Tumerudi tena na msururu wa makala zinazoangazia Beat Tapes toka kwa watayarishaji wetu kutoka Africa Mashariki. Baada ya kuwapatia Micshariki Africa Beat Tapes Alert (First Edition), nilipata mda wa kuskiliza miradi ya watayarishaji kadhaa na hii hapa ripoti kamili yenye nia na malengo ya kukuhabarisha kuhusu ma producer wetu na mapishi wanayotuandalia wakiwa jikoni na kisha kutupakulia kwa njia ya Beat Tapes.

Wise Geniuz – WG’s Vol 1 Hip Hop/Rap (Tanzania)

Wise Genius ni mtayarishaji anayepatikana kule Mbeya Tanzania ambaye nimekubali utayarishaji wake baada ya kuskia kazi za kwanza kwenye album ya Pizzo Madawa  - Panga Mbili na kisha kubahatika kumsikia kwenye miradi ya wana Hip Hop kibao. Kwenye makala yaliyokua na mahojiano yetu mwaka jana alisema hivi Wise Geniuz kuhusu baadhi ya miradi aliyoiandaa yeye,

“Orodha ya baadhi ya miradi niliyofanya (albums, mixtape na eps) ni Siku Njema album-Yunani Empire, Loyal To The Truth album-SAWINA, Njia Sahihi Ep-Nala Mzalendo, Utu Na Watu Ep -MentalityMionzi album- X-Ray Vina, Panga Mbili- Pizo MadawaPenda Unachofanya- Sajo MC, Gang Kubwa-Maujanja Saplayaz, Akili Kichwani Ep, Trickson Knowledge x Nala mzalendo, Dreams- Lugombo MaKaNTa ( washiriki wengine wa hii ni Hayati Burn Bob [R.I.P], 10th Wonder, Old Paper na Dabo.)”

Soma makala kamili hapa.

Mapema mwaka huu WG aliachia beat tape yake ya kwanza rasmi ambayo tumeona ni vyema tuwashirikishe pia ili muweze iskia.

Midundo niliyoipenda: Mmmh, The Guitar, Tears, Ain’t That, The End, Hold On, Jury, Let it be

Mcheki Wise Geniuz kupitia;

Facebook: Wise Genius (MD)
Instagram: Wise_Genius_WG
Twitter: Wise Geniuz

Duke Tachez – 2021 Beat Tape (Tanzania)

Legendary underground Hip Hop producer Duke Tachez ndio mtayarishaji wa kwanza kuachia beat tape mwaka huu(natumia kumbuku za Micshariki Africa). Duke Tachez ambaye anafahamika rasmi kama Duke Gervalius ameanza utayarishaji wa mziki kutoka mwaka 1988 na amejikita sana kwa uandaaji wa mziki wa Hip Hop.

Kwa wale ambao ni wapenzi wa Hip Hop kindakindaki nina uhakika lazima mtakua mnafahamu baadhi ya kazi alizoziandaa yeye zikiwemo kazi za wana TamaduniMuzik na kadhalika. Pia hapa Micshariki Africa tulifanikiwa kuchambua moja ya kazi zake akiwa na emcee Bokonya ijulikanayo na Beat and Rhymes EP Vol 1 .

Ni baraka kuona Duke bado akitubariki na beat tape hii ambayo inakuonesha kuwa bado anazidi kutuandalia midundo kwa ajili ya ma emcee pamoja na mashabiki. Ipeni skio lenu hii tape.

 Midundo Niliyoipenda: Ngoma hazikuwa na majina kwani zimewekwa kama mix flani.

Facebook: Duke Tachez
Twitter: DukeTachez
Instagram: Duke Gervalius
YouTube: Duke Tachez

Mohjay Da Producer – Mohstrumental Beat Tape (Vol 55) (Kenya/Germany)

Binafsi mimi sikuwahi kumfahamu mtayarishaji Mohjay Da Producer kabla ya mwaka huu nilipofanikiwa kunasa baadhi ya midundo yake pale YouTube. Kitu nilichokiona moja kwa moja ni kuwa mtayarishaji huyu  anamkubali sana mtayarishaji J Dilla.

Katika hali ya kumtafiti mtayarishaji huyu niliona kaandika hivi Mohjay kumhusu pale SoundCloud,

“Mohjay aka MohTeachin ni msanii wa hip hop anayekuza amani, haki kiuchumi na kijamii. Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 10 kama meneja wa talanta, mhandisi wa sauti, mtayarishaji, mkurugenzi, na mbunifu wa picha.

