Adam Shule Kongwe

Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards (July 2022): Adam Shule Kongwe

Adam Shule Kongwe amekuwa busy sana mwaka huu wa 2022 kutupatia kazi nzuri za Hip Hop zinazoburudisha na kutuelimisha pia. Mapema mwaka huu aliachia mradi wake wa kwanza ambao ulikuwa ni kandamseto kwa jina Chi ilhali mwezi jana aliachia EP yake ya kwanza Kutoka Kwangu Kuja Kwenu (K.K.K.K).

Kando na miradi hii emcee huyu amekuwa busy akishirikiana nasi katika darasa letu la Shule Na Shule ambapo amechana kuhusu mada tofauti tofauti. Mada ambayo aliyoigusia majuzi kati mwezi Julai ilikuwa ya Usalama Na Afya.

Kwenye wimbo huu emcee huyu alijitwika jukuma la mabwana OSHA(Occupational Safety Health Authority) na kuhamasisha hadhira kuhakikisha kuwa kwa kazi yoyote ile wanayoifanya iwe ni ya kuajiriwa au kujiajiri au hata shughuli za nyumbani au mashambani cha kuzingatia kwanza ni usalama na afya ya mhusika na watu wanaomzunguka. Pia wimbo huu wa Usalama Na Afya kazini ulitumia michoro ili kuweza kuonesha matukio tofauti tofauti yaliyokuwa yanatajwa hapo.

Kazi hii ilifanyiwa utafiti wa kina ili kuweza kuleta jumbe zilizoshiba madini ya usalama na uwasilishaji wake pia ulikuwa ni rahisi na mzuri kwa mtu wa kawaida kuelewa kilichokuwa kinachanwa hapo.

Hongera sana kwa Adam Shule Kongwe kwa kujinyakulia tuzo yetu ya saba ya mwezi July 2022 ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards.

Pakua/Download Wimbo Huu Hapa!