Toka kwa: Nafsi Huru
Nyimbo: Ukweli
Album: Compilation CD
Producer: Nje Producer Msanii – Ufuoni Records

Vesi la 1

Tunazungumziwa tunaskia na bado tunapuuza
jua kuskiza ukibisha unapoteza elewa?
Allah anaongea na sisi kupitia sisi
Aliyeumba mbingu aliyeumba ardhi ni mmoja
na alituambia kupitia watume wake watukufu
vitabu vitakatifu kuishi vyema
tusiue tusiibe, tusifanye uasherati, tusizini
japo majaribio mengi kuepuka tujitahidi
ulimi tuuzoeshe ukweli, katu tusitapeli
hasa kwa jina lake Manani, Musisengenye nyie
wazabizabina musipende fitina
uwe na mamilioni huna hata ndururu mshukuru
Jalali ije heri ije shari, masika kiangazi
kwa kubwa ama dogo unapopata unapokosa
usimshirikishe na yeyote ama chochote
tumwogope ye pekee, tumwelekee
mbele yake kisowezekana hakuna
na huo ndio ukweli wa kila mwanadam

Vesi la 2

Sio lazima utege skio ndio uiskie radi
pia viziwi hushtuka inapo tetemeka ardhi
Walimwengu ni baadhi ndio waadilifu
wengine wote `waliosalia sio waaminifu
kabla kuasi pia ibilisi alikua malaika
usione ajabu bila aibu wakaribu akikugeuka
unapokua mkarimu wengi huchukulia ni unyonge
imani huvunjwa mdomoni ukatolewa tonge
raha yako wainyonge, wakikuzuia usonge, uskonde
chuki ni mzigo ukiubebesha moyo wako unauchosha
Mungu aeze kukupenda tenda yale ye anapenda
usikosee na ukikosea isiwe kusudi
ukiamua kupigana iwe ni pale hauna budi
tumia kimya na maneno ya hekima kujiepusha na vita
unapoweza toa fadhila saidia bila kusita
utendayo na usemayo huonyesha we ni mtu wa aina gani

Vesi la 3

Anakuambia mwarabu
Almaut baabun wakulu nafsi dahilu
kwa tafsiri mauti ni mlango kila nafsi itaingia
na huu sio uongo wengi wametangulia
kwa hivyo ishi unavyo ishi
jua siku yako inawadia
mi mwenyewe huchukia matendo yangu nkayatubia
Maanani niongoze njia nijaze imani
nijalie uadilifu mimi na wenzangu pia
oyaa jamaa hakuna atakae kuelewa usipo jielewa
lazima ujipende ndio ueze kupenda na kupendwa
Binadam tumezaliwa wafalme na mamalkia
wakati wako katika dunia vizuri tumia
kua mwema ng'ang'ania kila tendo zingatia
kila tukio liwe funzo kila funzo iwe nguzo
ya yale maisha mazuri sote tunayataka
ebwana kuona kesho hakuna mwenye hakikisho
kila jua linapo tua jua unakaribia mwisho