Momumo kama linavyo maaanisha jina lake, ni kijana, emcee na mwanafamilia wa Hip Hop anaependa kuunga mkono hoja chanya za maendeleo kwenye familia, jamiii na sanaa. Momumo ni mmoja wa wanafamilia ya MaKaNTa(Maskini Katika Nchi Tajiri) wanao patikana Mbeya. Leo tumepata fursa ya kufanya mahojiano nae.

Karibu Momumo, kwanza naomba nitajie majina yako kamili?

Majina ni Emmanuel Issaya.

Momumo ni jina linalotoka katika lugha ya kibantu (Kinyakyusa) likiwa na maana ya, sawa kabisa, hivyo hivyo, au ndivyo ilivyo kwa maana ya kuunga mkono hoja ama jambo fulani. Unaweza kutuambia ni sababu zipi zilikufanya ujiite hivyo kwa kuhusianisha na utamaduni wa Hip Hop?

Momumo inatokana na asili ya kabila langu Nyakyusa kama ulivyosema. Nilianza kutumia jina la Paya kabla ya Momumo, ambalo lilikuwa jina la biashara zangu za sanaa, wateja niliokuwa nawauzia tshirt ndo walioanza kuniita Momumo, na ndipo ilipotokea Momumo Paya.

Ulianza lini kujihusisha na utamaduni wa Hip Hop....na ngoma yako ya kwanza kurekodi ilikuwa mwaka gani?

Nimeanza kujihusisha na Hip Hop mwaka 2006 na ngoma yangu ya kwanza nilirekodi 2007.

Na kwanini ulipenda kuwa katika maisha ya utamaduni wa Hip Hop na si maisha ya utamaduni mwingine?

Sababu Hip Hop inawakilisha maisha nnayoishi...na kuguswa kwa ujumbe uliopo ndani ya Hip Hop.

Unafahamika kama balozi mzuri wa utamaduni wa Hip Hop toka katika kundi la MaKaNTa. Je ulijiunga lini na kundi hilo na ni kwa sababu zipi?

Nilijiunga na Makanta 2016 na sababu kuu ni upendo na support waliyonipa toka narekodi "Bado sijaona". Pia Nilipenda uwakilishi wao kwa jamii.

Mpaka sasa umeweza kuachia kazi ngapi kama Momumo? Pengine una mawazo ya kuwa na mradi wa mixtape au album hivi karibuni?

Kama Momumo nimeachia kazi 3 nazo ni No doubt na Asante na album yangu ya kwanza HISIA.

Toka 2006 mpaka sasa ni miaka kumi na moja imepita, je ni mafanikio gani umepata kutoka kwenye utamaduni huu wa Hip Hop?

Mafanikio niliyopata ni kwamba nimejifunza vitu vingi kupitia utamaduni huu pia nimejenga madaraja ,kufahamiana na watu wenye mawazo chanya... Ambao wanazidi kunijenga kila siku.

Nje ya mziki unajishughulisha na kitu gani ili kujikomboa kimaisha? maana Hip Hop ya handakini wengi wanasema hailipi

Nje ya muziki mimi ni mbunifu, mchora machata, pia najihusisha kuchapisha T-shirt, caps pia ni afisa masoko mtarajiwa.

Nimesikiliza nyimbo zako ulizoweka katika akaunti mbali mbali za mitandao ya kijamii, nikagundua kuwa umetumia midundo ya watayarishi kutoka ughaibuni ilihali kuna watayarishaji wengi tu bongo hii kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Unaweza kutuambia ni sababu zipi zilikusukuma wewe kufanya hivyo?

Nyimbo nilizotumia midundo ya watarayishaji wa nje ni mbili tu ambapo nina nyimbo zaidi ya 6 nilizotumia midundo ya watayarishaji wa ndani(Tz). Ni kutokana na kuvutiwa na kazi walizofanya, midundo mizuri huwa ina ni inspire kufanya kitu kizuri. Pia ni midundo niliyokuwa naitumia kabla ya kuingia studio.

Mtozi gani anayekuvutia kufanya naye kazi?

Ni Chizan Brain, P funk, Bin Laden, bila kumsahau producer wangu Patrino.

Imezoeleka na ni kawaida sana kwa wasanii kuingia katika sanaa ama kujihusisha pindi baada ya kuvutiwa na watu kadhaa wavumao kupitia wafanyacho. Kwa upande wako ni akina nani waliokuvutia kwa kuanza na nyumbani mpaka ughaibuni?

OK... Navutiwa na wasanii wengi kwenye huu utamaduni, sababu napenda kujifunza kwa kila nnaemsikia... Ila kwa Tz aliyeni-inspire ni kaka Salu Tee, Lugombo, Prof. Jay, Sugu. Ughaibuni ni Nas, 2pac, Smif n Wessun, J.Cole, Fashawn.....na wengineo waliofanya kazi nzuri.

Kundi la MaKaNTa (Maskini Katika Nchi Tajiri) lina memba wangapi ? Je memba wote ni wachenguaji?

Kundi la MaKaNTa lina members zaidi ya 15(tukijumuisha na Makanta Jr's. Wote sio wachenguaji, wengine wapo kwa ajili ya ku support ,pia kusaidiana majukumu mengine. Pia MaKaNTa ni zaidi ya kundi... ni familia Lugombo, Adamoe, Jadah, Sigga Nyota, Tovuti, Mkolosae, Momumo, Ezdon, Chedah, (MaKaNTa Seniors) bila kumsahau Samicho.

Unazungumziaje juu ya wanaoitazama Hip Hop kama uhuni?

