Wiki hii tutaanza rasmi na makala yetu ya kwanza inayoangazia Beat Tapes ambazo nimepata mda kuziskiliza na ningependa mashabiki wa mziki wa Hip Hop waweze kuziskia pia. Lengo la makala haya ni kupata fursa ya kuangazia kazi za watayarishaji wetu ambao mara moja moja huachia kanda za midundo kwa ajili ya uskilizaji wetu.

HR The Messenger - Chocolate Chops Vol 1

HR The Messenger ni mtayarishaji anayefanyia shughuli zake kule Ongata Ronga Kenya na amepiga kazi na wasanii kibao nchini Kenya kama vile Fikrah Teule, Monski, Wakadinali, Danytox Intronix na Lord Arnold.  Mtayarishaji huyu anapatikana pale Philosophy Recordz. Pia tulishawai fanya mahojiano nae hapa Micshariki Africa.

Kando na HR kuwa mtayarishaji wa midundo yeye pia ni emcee aliewahi kushinda tuzo za Hennessey Hip Hop Unkut Awards kwa mradi wake uitwao Reign.

HR The Messenger aliachia mradi huu wa midundo mapema mwaka huu 2022 mwezi wa Februari baada ya shamrashamra za Valentine’s Day kama zawadi yake kuja kwetu ya kuadhimisha siku hii ya wapendanao. Beat Tape imesheheni midundo ya Lo-Bap yaani mchanganyiko wa mdundo wa Lofi na Boombap.

Midundo niliyoipenda: Let Go, Heights, Camp Fire

Mcheki HR kupitia;
Facebook: Njuguna HReinassenace Kimemia
Instagram: hr_the_messenger
Twitter: HR The Messenger

Kunta Official Beats – InsTruthMentals (Vol 1)

Kunta Official Beats ni mtayarishaji wa muziki na msanii kutoka Nairobi, Kenya. Alianza safari yake ya muziki akiwa msanii wa Hip Hop akiwa bado katika ujana wake. Utayarishaji wa muziki mara zote ulikuwa wa shauku kwake mara tu alipopata kurekodi kazi yake ya kwanza katika studio ya muziki. Mtayarishaji aliyejifundisha mwenyewe, amekuwa akifanya biashara hii ya muziki kwa muongo mmoja uliopita, ambapo amekuwa akiendeleza ujuzi wake wa uzalishaji.

Ametayarisha rekodi za wasanii tofauti kutoka kote ulimwenguni: Kenya, New York, Tanzania, Jamhuri ya Dominika, New Jersey, Ugiriki, Afrika Kusini, Uhispania, South Carolina na wengine wengi. Kwa hiyo ana uzoefu mkubwa kwa upande wa uandaaji midundo na alifanikiwa kuanzisha lebo yake ya utayarishaji inayojulikana kama Kunta Official Beats. Mnamo Oktoba 2020 alitia saini mkataba na Lebo ya Hempire Word Wide nchini Afrika Kusini. Hivi majuzi alipata pongezi kwa sababu ya midundo yake kutoka kwa KRS ONE.

Anafafanua mapigo yake kama InsTruthMentals anapokusudia kusema Ukweli kwa akili/akili za watu. Kutolewa kwa InsTruthMental juzuu ya. 1 na 2 ililenga kuonesha kazi yake kwa ulimwengu.

Midundo Niliyoipenda: Resistance, Kremlin, Sundown, Never Love Again

Taarifa kutoka kwa Kuna

Producer Kunta yuko katika harakati za kutoa beat zake za 2019-21 zilizowekwa alama (tags) za #InsTruthMentals kutoka kwa maktaba yake.

Iwapo unahisi kuwa wewe ni msanii unayestahili kupewa midundo hii au unamfahamu mtu anayestahiki kupewa midundo hii tafadhali cheki nae.

Ps: Anasambaza beats bure.
#KuntaOfficialBeats

Mcheki Kunta Beats kupitia

Facebook: Kunta Kinte Mcs
Twitter: kuntanakinte
YouTube: Span1Kunta
Email: kuntakintethemc@gmail.com

Aby Bangladesh – Music For My Friend$

Aby Bangladesh ni mtayarishaji wa muziki aliyejikita kwenye midundo ya Hip Hop na Soul na wakati mwingine RnB. Aby ni producer anayepatikana kule Morogoro Tanzania kwenye studio inayojulikana kama Digital Vibes.

