Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards (April 2022): Trabolee

Tuzo ya nne ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards (April 2022) tumemkabidhi Trabolee kwa ajili ya ngoma zifuatazo; (Ma Li Za Ro Ho, Rafiki Pesa, Rangi Zingine, The Healing).

Trabolee anaendelea kunadi mradi wake mpya alioshirikiana na mtayarishaji Akili Blaq, “Ma Li Za Ro Ho (1NE)” ambao pia tuliuchambua hapa. Kufanikisha hili emcee huyu ameweza kuachia video nne kutoka kwenye orodha ya ngoma zinazopatikana kwenye album hiyo. Video zenyewe ambazo zinakuonesha bayana kuwa TRA ni ART na kuwa ubunifu wake hauishii tu anapokua studio bali hata anapoandaa video zake kwa ajili ya mashabiki wake.

Ngoma iliyobeba jina ya album yao Ma Liz Za Ro Ho ni moja ya ngoma aliyoachia kichupa simple lakini chenye ubunifu sana. Unatamani mali za roho au unataka malizaroho?

Wimbo mwingine toka kwa album hii ambao pia una video ni The Healing ambao unaongelea maswala ya uponyaji katika nyanja zote za kimaisha; kiakili, kifedha, kiafya, kidini, kisayansi, kimawazo, matibabu kwa ajili ya vitu vikubwa na vitu ambavyo ni vidogo vidogo ila ni muhimu vitibiwe.

Rafiki Pesa pia iliundiwa video flani tofauti sana. Anakwambia Trabolee,

“It’s the root of all evil when you don’t have it/
Make it turn savage/
Alafu when you grab ka Ruto utasema “Money never made me happy”/
Money makes a dope rapper wanna stay average/
Make you act like a vegetable just to get cabbage/”.

Changamoto za kuwepo na kutokuwepo na senti.

Wimbo wa mwisho ambao umetuwezesha sisi kumkabidhi emcee Tra tuzo ya mwezi April 2022 ni Rangi Zingine ambao ni wimbo unaotuhamasisha sisi watu weusi kujipenda kwani kila kitu huanza na kumalizika kwenye weusi.

Hongera sana kwa Trabolee akisaidiwa na mtayarishaji Akili Blaq kwa kuchukua tuzo ya mwezi April 2022.