Mukimala/3rdeyegoof

Karibuni sana Micshariki Africa jukwaa la Hip Hop. Micshariki Africa ni jukwaa namba moja la Hip Hop linaloangazia utamaduni wa Hip Hop wa Africa Mashariki. Leo tumebahatika kupata mtu ambaye anawakilisha vyema utamaduni kwa kusimama vyema kwenye nguzo mbili za utamaduni huu ambao ni uchanaji/emcee pamoja na nguzo ya graffiti.

Simzungumzii mwingine bali ni Mukimala au kwa jina jingine analo litumia kwenye shughuli zake za graffiti, 3rd eyegoof.

Karibuni sana ili tuweze kumfahamu na kuweza kufahamu shughuli nzima za uchanaji pamoja na graffiti.

NB: Kama ungependa kuskia Podcast ya gumzo hili badala ya kusoma tafadhali nenda moja moja hadi mwishoni mwa makala haya

Karibu sana kaka Mukimala hapa Micshariki Africa jukwaa la Hip Hop. Kwanza kabisa tuanza kwa kukufahamu unaitwaje rasmi na unatokea wapi na unajishughulisha na nini?

Nashkuru sana kaka.

Kwa jina kamili mimi naitwa Raphael Mukimala Kato Bitungwa na ni msanii wa Hip Hop na natoka kwenye kundi la Hip Hop la The MC na tunawakilisha vizuri sana Hip Hop.

Mimi ni mkazi wa hapa hapa Dar Es Saalam na ukiachana na maswala ya Hip Hop mimi pia ni mjasiriamali, nafanya biashara zangu ndogo ndogo.

Kaka Mukimala tueleze kidogo historia yako ya nyuma ya muziki. Pia tungependa kujua ulizaliwa wapi, ulisomea shule gani na umefikia wapi kimasomo? Pia tueleze kuhusu historia yako ya muziki na sanaa.

Historia ya muziki. Aaah naweza kusema nimeitoa kwa mzee wangu, yeah kuna kipindi nilijiunga na kwaya ya kanisa moja inaitwa St. Peters, Oysterbay , ilikua 2000. Nilikua naimba kwaya na nilikua na sauti man, sauti ya kwanza. Sema baadae nilipokua kidogo na bass (sauti) ikatokea na sauti ikapoteza muelekeo kidogo nikasema hebu ni chill nikaanza kuandika mashairi na nini.

Aah na mapenzi ya mashairi ilitokana na literature, nilichukua HDL (Advance) kwa hiyo nilijikita sana kwenye maswala ya kiingereza na maswala ya mashairi. Kwa hivyo kabla hata ya kuanza kuchana mimi niliandika mashairi kwanza na nikakutana na rap enzi hizo nilipokua najifunza internet na ma internet café yalikua mengi ya kutosha. Mwanangu nikipata jero (Tshs 500.00) au buku (Tshs 1000.00) lote nalimaliza kwa internet café naenda ku Google muziki.

Wikipedia ilikua inanikoma si unajua, una Google jazz una Google nini sasa nikawa na Google Rap ikawa ni Rhythm And Poetry. Sasa nikaanza ku reflect na michano yangu, nikiwa naandika mashairi nikibadilisha inakua michano ikawa ina sound poa ndo nikajikuta naanza kuchana sababu hata hii michano yangu mingi sana ukiisoma  ni mashairi tu ya kawaida sio kuwa ni kufoka foka kwa sana, ni lazima itaku boost kiasi. Wajua tena ita ku boost kidogo ukafungue hata chapter mbili kwenye vitabu kadhaa si wajua, so huo ndio mziki man.

Kwa upande wa sanaa naweza kusema kutokea kitambo shuleni kwa sababu nilivyokuwa nipo kwenye hizi shule za kishua (internationals hizi) tulikuwa tuna masomo ya Arts & Crafts ambapo tulikua tunafanya masomo ya sanaa na nini.

