Toka kwa: Momumo
Wimbo: Ishi Leo ft Majanta, Dwise, K Mapacha
Albam: Hisia
Tarehe iliyo toka: 15th December 2020
Watayarishaji: Patrino
Mix & Mastering: Burnbob (R.I.P)
Studio: MaKaNTa Jr. Records
Beti ya Kwanza
Sipo mwanzo sipo kati na sijafika kwenye nukta/
Nipo kwenye huu wakati muda wote unanipata/
Wengi tunaishi Kwenye wakati Uliopita/
Visasi Ubishi, Na Kushabikia Vita/
Matusi Kwa maandishi, ni marudio Hakuna jipya/
Huku Tunaishi, Hakuhitaji Kupotoshwa/
Hayazoleki Haya Maji Yakishamwagika/
Huwezi rudisha tumboni, Chakula Ulichotapika/
Ni Kama Imani, Ikivunjwa inavunjika/
Yani Mfano wa Glasi, Haijirudi Ikivunjika/
Punguza Wasiwasi, Haya Yote yanapita/
Bado una nafasi ,ishi Leo ishi sasa/
Tunaloweza fanya Leo, Tusisubirie Kesho/
Ya Kesho hatujui, Japo mipango ipo/
Tusihubiri Uadui, Tupendane ngali tupo/
Kama muda ndo huu, ndo huu wakati Special/