Wimbo: Siku Njema
Msanii: Monaja
Tarehe Iliyotoka: 10.07.2020
Watayarishaji: Shaky Aloyo/Monaja
Mixing and Mastering: Shaky Aloyo
Studio: Angaza Studios
Monaja
Kiitikio
Imekuwa muda mrefu/
Wasi wasi kwa nyoyo zetu/
Mwisho wa usiku mrefu/
Ntaona siku njema, siku njema/
Kila juma ni mkosi/
Imani yangu haitoshi/
Sijamaliza machozi/
Ntaona siku njema, siku njema/
Beti Ya Kwanza
Mc flani alidai uchungu ni mwanzo wa kupona/
But ni hufanyika shida zingine zikianza kugonga/
Kabla upate nafuu imagine kusota time ya ugonjwa/
Imagine keja ‘ko kubomolewa wajunior wako wakiona/
Na ni time ya mvua unajua na kuna ugonjwa wa kuambukiza/
Imagine raiya kulindwa kwa makarau kuwapiga/
Ibidi ujijazie hii gava haijali zetu maisha/
Naezakushow imagine but hizi vitu zote zishafanyika/
Matha na wajunior wake kufungiwa keja juu hawakuweza/
Lipa rent ya miezi mbili so kwa mjengo flani wakajiweka/
Mjengo haikuwa imemalizwa alafu usiku flani kukinyesha/
Kulia kwa watoi ilileta rende yenye ilimbaka na kumtesa/
Matha mwingine alikosa dough akalazimika kuchemsha mawe/
Alikosa kitu ya kumanga njaa kutesa wanawe/
Hiyo kuchemka wafikirie ingefika time kudema wamange/
ilifka baadaye lakini huyo matha alipoteza mwanawe/
Kiitikio
Imekuwa muda mrefu/
Wasi wasi kwa nyoyo zetu/
Mwisho wa usiku mrefu/
‘taona siku njema, siku njema/
Kila juma ni mkosi/
Imani yangu haitoshi/
Sijamaliza machozi/
Ntaona siku njema, siku njema/
Beti Ya Pili
Ilikam na ndege tukalaumiwa ni ka si tuliubuni/
Kumbuka waafrika wakivurugwa China kufanya watake kurudi/
Gava ikatetea China kulaumu mraiya kimaksudi/
Juu kutekwa nyara na madeni kukanyagia haina budi/
Hii ukoloni mamboleo itaendelea hadi siku za uso-/
Ni dunia yote watu weusi wataumizwa kwa mbinu ya fujo/
Kwa nywele ngumu rungu inakuwa ni ka jibu la fumbo/
Magava kutumia kifua kwa watu hawana kitu kwa tumbo/
Na wanatoa amri zao kutoka watu weusi wenye wana ganji/
Security yao wakiiba kutoka mraiya mwenye hana mali/
So makeja Ruai na Bangu zilibomolewa kuivisha mradi/
Ya madongera wanaotawala tunajua hao ni kina nani/
Na hii-gonjwa kutumika kifumba macho wakichoma/
Picha zao mraiya zikiumia mafuriko wakioga/
Na hii ngoma dedication kwa Walibora/
Na wasanii wenye wanaota juu ya siku njema wakichora! /
Kiitikio
Imekuwa muda mrefu/
Wasi wasi kwa nyoyo zetu/
Mwisho wa usiku mrefu/
Ntaona siku njema, siku njema/
Kila juma ni mkosi/
Imani yangu haitoshi/
Sijamaliza machozi/
Ntaona siku njema, siku njema/
Beti Ya Tatu
Ngori yenye tunapitia imetuonyesha venye kuna ubinafsi/
Ma source kununua bidhaa supaa bila kitu kubaki/
Hizi mikopo kutoka nje zikitafunwa kwa ulafi/
Hata zilikuwa misaada za kutuokolea huu wakati/
Wengine kupiga siasa ni ka wamepata nafasi/
Kujipanga kabla kura na miaka mbili zimebaki/
Na hao ndio leaders zetu enyewe mraiya hatuko lucky/
Enyewe hatuna kismat enyewe hatuna bahati/
But even though tunapitia mabaya ndani ya roho kuna imani/
Na hata ka ni kidogo hiyo kidogo tunahitaji/
Itafika time ya si kukumbatiana na wazazi/
Bila si kuwaambukiza walai bila hiyo wasi wasi/
Mask zetu zifungue, nafsi zetu zipumue/
Anga zetu zifungue wakati wetu ndio ikue….siku njema/
…Najua tunapitia mengi saa hii but yatapita/
Hata hiyo kawaida tulizoea haifai kuwa kawaida…/
Lazma tupambanie siku njema, haitafanyika bila si kuijenga/
Lazima tupambanie siku njema, haitafanyika bila si kuijenga/
Lazima tupambanie siku njema, haitafanyika bila si kuijenga/
Lazima tupambanie siku njema, haitafanyika bila si kuijenga/
Siku njema, siku njema, siku njema, siku njema, siku njema, siku njema, siku njema, siku njema/