Aah mimi nimezaliwa Ubelgiji (Belgium) na nimesoma mpaka 45 na 45 nilimaliza ilikuwa 2008. Nilipo maliza 45 nikaona miyeyusho nikaona siendelei maswala ya shule sababu nikaona nilikua sijengi ndoto yangu kwa sababu mimi mwenyewe nilikuwa napenda maswala ya sanaa na nini nikajikita kwa maswala ya graffiti design nikachukua cheti ambacho baadaye kikanipatia kazi na hapo nikajiongeza nikachukua Diploma ya miaka mitatu India na nikarudi 2013 nakumbuka na nikaajiriwa kwa miaka kadhaa baadae nayo nikaona miyayusho nikajiajiri mwenyewe.

The MC kundi lenu na Catalyst lilianzaje na mpaka sasa mna miradi mingapi na ilitoka lini iwe ni mradi wa mmoja wenu binafsi au kama kundi?

Sasa jina The MC lilikuja ki masihara. Ilikua mwaka jana kama sijakosea,tulikuwa tunatembea Sinza mimi na mwanangu halafu zikapita zile posti zile biashara za barabarani zile huku nyuma zimepigwa chata M na C na spray paint. Mimi nikasimama chini ya M (Mukimala) Catalyst akasimama chini ya C umeona. Sasa ile tumefika ghetto tunaperuzi nini tuanze ku discuss kabla hatuja iposti tukaanza kuwaza mwanangu, “MC, Sisi wenyewe si ma emcee mwanangu, alafu MC unakumbuka hilo jina kwa nani jina la ki MC si unajua kuwa jina la kundi ila tukapotezea lakini baadaye ilivyokua demanded kwenye baadhi ya appearances kwenye tulikuwa tunaenda ku perform na nini aah tukaji brand The MC. Ndio tayari hiyo, ishakuwa .

The MC - Mukimala (Kulia) na Catalyst (Kushoto)

Kwa sasa tuna miradi miwili lakini mengi yanakuja, unajua, stay tuned kaa mkao wa kula. Refraction tuliachia miaka miwili iliyopita ambayo ilikuwa chini ya Digg Down Records. Ilitayarishwa na Abby MP na De La Funky na mradi wa pili ndio huu hapa Hisia Za Kahawia ( Brown Senses Outta Scratches) ambao umetayarishwa na kaka Black Ninja toka BBC ambayo ni Boom Bap Clinic, yeah man tuna hizo santuri mbili for now lakini mengi yanakuja like we have more coming, kwa hiyo mkae mkao wa kula kama nilivyosema mwanzoni.

Ukiachana na hizo mbili mimi kama mimi mwenyewe niliachia moja ya mashairi 2015 ilikua ni mashairi matupu halafu ni kiingereza ilikuwa inaitwa P.O.E.M.S (Phrases Often Emancipate Minds Soothingly) hiyo ilikua 2015, kitambo sana ila ndio hizo ila kama kundi The MC miradi miwili tu.

Mukimala, mradi wenu Refraction niliupenda sana. Hebu tueleze kidogo kuhusu mradi huu. Huu mradi ulikujaje na mapokezi ya mradi huu yalikuaje kutoka kwa mashabiki?

Yeah man, mradi wa Refraction, refraction ni kitu poa sana. Refraction ni matokeo ya discussion ya mengi tunayoongeaga kati yangu na Catalyst wakati tume chill sana.

Tulikuwa hatutaki iwe kitu cha kawaida, kawaida nikimaanisha tu ni title tu halafu tunaongelea topic flani, hapana. Sisi tulitaka hiyo hiyo title moja iwe ina maana nyingi kwa sababu ndio style yangu na ya Catalyst. Siwezi nikamuongelea sana kaka yangu kwa sababu wote tuna uhuru wa kuongea lakini ni style yetu tuseme huwa tunafanyaga vitu vyenye maana nyingi.Hata tukiwa tuna address kitu huaga hatuangalii kwa njia moja huwa tunaangalia kwa njia nyingi, wajua kwa hiyo tukaichukulia refraction ina suit sana. Ni kama reflection flani ambayo inakuwa inaonesha mitazamo miwili kwa sababu refraction ndio ile reflection ile ya upinde wa mwanga, wazee wa sayansi si unajua.

