zamu zao wakati walitakiwa wawe imara.

12. Kama Muafrika
Mantiki Barz anapanua wigo wa mawazo hapa anapo ongelea kuhusu mama yetu Afrika. Ame sample viongozi wa Afrika kwa nyimbo hii wakiwepo mahayati Robert Mugabe, Thomas Sankara na PLO Lumumba wa Congo. Anaongelea changamoto za sera za kigeni zinazo nyemelea bara letu kama vile ushoga na usagaji na anazipinga vilivyo. Anasistiza umoja wetu kwa kusema,

“Hatupaswi tengana sisi, tuishi kwa amani/
Tuipuuze mipaka ya mkoloni kwa ramani!”
Anakashifu wanaopenda kuenda kuishi ugaibuni ilhali hapa nyumbani tuna kila kitu. Wimbo huu ni funzo kuhusu kujitambua kua muafrika thamani yake ipo juu na asikubali kuonewa.

13. Heshima ya Mtaa akiwashirikisha Rabi James na Slogan
Kilaa mtu ana kitaa anacho toka sawia na Mantiki pamoja na Rabbi James ambaa wote ni tuluthi mbili n ya kundi lao la Ngome ya Chuma. Pia ameshirikishwa Slogan. Kila mmoja anatoa heshima (homage/respect kwa kimombo) kwa mitaa iliyo wapa elimu na walipo hitimu kama anavyo sema Rabi,

“Rabi ni msanii mchenguaji/
Mc, Mtaa ninayo ishi imeshanivika taji!”
“Heshima ya mtaa, vile wana tuna kaa ni safi tuna maintain!”

14. Jerry
Kwa wimbo huu Mantiki anataka tumjue yeye kiuhalisia ni nani, anata tujue kua yeye ni “Jerry”. Mdundo wenyewe umeunda na Abby MP na chemistry yao inazidi kuonekana hapa wanapo fanya kazi tena pamoja. Mistari inayo kuonyesha japo kua Jerry ni msanii amehitumu na Shahada ya chuo bado ni mwanafunzi anaye tatufa Shahada ya Mtaa anaposema,
“Nimehitimu, japo elimu haina mwisho!”/ Naendelea jifunza, nisomapo kila tigo.”

15. Mr. DJ

Kwa wimbo Mantiki anaongelea maisha ya kijana mmoja DJ na changamoto ya kazi yake. Kupitia wimbo Mantiki anaongea kuhusu gonjwa la kisasa linalotusumumbua kwa sasa na vile DJ alivyo pata huu ugonjwa baada ya kubadilika ghafla alipopata senti kidogo akikumbuka,

“Hata mi nilikuambia kua huyo manzi ana moto/
Kaungua ndio mana hakunyonyesha hata mtoto/
Kashatumika sana na kagawa kila chocho/
Ukamuona mpya nao walitupa kama kopo/
Mara kifua kina sumbua sumbua ghafla/
Ukaona si vibaya ukienda kujua afya/
Ukajipalia makaa, ulidhani nini sasa/
Dalili zilionyesha una ugonjwa wa kisasa!”

Yote kumi Mantiki anasisitiza umuhimu wa kupima na kuto wanyanya paa waathirika.

16. Nje ya Muziki
Track hii iliyo undwa na De La Funky inaanza kwa sauti za mingurumo ya radi pengine zikiashiria mvua ya mistari atakayo achia Mantiki kwenye ngoma hii akitaka kutuonyesha maisha ya Mantiki Barz nje fani hii. Anaendelea kutuonyesha kuna tofauti kubwa kati ya “Jerry” na Mantiki. Anasema yeye pia ni mtu wa kawaida anapo andika,

“Nje ya mziki mi ni baba, mi ni mume/
Nimezaliwa mwanamme, sina budi niji tume/
Nazidi kuimarika, hata mkiniundia tume/
Familia inanibariki, nalindwa na mitume!”
Mantiki anasisitiza usimkariri kua unamju kisa na mana unajua mziki wake. Yeye ni zaidi ya mziki na kazi zake. De La aliua beat hapa.

17. Siku Moja; akimishirikisha Richie 99

Je Shahada ya Mtaa ingekamilika bila kuongelea changamoto ya mihadarati kwa mfano “Cha Arusha” mitaani? Vesi ya Richie 99 anaelaza kwa ucheshi kilicho mkuta alipo piga puff moja cha kilinge na maruerue yalivyomfika,

“Nikaskia mpaka sauti za king’ora/
Mara nimekua katuni wa kuchorwa/
FIFA wamenipa tuzo muigizaji bora/”

Au alisema vizuri vile marijuana ilimuhamisha nchi bila pasipoti,

“Haya ndio maajabu ya Rizla/
Akili ilikua Vatican, mwili ukabaki Sinza!
Goli keeper nilijihisi kama winga/
Nikafanya yaku shangazi kama mgumba kapewa mimba!”

Mantiki Barz alimshirikisha mtunzi wa beat Troo Funk alioandaa beat hili Old School ambalo waliliua kinyama pamoja na Ritchie 99.

18. Usisubiri Serikali; akimshirikisha Bokonya
Super sub kawaida huingizwa dakika za mwisho kwenye soka ili kubadili matokeo. Na kwa wimbo huu ambao ameshikishwa Bokonya “The Super Sub” Mantiki anasistiza umuhimu wakujitegemea mwenyewe badala ya kutegemea serikali. Kiitikio kina hamasisha vizuri kinapo tuambia hivi,

“Usisubiri serika ikutatulie matatizo/
Usiwe tegemezi, acha hizo/
Mafanikio yanaletwa na wewe/
Usipo hangaika unajichelewesha mwenyewe!”

Pia Mantika anaongea kitu kimoja muhimu sana kwa wakati wetu anapotukumbushia kuhusu marehemu Akwilina Akwilini aliposema,

“Usisubiri kuwaskia wakiruhusu maandamano/Japo ni haki yako ila Akwilinaa ni mfano.” Akwilina ka enziwa vyema, apumzike pema peponi.

19. Chama Langu; akimshirikisha DLH
Chama Langu ni shout out ya vitu anavyo thamina Mantiki Barz maishani mwake kwa mfano mziki wa Hip Hop, team yake ya nyumbani Simba pamoja na team yake ya ughaibuni Totteham Hotspur FC. Chama lake ni familia yake na mashabiki wake wanao nunu kazi zake. Anafurahia sana kuzungkwa na chama lake la uhakika wakiwepo studio iliyo muwezesha kutoa hii album yake, Digg Down Records.

20. Acha Shule; akimshirikisha Small Lethal na DLH
Msanii Small Lethal toka Kenya alibariki track hili na kuonyesha kua Kenya na Tanzania wanaheshimiana ki muunagano wa Africa Mashariki na zaidi pia ki Hip Hop. Kwenye traki hii wanashirikiana kuonyesha vile shule ya mtaani ni muhimu pia au zaida ya shule shuleni!

“Acha kuskiliza nadharia/karibu mtaani ujifunze uhalisia wa hii dunia!” ni msisitizo kua Shahada ya Mtaa upatikana kwa vitendo.
Shahada Ya Mtaa ina track tatu za Bonus ambazo zinakamilasha album hii iliyojaa elimu na hekima. Karibu mtaani.

Ukitaka albamu hii wasiliana na Barz