Miradi na uharakati wake unaojali kijamii ni pamoja na ushirikiano wa kimataifa, filamu za hali halisi, ukuzaji wa hafla za hisani na usimamizi.

Miradi ya haki ya kijamii ya Mohjay ya “MohTeachin” ni pamoja na “Talent Beyond Bars: Kamiti Prison Cypher” Initiative, “Ivy Kenya – Orphanage & Children’s Center” inayojitolea, mfululizo wake wa mafundisho wa “Freestyle Walk: Art Of Sampling”, na “Pwani Vina: Hip Hop Hookup" ukuzaji wa tukio.

Mohjay alizaliwa (Limuru) Nairobi, Kenya, na ameishi Mombasa, pia anatumia muda nchini Tanzania, na Uganda.

Kwa sasa anaishi Hanover, Ujerumani.”

Midundo Niliyoipenda: Ngoma hazikuwa na majina kwani zimewekwa kama mix flani.

Mcheki Mohjay Da Producer kupitia;

www.https://mohjaydaproducer.com/

Jeraw Beatz – You Know The Vibes (Kenya)

Mtayarishaji Jeraw Beats kutoka Kenya inawezekana hili jina ni geni kwenu ila kama wewe ni shabiki wa mziki wa Hip Hop kutoka Kenya kuna uwezekano ushawahi kuskia moja ya kazi zake lakini hukujua yeye ndio alikuwa nyuma ya ngoma ila. Kwangu mimi binafsi nimeshangaa na idadi ya ma emcee aliofanya nao kazi kama vile Wakadinali, Steph Kapela, Asum Garvey, Das Walanguzi, Poppa Don, Collo (Kleptomaniax), Breeder, Elisha Elai, Shukid, Hozef na wengine wengi.

Check beat tape yake hapo chini kisha anza kufuatilia kazi zake kama ulikuwa umfahamu mtayarishaji huyu.

Midundo Niliyoipenda: You Know The Vibes, Jerrawbeatz Kazuntight Westcoast, Legacy Ish Boombap, Take One Boombap, Found Truth Boombap

Facebook: Jeraw Beatz
Instagram: jerawbeatz
YouTube: Jeraw Beatz

Ares 66 – Shovel Business Vol.2 (Boom bap Edition) (Kenya)

Unaposkia jingle inasema “Big Beats Afriq” jua kuwa studio na mkono wa mtayarishaji Ares 66 imehusika kwa kazi uliobarikiwa kuiskia.  Ares 66 ambaye alianza maisha yake ya muziki kama emcee mzuri tu alifanikiwa kujifunza na kuwa mtayarishaji mkubwa anayepatikana kule Umoja, Nairobi na amehusika pakubwa kutuletea vipaji vikubwa vya Hip Hop nchini Kenya kama vile Khaligraph Jones, Wakadinali, Dyana Cods, Sir Bwoy na Elisha Elai pia.

Pia amefanya kazi na ma emcee kibao kama vile Oksyde, Kayvo Kforce, P-Tah Wa Furu, Fena Gitu na wengine kibao. Inapokuja kwa miradi ya wasanii ndio usiseme maana amehusika pakubwa kwenye uandaaji wa album ya kwanza ya Khaligraph Jones, Testimony 1990 pamoja na miradi kibao ya Wakadinali ikiwemo Ndani Ya Cockpit 1 na 2 na nyingine nyingi.

Leo mchanaji huyu aliyegeuka na kua beat maker ametuletea midundo moto moto kutoka kwa misururu ya ma tape ya midundo iitwayo Shovel Business. Hapa nimewaletea Shovel Business Vol.2 (Boom Bap Edition). Karibuni msikie kazi hii hapa

Midundo Niliyoipenda: Grind, Cuba Liqour, Kubwa, Slide

Wasiliana na Ares 66 kupitia:

Facebook: Ares SixtySix
Instagram: r.s.sixysix
Twitter: Ares 66

Kama wewe ni mtayarishaji na una Beat Tape ambayo ungependa tuweze kuiskiliza na kuwashirikisha  waskilizaji wetu wasiliana nasi kwa kututumia link za miradi yako hapa: WhatsApp: +255765714824 pia ziambatane pamoja na taarifa kidogo kuhusu wewe kama producer, shughuli zako na mradi unaotaka kutushirikisha.