Hip Hop sio uhuni, kuna vitu vingi nimejifunza kwenye Hip Hop zaidi ya nilivyojifunza shule. Hip Hop ni zaidi ya darasa.

Je unatumia kilevi ama kivuto chochote katika utayarishaji na uwasilishaji wa utamaduni huu? Kama ndio kinakusaidia kwa asilimia ngapi? Maana wengi uhusisha vitu hivyo na matatizo ya kifikra katika Hip Hop.

Katika Uwasilishaji, situmii kilevi ...I am me 100%
Matumizi ya kilevi hayasaidii chochote kwenye uandishi, ni hobby ambayo ni personal na haihusiani chochote na utamaduni huu......

Upi ni mtazamo wako juu ya miaka michache baadaye ukiwa kama mwakilishi wa utamaduni huu?

Mtazamo.... Ni kuwa mbali zaidi ya hapa, nipate fursa ya kufikisha ujumbe kwa watu wengi zaidi.

Ni muda mrefu sasa upo katika tasnia hii, unadhani ni changamoto zipi zinakukabili?

Changamoto zipo nyingi na huwa haziishi ila kikubwa ni imani na kujua unachotaka ni nini kwenye kitu unachofanya nachukulia changamoto kama inspiration ya kufanya zaidi ya leo, na sio kikwazo cha kukatisha tamaa.

Pamoja sana mzee, labda ungemaliza kwa kutujulisha maoni yako kwa chipukizi, wasanii waliopo handakini na jamii kwa ujumla

Amini unachofanya, na fanya kwa usahihi...Hakuna kinachoshindikana, ukiamini umeweza. Pia tujiongeze kwa kusoma na kujifunza kila siku...Hip Hop ni maarifa "Mshike Elimu Usimuache Aende Zake ". Usifuate mkumbo, sababu fulani anafanya hivi amefanikiwa basi na mi nifanye…

Isikilize nafsi yako, ndipo usikilize wenzako its natural...
Kwa kuongezea nilianza kupiga ngoma kanisani nikiwa na miaka 8, pia kuchora nimeanza nikiwa na miaka 6, so it was written brother, this is my passion, its where my heart is....Toka nimeanza kufuatilia huu utamaduni, kadri nnavozidi kuchimba nagundua nilikua ndani ya misingi since way back, I love Hip Hop sababu inaniruhusu nijielezee pia kufikisha kile kinachohitajika na jamii.

Tueleze kidogo kuhusu shughuli zako za sanaa na uchoraji. Ulianza vipi na mpaka sasa umekua kiasi gani?

Nimeanza kuchora bado nikiwa shule ya msingi. Nilianza kuchora comics, watu wengi walikua wanapenda sana na ndio kilichonifanya kuanza kuwa designer na kufanya logo za kwenye t shirt na hata ku print nilikua natumia mkono mwenyewe.Changamoto zipo ila hizi ni njia moja wapo ya kutufanya tukue zaidi ila changamoto ni kama daraja la kutufanya tusonge mbele zaidi.

Mbona uliamua kuweka albam zako zote kwenye platform za streaming kama vile Boomplay?

Niliamua kuachia albam zangu zote mbili kwa mashabiki kama zawadi ambao walikua wamekosa nafasi ya kuweza kulipia na kupata nakala ya albam hizo. Albam hizi zipo Boomplay peke yake.

Ni njia ipi unaipendelea kwa kusambaza kazi zako za mziki, kumuuzia shabiki mmoja mmoja baada ya mawasiliano nae au kuweka albam kwenye streaming apps?

Njia ninayo penda kuitumia ni kumuuzia albam shabiki yangu moja kwa moja baada ya kuwasiliana nae. Kwenye streaming apps mtu akishasikiza na angependa kua na copy basi anakuja ili nimuuzie ila sio kwamba albam zote nitakuwa naweka huko, hapana kwani mpaka sasa hivi sijafikiria kuweka albam nyingine kwenye streaming platform.

Unaona kuna manufaa gani au changamoto gani zinazokuja kwa kutumia mbinu hii kuwapatia mashabiki zako mziki?

Changamoto ni kwamba miziki yetu ni mizuri ila hatuna exposure kubwa au watu wa kutosha kuweza kuwafikia na kuwauzia kwa sababu hiyo ya kuuza mmoja mmoja inalipa zaidi kuliko kwenye streaming platform. Kwahiyo mtu akisikiliza kule sawa hela inaingia ila sio kama ile ungeipata kama ungekua unauza albam moja moja, yani one to one kwa mteja wako.

Je unapoweka mziki pale hua unalipwa au bila bila?

Kuhusu kulipa, ndio wanalipa japo siyo ki hivyo ila wanalipa. Streaming zinavyozidi kua nyingi, senti nayo inazidi kuongezeka. Ila kwa pale mtu anaweza kuiskiza ile albam tu ila hawezi baki na nakala ila akihitaji albam ananicheki mimi pia namuuzia, copy anabaki nayo.

Pia mziki wa streaming apps unalipwa kila baada ya miezi kadhaa kwa mfano quarterly. Yani ni hivi, ukishafikisha hela kadhaa unaruhusiwa kuchukua hiyo hela yako, kwa hiyo malipo yapo, ndio.

Mtu akitaka kupata kazi zako anafanyaje ili zimfikie kwa wakati

Anaweza kunifuata kwenye mitandao ya kijamii ambapo atapata links zote za nyimbo zangu.

Aminia sana,pia shukran kwa time yako. Much respect kwa MaKaNTa

Facebook: Momumo Machata (Momumo Paya)
Instagram: momumo_
Twitter: MomumoPaya
YouTube: Momumo