Sasa ukiangalia kila track katika Refraction ina maana mbili Hybrid/High Breed, Kerosene/ Kero Scene ina maana mbili hapo hapo najenga picha mbili tofauti kwa hiyo sisi kama wasanii tunapenda kutumia sanaa sio kumfanya mtu aumize kichwa ila tunapenda kukufanya ujenge picha yako mwenyewe kwa akili yako. Unajua kwa sababu ni utamaduni ambao watu wanauchukulia poa sana kuchukua maneno na kuya formulate ili nijenge picha kwa akili ya mtu.

The MC -Refraction

Zamani watu wanaweza sema ni maswala ya uchawi lakini sio. Mimi kwangu nachukulia ni uchawi kwa sababu sio poa, yaani hivi ni vitu amazing. Tunachukulia poa sahivi ndio kwa sababu ya maswala ya shule na nini lakini maswala ya kughani na ku tell a story aah hiyo ni power moja hatari sana na sio ya kuchukulia poa. Kwa hiyo, yeah man Refraction ndio ilikua hivyo.

Na mapokezi yalikuwa mazuri sana like mimi nilitosheka sana kwa sababu watu wengi walikuwa wanatuzingua sana wanasema daah mwanangu itabidi mtoe kazi halafu finally kazi ikatoka na watu wengi wamenunua, watu wengi walionesha support na walikuja kwenye uzinduzi wa albamu. Na ilikuwa ni upendo mpaka sasa ni upendo man. Unakutana na watu wao wanakukumbusha kabisa, “Oya mwanangu wajua sijauchukua mradi wenu…” Kwa hiyo unamfanyia mpango anapata nakala au kama vipi soft copy unamtembezea so ni upendo man mimi nashkuru sana.

Japokua nyote wewe Mukimala pamoja na Catalyst mnaongea lugha ya Kiswahili freshi kabisa kwa nini mliamua kuchana kwa Kingereza kwenye album hii ya refraction. Je nyie mshaishi mamtoni maana lafudhi za kingereza pia si mchezo?

Bahati nzuri au mbaya wote tunabonga Kingereza na Kiswahili na tuliamua kuchana kwa Kingereza kwa sababu tunaweza. Mimi na kaka yangu huwa tunapenda kujenga madaraja, wajua. Na huwezi ukajenga daraja na lugha moja na ukiangalia sahivi Kiswahili inakimbiza noma. Ni lugha mbili ambazo zina nguvu kubwa sana duniani. Watu wengi wanajifunza Kiswahili watu wengi wanajifunza Kingereza watu wengi wanajifunza na kuongea vyote, wajua.

Kwa hiyo sisi tumetumia lugha zote mbili ili tujenge daraja kati ya wale watu ambao hawawezi kuongea Kiswahili ili waweze kutuelewa na waweze kuelewa maisha ya ki Tanzania kwa sababu ya tunachokiongelea hata kama lugha tunayozungumza sio ya ki Tanzania yote ambayo tunayaelezea kwenye mistari yetu ni maisha tunayoyaishi hapa Tanzania katika class zote katika tasnia ya mbongo.

Na hili swali la pili, hatujawahi kuishi mamtoni (akicheka).Yani hivi tunavyo chana ngeli ni matokeo ya kuskiliza Hip Hop na ni matokeo ya mapenzi ya Hip Hop.

Kando na kuchana niligundua pia wewe ni mchoraji mzuri tu unayetumia jina 3rd Eyegoof. Hebu tueleze kuhusu hili, kwa nini ukaamua kujipa jina hili tofauti na lile la kuchana. 3rd eyegoof linamaanisha nini?

