Tuzo ya kwanza ya Micshariki Africa Emcee Of The Month tumemkabidhi Lugombo MaKaNTa kwa ajili ya wimbo wake Gangsta.
Kwenye wimbo huu Lugombo katumia sitiara, ucheshi, kejeli, masimango ili kuweza kutuonya kuhusu jambazi hili sugu linaloishi nasi na mbinu zinazomuwezesha kutukandamizi na kutumiliki.
Ujasiri uliotumika kuchana kuhusu jambazi huyu ambae tunaishi nae si kidogo. Kinaya ni kua maisha yetu yanamtegemea sana huyu Gangsta ili yaweze kusonga mbele!
Hongera kwa Lugombo MaKaNTa, emcee wetu wa mwezi wa Januari 2022.
GANGSTA_LUGOMBO (LYRICS)
BBC once agaaaiiiin! (BBC Jingle)
Intro (Lugombo)
(Me I'mma Gangsta!!! You don't wanna f**k with me!)
Me I'mma Gangsta, You don't wanna f*k with me, You don't wanna f*k with me!
Unless you gotta die tonight! Unless you wanna die tonight!
Me I'mma Gangsta, You don't wanna f*k with me, You don't wanna f*k with me!
Unless you wanna die tonight! Unless you gotta die tonight! GANGSTA!!
Beti Ya Kwanza
Mnapanga foleni, shida zenu kunililia/
Nawapanga tokeni, nikiwaahidi kuwasaidia/
Nawageuka nawaibia, mali zenu najilimbikizia/
Mimi ni Gangsta, sio chaguo kunivumilia/
Mimi ni Gangsta, wengi mnanisujudia/
Wanaobusu pete yangu, uhakika kufanya biashara/
Wanaofuta viatu vyangu, sio rahisi kupata hasara/
Wanaotamani kiti changu, nilishawatoa kafara/
Madaktari, Maprofesa mbele yangu hawaishi wasi/
Miaka tele nawatesa, nikipingana na sayansi/
Hahah! Hamjanijua vyema!
Tega sikio pengine unaweza pata, some "secrets"/
Sitaki kusikia fikra za "Galileo" na "Socrates"/
La sivyo Guantanamo Ukonga, nakupatia chumba/
Ukibisha umeyumba, nakumbushia Patrice Lumumba/
Nina siri nyingi hamnigusi hata kwa sumu na ndumba/
Nakula na Magangsta uchwara, Dili zao zisijevumba/
Mi ni!..Mi ni!...Mi!...(Stuttering....)
Mi ni GANGSTA!
Chorus
Mimi ndio siri, Mimi ndio mkali/
Mimi ndio mwenye Mali, Mimi sirikali/
Mimi ni Gangsta, unaepata hofu kunizoea/
Mimi ni Gangsta, dakika sifuri umepotea/ X2
Beti Ya Pili
Uoga wako, muhimili kwa biashara yangu/
Ujinga wako, muhimili kwa utawala wangu/
Hakika hauna chako unaishi, kwenye Mali zangu/
Nakuonesha picha si kamili hubishi, unaikubali/
Wanaonijua kiundani, wanaweweseka kunitafakari/
Labda kama hujui, usiku kwangu ni kama mchana/
Inawezekana hujui, kuhusu wasiojulikana/
Ukweli naamua Mimi, uongo naamua Mimi/
Najua wengi hamuamini, pingeni nikate ndimi/
Usisahau niliamua lini, wangapi watabaki mjini/
Nyinyi sio ndugu zangu, na sina rafiki wa kudumu/
Na hamjawahi kunichagua, Nina mbinu za kudhulumu/
Bingwa wa kuzuga, Mimi kondoo Mimi chui/
Hekima na upumbavu, Mi Nyerere Mimi Nduli/
Mpole na Mbabe, Uhuru mi' Magufuli/
Mimi ni Gangsta, Marekani Mi' Urusi/
Chorus
Mimi ndio siri, Mimi ndio mkali/
Mimi ndio mwenye Mali, Mimi sirikali/
Mimi ni Gangsta, unaepata hofu kunizoea/
Mimi ni Gangsta, dakika sifuri umepotea/ X2
Beti Ya Tatu
Endelea kunisikia tu, kwenye vyombo vya habari/
Usiombe yakukute, Mashuhuri hawana Hali/
Jukwaani walikuuzia chai, walikuuzia asali/
Ili uje unipinge leo kwao mambo sio shwari/
Nakuwinda kwa risasi, nakuchinjia getini kwako/
Mazishi nasimamia, na nailisha familia yako/
Eti miili imeokotwa ufukweni, hamjacheki msituni/
Mimi ndio naruhusu mfanye yenu, nyie wahuni/
Naamrisha ndugu zenu, wawatupie mabomu ya machozi/
Na ikibidi wawatupie jela tu, nyie matozi/
Mnanipigia kelele za uhuru na Demokrasia/
Wakati wote sisi ni wezi, ila hakuna anayenifikia/
Kuleni kwa kamba zenu, Mimi sijali hata mama zenu/
Hakuna wa kunighasi, nimeshikilia uhai wenu/
Msipokomaa wavuja JASHO aisee mtajifia/
Nishaanza kuchukua kodi ya pumzi, Hamjanishtukia?/ Hahah! Mimi!
Chorus
Mimi ndio siri, Mimi ndio mkali/
Mimi ndio mwenye Mali, Mimi sirikali/
Mimi ni Gangsta, unaepata hofu kunizoea/
Mimi ni Gangsta, dakika sifuri umepotea/ X2
Bridge (Spoken and sang)
Mbishe msibishe! Mnanihitaji!
Na sitaki kusikia kelele "ng'woo ng'woo sisi Maskini Katika Nchi Tajiri!!! Mimi Sina shida! Eeh Sina shida kabisa! Sina shida ya Umeme, Sina shida ya nishati, sijui matibabu!!!
Me I'mma Gangsta, You don't wanna f*k with me, You don't wanna f*k with me!
Unless you gotta die tonight! Unless you wanna die tonight!
Me I'mma Gangsta, You don't wanna f*k with me, You don't wanna f*k with me!
Unless you wanna die tonight! Unless you gotta die tonight! GANGSTA!!