
Tuzo ya pili ya Micshariki Africa Emcee Of The Month Awards tumemkabidhi Kanambo Dede kwa ajili ya wimbo wake Walahi.
Kwenye wimbo huu emcee huyu chipukizi toka kule Kayole, Nairobi, Kenya aliamua kutusimulia stori ya maisha yake ili tuweze kujifunza kitu kwa kumtumia yeye kama mfano akichana na kuwasilisha vyema mashairi yake juu ya mdundo mzuri.
Ama kweli wahenga hawakukosea waliposema, “Ujana maji ya moto” kwani kupitia wimbo huu Kanambo anaweka wazi changamoto za ujana zilizomtoa kwenye reli kama vile shinikizo la rika (peer pressure), mimba ya utotoni, utumiaji wa mihadarati pamoja na kutotii wazazi wake kulivyo mpeleka pabaya hadi akajiunguza na hayo maji moto.
Kupitia wimbo huu pia tunaona umuhimu wa msamaha; umihumi wa kujisamehe, umuhimu wa msamaha wa mzazi na umuhimu wa msamaha wa jamii. Msamaha huu ndio unamuwezesha binti huyu kupata fursa ya kuanza maisha upya baada ya mamake kumsamehe, kumchukua na kumsaidi mwanae hadi anapojifungua mtoto baada ya Kanambo kugundua na kukubali makosa yake na kujirudi.
Ni kupitia msamaha huu ndipo Dede akapata fursa ya pili ya maisha na kuweza kutuonesha kipaji chake baada ya kusaini mkataba wake na King Kaka Empire alipo onesha uwezo wake mara ya kwanza kwenye kipindi kimoja pale YouTube kwa jina Street Vybez.
Hongera kwa Kanambo Dede, emcee wetu mwezi wa Februari 2022.
Beti Ya Kwanza
(Kaka Empire is the lifestyle)
Nilikuwa naishi Kayole/
Nikapigwa ball nikarudi kwa mokoro/
Sina hata form sijui kulea mtoto/
Pesa kidogo matumizi nazo mob jo/
Riba ni zangu zinatrend kwa masoko/
Alipata ball na alikuwaga mono/
Sasa mtoto amepata mtoto/
Na burden yote imeland kwa mokoro/
Wanauliza nani ako responsible? /
Ni fala flani I don’t like talking about/
Rewind from the top nikushow vile ilistart/
After ryma nikaingia seco/
Mama aka nyc atleast ako na hope/
It’s a good start for a first born/
Nilibambika coz I was at another level/
Stori ya Bio na Chem hatuwezi nego/
Sikuwanga into studies tangu kitambo/
Backbench jeshi yangu jeshi ya mambo/
Ma homies wangu wote ni ka ma psycho/
Party after party hakuna kurudi home/
Mathe akadai that’s it am on my own/
Nikabidi niende ghetto kusaka form/
Kamau wa Thufu ndo alikuwa my first boss/
Mi na swao nawatibu hangover ya ng’ango/
One day from work nikafika home/
Nikapata roommate ameteka huyu boy/
Okey okey.../
He’s hot lakini ni ka hana form/
Day one day two kijana haendi kwao/
To cut the story short alishapataga hao/
Before we even see it tushakuwa family/
Nishapata shem to me he is just a friend/
Mwenyeji akazied akaniacha na mgeni/
Alichoka maisha ya ghetto ye hawezani/
Lakini hakumedi ananiacha na nani/
With a stranger under one roof/
Raha nani nakwambia ni ka movie/
Ya Hyena na meat meat/
Dubs alicheat na mimi/
Siogopi kusema coz I ain’t sorry/
Ikakuwa big deal am the bad bestie/
Akaeka beef si kidogo ingine real/
Wakarudiana nikakuwa bunny/
Wakaachana akarudi side hii/
Kijana ako na lugha nikashindwa kuresist/
One big mistake problems begin/
Kwa Kamau wa Thufu nilikuwa Nisha resign/
Nikaenda kwa mathe department ya cham/
The beauty and the lazy mi ndio nalipa bills/
Si wananiambia nimuache siskii/
Nika amenitepa things/
Am very fertile na ye anacheza fiti/
Nikaacha job am very dizzy/
Mara oh am sleepy, didn’t know am risking/
Mwenye nategemea he is more than lazy/
Nikazoea njaa na kuhandwa na malandi/
One morning am yawning/
Kalonje hana kicks ujue ni ngori/
Naitisha za mashuksha ananishow jo nichill/
That’s it am done with this shit/
Narudi home hope mathe atani forgive/
Makosa nilifanya si ati nilikill/
So kenye nafanya nita pack and leave/
Najua si rahisi lakini huko ndo ngamani/
Nilibreak her heart vile nilikataa kustudy/
Ubaya ya maji ikimwagika haizoleki/
Mapenzi ya mathe real ting haifichiki/
Akanikubali msamaha tukaishi/
9 out of 9 siku hainaga utani/
25th ngware one akakam in/
My son am a proud mummy/
God hizi ni blessings, haha…/
Kiitikio
Kadi sikucheza right/
Lakini Wayne apate kidish walai/
Soon nicheki kwenye flight/
Lakini now mnifunze kufish walai/
Walahi ooh walahi/
Walahi ooh walahi/
Kadi sikucheza right/
Lakini Wayne apate kidish walai/
Soon nicheki kwenye flight/
Lakini now mnifunze kufish walai/
Walahi ooh walahi/
Walahi ooh walahi/
(The beat killer)