Mimi napenda sana kuchora sana na najitahidi na najifunza kila siku mbinu tofauti na mpya. 3rd Eyegoof hili jina lilitokana na maswala ya graffiti. Wajua nilipoanza kupiga machata nilikuwa na tag yangu moja ambayo nilikua nachora madoti matatu, dash moja na kama kaulimi kametoka hivi kwenye mdomo hasa hiyo ikawa tag yangu ikawa sijaipa jina wala nini. Tokea 2003. Hata nikichora vitu vyangu shule nini utapata tag yangu naichora tu hivyo . Mimi nachora tu hata sielewi.

Lakini nilivyokua nikiangalia na maswala ya kiroho na uchizi wangu mimi kama mimi kwa sababu ukiangalia 3rd eye ni jicho la tatu maswala ya kiroho. Alafu goof ni mtu chale chale wajua kama ukikaa ukinifahamu ni mtu niliyejikita sana kwenye maswala ya kiroho halafu ni mtu chale chale pia kwa wale ambao wananifahamu kwa hiyo nikaona na ile chata mbona kama imeona kwa sababu ni macho matatu halafu chale chale ile inaonesha ulimi, ndio nikajibatiza 3rd Eyegoof. Hiyo hapo nikawa nimeifanya inani separate mimi na maisha yangu ya michano.

Kuchana natumia Mukimala ambalo ni jina langu halafu 3rd Eyegoof nikiwa napiga machata nikiwa nachora kwa sababu 3rd Eyegoof pia naitumia kikazi. Ukiangalia page yangu ya Instagram utaona kuna animations nafanya kwa hivyo pembeni huwa naitumia 3rd Eyegoof sanasana kwenye sanaa.

3rdeyegoof

Hii sanaa ya uchoraji ulianzaje, uliikuzaje na umewezaje kukuza vipaji vyote hivi? Ni vipaji gani vingine unamiliki ambavyo hatujui?

Sanaa ya uchoraji ilianzia shule na pia maskani nilikuwa na kaka yangu mmoja ni mtoto wa kaka ake mother anaitwa Rugemalila Katwa, aah man anachora vibaya sana. Bigwa alikuwa anachukua toys zetu anazichora vile vile, kitu kinatoka 3D. Aisee yeye ni kati ya wana walio ni inspire sana. Bi mkubwa naye alikuwa ananisaidiaga kuchora vitu wajua. Shule pia kule tulikua na madarasa ya kuchora na nilipoingia kwenye maswala ya graphics design kwa sababu lazima ujue kuchora kufanya graphics design. Unakutana na mteja anaomba umtengenezee logo lazima uichore, wajua kupitia maelekezo yake. Unajikuta tu yani maisha yangu yote ni ya kuchora tu.

Na kipaji changu nakikuza kwa misingi niliyoivaa mwenyewe, lazima kwa siku nichore michoro kadhaa. Haiwezi ikapita siku bila kuchora, yaani hiyo nimejiwekea. Yaani ipite siku bila mimi kuchora aah huyo sio mimi lazima mimi nichore. Iwe ni kwenye karatasi ambayo baadae najua nitaihamisha kwenye computer au kama ninayo computer hapo hapo nitachora kwenye computer.

Halafu nimewezaje kuvikuza hivi vipaji vyote? Kuvi practice daily, kuvi maintain. Wajua mi naishi kwa ule msemo ambao unasema, “Fanya Unachopenda” (Penda Unachofanya) na kusema kweli nikifanya kitu ambacho sikipendi ni unafki nitakuwa najisuta mwenyewe, roho yangu itakua inanikataa. Wajua mi maisha yangu yote nime ya base katika vitu ambavyo navipenda, na andika mashairi, na perform mashairi, nafanya michano, nachora na zote zinauza, wajua. Nashkuru.

