Toka kwa: Muki Rai x Arcane Krispah ft Oksyde
Wimbo: Mali Ya Polisi
Albam: Mbingu Zatazama
Tarehe iliyo toka: 25.04.2021
Mtayarishaji: Arcane Krisphah (Ndovu Kuu)
Studio: Utopian Records
Beti Ya Kwanza – Muki Rai
Katika ile hali ya kusaka maziwa, Mtaani tumezoea ni kawa ni kudandiwa/
Me si wa Mungiki ila me ni mzaliwa, so usdhani iyo bunduki inantishia/
Ni wazi ya kuwa, yako kuniua ndio nia, bila ata hatia/
Nikiwa tu kwa njia me sio kiruka njia, mimi tu ni raia sivunji sheria/
Hapa ndio home sa siezi kula vako? Hapa ndio home kwani siezi piga rao?/
Aih mkubwa, heshima si utumwa usinidharau, ni how?/
Unipige kibare, unipigie kelele, unitie chengerere, aih, aje?/
Alafu ujifanye beste yangu unihande nkugey za bwerere ndo uniache/
Aih, aje? hiyo sa si ni utiaji, ukicheki mariamu ebu chunga/
Coz if they catch you slipping, utasingiziwa, na bila ata ubishi jo mbaroni utatiwa/
Huskii kiutani unaezatashtukia/
Uko Korokoroni umeshahukumiwa/
After kushtakiwa hatia bandia, tunavumilia tumechoka dhulumiwa/
Ma yut wana ,machungu sa ile kitu wanataka, ni kufanya revenge juu ya damu ilimwagwa/
Na unawezaaaa, ka toanishwaaaa, ushukishiwe Gangsta Points/
Huku kila moment colombo ikiwaka, tuna commemorate maboy wali,madwanga/
Itabidiiii, Mmeihalalishaaaa, kabla unishike ka sina joint/
Beti Ya Pili - Oksyde
Wata kushika tu Bure... Huku affair ni risky/
Ulizia their histry.. Ya mbanga na mbaru uku city/
Ana sema ata ni let free ati ni bonge tu fiti/
Shieeet me niko chini, "Kijana wee leta ata fifty"/
Ati hawaezi ni wacha huru lazima ni walipe ushuru/
Nki try Ku say najua my rights…wanasema me ni kichwa ngumu/
"Kijana taku nyoa rasta unadhani we guru"/
"Na ukileta Kiherehere nanii takupigisha nduru.."/
Wana tumia violence kifua alafu wanaiita utumishi/
Ku patana nao ma chuom ma time ni swara juu uanga ni ubishi/
badala userve na ku protect wanashindilianga na vitisho/
Mtaani vijana na mbaru hatusikizani si cheza brikicho/
Ta ni shika aje na hau reason at all/
Umeni shika no reason at all/
Ile kunjaribu kupiga call nka zabwa kibare tenje ikafall/
Bila makosa nkaandikiwa loitering
Kutoka Kangemi ndani ya mariamu waka ni tupa Outering/