Uchambuzi Wa Album: MK10 Vol. 1
Emcee: Musa Kiama
Tarehe iliyotoka: 11.02.2022
Watayarishaji: Bret, PMG, Santuri, Musa Kiama
Mixing & Mastering: PMG
Studio: B Recordz
Nyimbo Nilizozipenda: It’s On, Happy Face Emoji, Njoo Nkupeleke, Hatima, Against Taifa, Timing, L 4 Lanez, Mine
Musa Kiama
Moja ya ma rapper kutoka Mombasa ambaye nimekuwa nikimfuatilia kwa muda sasa ni Musa Kiama. Baada kuachia singo kadhaa na EP yake mwaka jana Full-Time EP emcee Musa Kiama alitubariki na album yake MK10 Vol 1 mwezi wa Februari.
Mradi huu ambao umeundwa chini ya usimamizi wa mtayarishaji PMG wa B Records Bamburi Mtambo ulitambulishwa na singo iliyoachiwa mapema sokoni Hatima ambayo iliwaandaa mashabiki kwa ajili ya ujio wa kazi hii. Wimbo chanya sana unaosherehekea maisha.
Na ndio hapa mradi unapojikita kusherehekea maisha; mazuri na mabaya yake, changamoto za maisha, utamaduni pamoja na mahusiano yetu ya kila siku. Mradi huu ambao asilimia kubwa ni boombap pia unamkuta emcee huyu akifanya majaribio ya kuchana kwenye mdundo wa Drill ambapo ndipo upepo unaovuma sasa hivi kwenye wimbo unaofungua mradi Crocodile Tears akitufungulia moyo wake akisema,
“Mziki kwangu ni mboga alie na beef ni doubting Thomas/
Really got nothing to prove but baby I cannot loose/
I’m fighting bipolar I’m not going crazy you can’t walk in my shoes/
Piga kazi na empty stomach I know where I’m from I don’t want to go back/
Taking my kindness for weakness what do you call that/”
Happy Face Emoji kama vile Hatima ni wimbo unakutia moyo kukukabiliana na changamoto zozote na kushkuru kwa kila jambo hata mambo yawe magumu kiasi gani.
Mine akiwa na Blu Concept ni nyimbo zinazoongelea mahusiano na mapenzi. Blu Concept kwenye Mine anamsapoti mwana freshi sana kwenye kiitikio kwenye mdundo unaogonga taratibu.
Njoo Nkupeleke ambao unapiga taratibu wakati kinanda mzuka sana kikilainisha zaidi mashairi ya Musa wakati mwana akikipaisha kitaa chake ili uone uhalisia wa maisha yake ya kila siku. Wimbo mzuka sana unao nuia ku appreciate mtaa.
Against Taifa akiwa na K Khassidy pamoja na Van Jan ndio unaonesha uwezo alio nao emcee huyu kama mtayarishaji pia. Kama vile Hatima aliouunda yeye wimbo huu ndio moja ya nyimbo zilizopiga sana kwenye speaker zangu. Umetulia si kimashairi bali hata ki mdundo akikwambia Mk “Roho ni ya mtaa/Mindset ni ya boss.”
Nyimbo mbili za mwisho kwenye mradi huu ni Timing akiwashirikisha Giriama Gang pamoja na L 4 Lanez akiwa na Haano Cadee. Ngoma zote mbili nilizipendea kitu kimoja, kando na kuchana Kiswahili wametumia pia lugha za nyumbani. Kwa Timing Giriama Ganga wanachana kwa moja ya lugha ya Mijikenda, Giriama ilhali kwenye L 4 Lanez Haano Cadee kwenye kiitikio kimechanwa kwa kisomali.
Mradi wa kwanza wa emcee huyu na binafsi nimeupenda ila ni mfupi mno kwani ndani ya dakika ishirini na tatu kabla haujakukolea vizuri, ushaisha. Ila ni hatua muhimu sana kapiga Musa Kiama Tena kwenye MK10 Vol 1.
Nunua mradi hapa
Au mcheki Musa Kiama kupitia mitandao ya kijamii;
Instagram: MK TENA
Facebook: MK
Twitter: Musa Kiama