Aah vipaji gani ninavyovimiliki vingine? Aaah vitu vingi man! Mimi ni mkulima,  napenda kupanda vitu. Napenda kupanda mimea tofauti tofauti, Spices, Pili Pili, Ndizi Mbivu, Matoke, Aah mambo mengi. Napenda kupika.

Je sanaa zote hizi zinakunufaishaje maishani mwako? Je zinaweka msosi mezani?

Aah yeah man. Sanaa zangu zinaninufaisha sana na zinawekea msosi mezani zinalipa bill ya maji zinalipa bill ya umeme. Hadi vocha zinaninunulia (akicheka). Kwa sababu ikitokea tender kama mtu anataka kufanya title ya animation, video au tangazo huwa nachukua hizo tender. Pia tender za graphics design kama mtu anataka nim dizainie website ntamtengenezea foundation lakini maswala ya coding sifanyi. Nitaidizaini ile template na nini alafu nampa. Michano, nafanya gigs zinanilipa, yeah man siwezi kulalamika nafanya ninachokipenda na naishi ninavyopenda.

Nanukuu, “Uchoraji ni uponyaji wa nchi”. Hapa ulimaanisha nini bwana Mukimala?

Aisee kaka unachimba sana, ati “uchoraji ni uponyaji wa nchi…” Hapa mimi nilimaanisha kuwa uchoraji ni dawa. Kama mimi, mimi nina dawa tuseme ngapi, tatu. Ya kwanza ni siri yangu, ya pili ni kuchora na ya tatu ni kulima. Mimi nikiwa na Vex, au stress au mtu akinikera kama nimeharibiwa siku kitu kinachoweza kunitoa katika ulimwengu wa hasira ni kuchora.

Yaani nikikaa nikishaanza kutengeneza mistari nikaunda shepu nikaunda nini, yaani hapo nishapotea nikaingia kwenye dunia tofauti man yangu. Yaani zile hisia za hasira na huzuni zote zinapotea, wajua ninakua kwa nchi yangu au dunia yangu peke yangu.

Kwa hiyo mimi naichukulia ni kama ni uponyaji kwangu mimi na uponyaji kwa wale wote ambao wanachora. Kwa sababu nishafundisha watoto hadi jinsi ya kuchora. Wajua kuchora inasaidia sana watu wenye matatizo ya akili watu ambao wame affectiwa kisaikolojia. Kwa hiyo ni mfumo mzuri sana wa kuponya kama meditation tuseme ndio nilicho kimaanisha.

Ngoma yenu Art Ya Booth iliyotoka hivi karibuni mliiundia video flani mzuka sana ya animation, hivi gharama za animation ukilinganisha na video za kawaida zipoje? Mbona hatuoni video za muziki za animation kwa wingi toka Bongo? Na utayarishaji wa video za animation hukuchukua mda  gani?

Yeah yeah ngoma ya Art Ya Booth tuliitengenezea animation. Gharama za animation na video za kawaida ni tofauti tu na inategemea sasa kama unafanya 2D animation na 3D animation. 2D animation sio gharama sana ukilinganisha na 3D kwa sababu 3D ina mambo mengi sana. Na ukisema kweli kwenye industry ya animation ndio nimetoka mda na sijui chaji zao ziko vipi ila mimi kama mimi huwa nakutengenezea kama ni tangazo huwa nachaji sekunde 30 elfu hamsini. Kwa hiyo unakuta kama wimbo wako ni dakika tatu kwa hiyo ni laki tatu. So hizo ndio charges zako. Ni simple ni fair, yeah man!

Aah kwa nini hatuoni video za animation kwa sana, mimi kusema kweli naona watu wanafanya animations tofauti na mara ya kwanza nilipoanza kufanya animations mimi. Wajua kama sasa hivi kuna Akili (Ubongo Kids) ile show ya TBC na kuna baadhi ya watu Zanzibar nimekutana nao wanafanya animations  na hata hapa Dar pia, sema tu watu wengi huwa wanafanya kazi zao offshores, wanachukua tender za nje wana malizana juu kwa juu na kidigitali kwa sababu inakuwa ni kazi za hela nyingi.

