Nuru Mturu

Tuzo ya nane ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards (September 2022) tumemkabidhi Nuru Mturu (Mama)

Uzuri wa kuchimba handakini ni kuwa hujui ni madini gani utakutana nayo. Na hili nililidhihirisha pale uchimbaji huu uliponifikisha hadi Chuga na kupata fursa ya kuskia kazi za emcee toka kule ambaye hapo awali hata sikuwahi kumfahamu wala hata kuskia kazi zake.

Nuru Mturu mwezi jana kazi yake ilifika kwangu kwa mara ya kwanza na alichonipakulia mezani ni kibao chake “Mama” ambacho kama anavyosema kwenye utangulizi wa wimbo huu aliu dedicate kwa akina mama wote duniani. Kazi hii ambayo ki mdundo ilisimamiwa na Wise Genius na kwenye final mixing and mastering pamoja na vocal za kiitikio alisimama mnyama Double ilikuwa kazi ya kiutaalam sana.

Bi’ mkubwa heshima kwako kutoka kwa mwana Hip Hop Nuru Mturu na wana Hip Hop toka Africa Mashariki.

Hongera sana kwa Nuru Mturu kwa kujinyakulia tuzo yetu ya nane ya mwezi September 2022 ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards.

Pakua ngoma hii hapa! Download this track here!