Aby Bangladesh anasema hivi kuhusu  beat tape hii, “Beat Tape hii Music For My Friend$ ina historia kidogo. Ilikuwa ni mwaka 2015 kama unavyoona kwenye picha ya makala tulikuwa studio ya marehemu Big Boss pale Kinondoni Dar. Tulikuwa na akina Teknohama, Nikki Mbishi na watu wengine kibao tukirekodi albam ya Teknohama iliyoitwa Technologia kama sijakosea. Naam tulikua tuko pale kama familia sehemu moja tumetulia na kujifurahisha na ndio ile picha ikapigwa.

Kwa hiyo for my friends ni kama ilikua dedicated kwa Big Boss japokua mradi sikuuita kwa jina lake ambaye yuko kwenye ile picha bonge hivi. Na majina niliyoyatumia kwenye midundo yangu  ni majina ya washkaji zangu. Kwa hiyo mtu ambaye yupo kwenye ile picha ila si mshkaji wangu sikumuandika kwenye beat tape tracklist hayupo.”

Midundo Niliyoipenda: Teknohama, S.O.N.G.A, Msouth, Boyka, Malle

Kuwasiliana na Aby Bangladesh mcheki kupitia;

Email: abybangladesh@yahoo.com
Tel: +255 717 778 341

Sela Ninja – Chiulu Beat Tapes

Sela Ninja anajulikana rasmi kama Christopher Robert Kasela, ni mzaliwa wa Chimala Tanzania. Sela alianza  kujifunza beat production kiujumla baada ya kupata ugumu wa kulipia studio session kipindi ambacho alikua bado mwanafunzi. Hali hii ilipelekea yeye kujitahidi kujifunza production kila ambapo alipata wasaa hadi akafika sehemu watu walipoanza kumtafuta kutokana na kuvutiwa na baadhi ya kazi zake.

Hadi sasa amefanikiwa kufanya production kwa watu tofauti maarufu pamoja na wasiokuwa na majina. Chiulu Beat Tape ni beat tape ya nne baada ya

  1. Street Blessing
  2. Black Is Beautiful na
  3. Tutu Bee

Sela Ninja anasema kuwa amekuwa na mfumo wa kuweka Beat Tape baada ya kupoteza beat zake ambazo hazijatumika zaidi ya mara tatu katika nyakati tofauti. Chiulu Beat Tape ni tape yenye beat 20 zenye mahadhi ya Hip Hop.

Kwa sababu Hip Hop kwa Sela Ninja ni utamaduni sio muziki hivyo kupelekea 99% ya kazi zangu kuwa za mlengo huo lakini ninatengeneza beat za namna tofauti ama aina tofauti ya muziki kulingana na mahitaji husika.

Midundo Niliyoipenda: Horn 222, Wajinga Sisi, Huyu Mtoto Ndio Yule Bibi, More222, Nawekeza_Belazoene Kemp Instrumental, Never222, Jikazeni, Rip Budha Temp, The General, Unrecognised

Wasiliana na Sela Ninja kupitia

Email: selaninja@gmail.com
Tel: +255 625 603 701
Facebook: Babu La Mababu
Instagram: selaninjaofficial

Sheem King – Project Bangers - Instrumental Mixtape

Sheem King ni emcee/producer anayepatikana Mwanza, Tanzania. Mtayarishaji/emcee huyu ambaye jina lake halisi ni  Hashim Yusuph Mwanja huyu yupo vizuri tukija kwenye maswala ya uchanaji pamoja na udundishaji.

“Nimetengeneza angalau beat tapes 5 na kutoa nyimbo za wasanii wa handaki kama vile Fivara, Ambecal, Macavasco, EscherBoi, HansDope, na wengine wengine.

Kanda mseto na midundo yangu mingi imetiwa moyo na marafiki zangu wa karibu ambao wana ndoto sawa na zangu na mojawapo ni kuona muziki wa Hip Hop wa handaki ukipiga hatua kwa kujaribu kuwafanya watu waelewe ni nini…”

Midundo Niliyoipenda: Awe Instrumental, Estrellita Hip Hop Boom Bap Sampled, Soul Search, Bars n' Nasty

Wasiliana naye kupitia:

Facebook: sheemking
Instagram: Sheem King Dopeboi Certified

Kama wewe ni mtayarishaji na una Beat Tape ambayo ungependa tuweze kuiskiliza na kuwashirikisha  waskilizaji wetu wasiliana nasi kwa kututumia link za miradi yako hapa: WhatsApp: +255765714824 pia ziambatane pamoja na taarifa kidogo kuhusu wewe kama producer, shughuli zako na mradi unaotaka kutushirikisha.