Uchambuzi Wa EP: Gorilla
Emcee: Msito
Tarehe iliyotoka: 03.07.2022
Nyimbo: 8
Watayarishaji: 32 Records, Kunta Official Beats, Dandora HipHop City (DHC),
Mixing & Mastering: Kunta Official Beats, El Shado
Studio: Msito Music
Nyimbo Nilizozipenda: Gorilla 1, Kinaga Ubaga, Weh Ishia, Street Life, Gorilla 2, Sura Punda, Taratibu, Rada Safi, Each 1 Teach 1
Msito ni emcee chipukizi ambaye binafsi sikumfahamu ki vile hadi pale nilipokutana naye kwa mara ya kwanza kule Dandora nilipokuwa na mshkaji wangu Kinaya ni kuwa kukutana naye mara ya kwanza kulituwezesha sote kwenda hatua moja mbele inapokuja kwa utamaduni wetu huu wa Hip Hop.
Msito ambaye alianza kuchana tangu utotoni alishawachia ngoma kadhaa enzi hizo na Dandora Music, Looking Up pamoja na Back In The Days. Hivyo wakati tukikutana naye alikuwa kwenye harakati ya kuandaa mradi wake wa kwanza ambao ni EP aliyoiachia mapema mwezi July kwa jina Gorilla.
Gorilla ilitambulishwa kwa mashabiki na wimbo Street Life ambao ulikuwa singo ya kwanza toka kwa EP hii ambao unaongelea maisha yake ya kitaa na changamoto zilizomkuza. Msito akichana ki utu uzima anasema,
"Zile noma nimepitia mi hukimbia shinda gear/
Day to day siwezi tulia hope success ziko near/”
Hii ndio kama kauli mbiu utakayoiskia kwenye mradi wote ambao umejaa madini toka kwa kijana huyu ambaye mashairi anayotema ni ya ki utu uzima kushinda umri alionao.
Mradi unafunguliwa freshi sana sehemu ya kwanza ya wimbo uliobeba jina la mradi huu Gorilla 1 ambapo emcee huyu anachana freshi sana akitema mwanzo mwisho kwenye wimbo wa dakika tatu bila kuweka kiitikio. Kijana anaonesha vile ana hasira na hili game na anachana tena kwa mtindo huu kwenye Gorilla 2 kwenye mdundo flani mzuka sana. Msito ana mistari ya kijanja sana ambayo anaiwasilisha vizuri sana.
Kwenye Kinaga Ubaga inayopiga kwenye mdundo flani makini sana emcee huyu anakwambia kuwa chochote unachotaka kumwambia uwe muwazi na usimpake mafuta kwa mgongo wa chupa kwani hakuna chochote hajawahi kiona wala kupitia kwenye haya maisha yake madogo kwa hiyo yupo tayari kwa lolote bora yawe ya kweli.
Kwenye Weh Ishia emcee huyu anagusia mada ya mahusiano akitueleza story yake kuhusu vile alikutana na manzi flani, anaonesha uwezo wake wa kuandika hadithi na kuisimulia freshi. Kwenye mdundo inaskika mlio wa violin inayobeba hisia za emcee huyu.
Baada ya kutuonesha uwezo wake wa kuchana akiwa solo kwenye ngoma 6 emcee huyu anaingia booth na ma emcee tofauti kwenye nyimbo 4 akiwashirikisha ; Brima toka kundi la Maovete na Snaidah Da Don Dah kwenye Sura Punda unaotumia mdundo wa Kunta Official Beats.
Emcee huyu pia anashirikiana fresh na Lyrics kwenye Rada Ni Safi anajaribu kuchana kwenye mdundo wa Drill na kusema kweli hata hapa ananata na mdundo freshi tu japokua unahisi kuwa yeye anapenda kuchana sana kwenye midundo ya Boombap. Hili linaonesha kuwa ana uwezo sio tu wa kuruka na mdundo wowote bali anauua vilivyo pia.
Mradi unafikia tamati pale dogo anaposhirikiana tena na mshauri wake Brima pamoja na emcee Shazzy B kwenye Each1 Teach 1 ambapo ma emcee hawa wanahimiza umuhimu wa kila mmoja wetu kuwa mwalimu wa mwingine. Mwalimu Brima na mwanafunzi Brima wanawakilisha freshi.
Msito kupitia mradi huu ameonesha yafuatayo; uwezo wa kuandika mashairi ya ki utu uzima japokua umri mdogo, uchanaji na uwasilishaji mzuri, utunzi wenye uwezo wa kugusia mada tofauti pamoja na utunzi wa hadithi pamoja na kuwa na skio la kuchagua midundo mizuri kwa ajili ya kazi zake. Msito anaonesha unyama kibao na mnyama anayemuwakilisha vyema ni Gorilla.
Mcheki Msito ili upate nakala yako ya EP hii kwa Tsh 10,000.00/Kes 500.00 pekee kupitia
Facebook: Denis Msito (Gorilla)
Instagram: denis_msito_32