Hapa hapa ki bongo bongo mpaka watu wengi wakupate eeh inakua ni ngumu sana kwa sababu hata wakati mimi nilikuwa nafanya kazi nilipokuwa nimeajiriwa, isingekuwa kuajiriwa nisingekuwa napata kazi, kwani wengi wanachukua watu wa mbele kwa sababu watu walikuwa wana ile mentality ya kuwa hatuwezi au hatujui kufanya animations na naona soko linazidi kukua.

Utayarishaji wa animations unachukua mda na inategemeana na vifaa unavyotumia kwa sababu inapokuja kwa animations ni wewe na computer yako, au kama ni Ipad au nini, sana sana ni computer inabidi iwe na specifications kali alafu iwe na graphics card kubwa iwe na memory ya kutosha ili kazi zifanyike haraka.

Kando na sanaa yako kaka Mukimala, umeajiriwa pengine au unafanya shughuli gani zingine?

Tukiachana na sanaa mimi ni mjasiriamali bro, mi sijaajiriwa popote nilikataa kuajiriwa kwa sababu niliona najenga ndoto ya mtu mwingine na si ndoto yangu. Nauza sanaa zangu iwe ni prints iwe ni canvas, iwe ni animations, mashairi na kughani si unajua yeah man, ndio ninavyoishi.

Je nyie mnapiga chombo chochote cha muziki?

Aah ukiachana na sauti yangu, labda ngoma man yangu kwa sababu kuna ngoma napiga hapa na pale ila sana sana ni sauti na ngoma.

Nini tutarajie kutoka kwako na kundi lenu la The MC baada ya EP yenu mlioachia mwezi jana?

Mimi ningependa niwaambie mkae tu mkao wa kula, kuna mengi yanakuja. Baada ya hii EP nitawadokeza kidogo.Mimi na Catalyst tutaachia album ya sisi wawili separately, tukiwa wenyewe kama wenyewe ili watu waweze kupata ladha yetu wajua tukiwa sisi kama sisi halafu baadae tukiwa pamoja kwa sababu kutoka mwanzo watu washazoea kutuona pamoja, kutuskia pamoja. Kaeni mkao wa kula kuna utamu unakuja na projects nyingi sana zinakuja na zitazaliwa kupitia hizi projects ambazo zinazaliwa.

Ungetoa ushauri gani kwa vijana wenye vipaji ambao wanasubiria kuja kuajiriwa?

Aah mimi staki kuwa muongo, kama wewe unaona kabisa kuajiriwa sio kitu chako mimi nikushauri ukae chini na wazazi wako uongee nao uwapange uwaambie kabisa mimi ninachokipenda na u focus katika talent au kipaji chako. Lakini kama wewe unaona ni mtu unafaa kuajiriwa na ni ndoto yako kuajiriwa usione soo man we ajiriwa. Nenda peleka CV yako fanya yako. Lakini kama kuajiriwa sio ndoto yako mi nakwambia wachana nayo, focus kwenye kipaji chako kikuze, na kitakuletea kipato kama ndio kitu unachotaka kukifanya.

Nini cha mwisho ungependa kutuambia ambacho sijakuuliza? Na pia nini ambacho watu hawajakijua kuhusu emcee Mukimala pamoja na kundi lenu The MC?

Nashkuru sana kaka sina chochote cha kuongezea, ila nakutakia amani bro, asante.

Shukran sana kaka Mukimala kwa mda wako!

Wasiliana na Mukimala/3rdeyegoof kupitia;

Instagram: mukimala1
Facebook: Raphael Mukimala Kato Bitungwa
Instagram: 3rdeyegoof