Mradi: Ishi The EP
Msanii: Nala Mzalendo
Nyimbo: 3
Tarehe Iliyotoka: November 2020
Midundo: Production, mixing, mastering na Nach B/ Str88IT

Nala Mzalendo

Nala Mzalendo ametuletea mradi mpya kutoka Mbeya City wakati huu ambapo majanga yameikumba duniani ili kutukumbushia kua ku 'Ishi' ni muhimu kuliko changamoto tunazo pitia maishani mwetu.

Naladona kama vile gwiji wa mpira alietuacha wiki jana marehemu Diego Maradona ni mfupi wa kimo ila ni mrefu wa chenga na shuti za mistari. Ep hii ina mikwaju matatu ya nguvu;

1. Nawakumbusha

Kwanza kabisa Nala anatukumbushia kua yeye ni yule yule, “Mtu Mfupi, Mistari Mirefu”. Na kwa kupitia mistari yake anakuonyesha kuhusu hali halisia ya maisha yetu ya kila siku.

“Nawakumbusha/
Unaweza uka kamilika vyungo vyote vya mwili/
Ukapewa fuvu la kichwa, lakini ukanyimwa akili!/ ”

Kwa kupitia EP hii Nala anatakuwakumbusha kuwa bado yupo kwa game na mistari yake bado ipo makini.

2. Ishi

'Ishi' ni nyimbo makini sana inayo onesha pande mbili za maisha tunayo yaishi. Ni nyimbo inayotuhimiza kupenda maisha na kuishi. Nyimbo hii ina kweli kibao kwenye mistari yake kama vile,

“Naweza kuishi na chuki na hauwioni/
Tatizo itanichoma kama mkuki moyoni/”

Pia anatuchekesha kwa kututania kuhusu umuhimu wakuishi bongo kuliko ughaibuni,

“Raha ya kuishi bongo ni kuishi huku unabezwa/
Nani ange ku diss kama unge ishi Uingereza!/”

Mistari ya Nala yamejaa busara ya kuto hukumu, anasema,

“Naishi na wema, pia naishi na ubaya/
Naishi na mpenzi wangu, haijalishi ni malaya/
Kila kitu kina mwisho maisha haya/
Ipo siku ata okoka atakuwa mwanzilishi wa kwaya!/
Usijali watu wanavyo kuongelea kumbuka kua/
“Mi sijali naeza kuishi kama nani/
Mbona historia inasema niliishi kama nyani?/ ”

Jee ana niki cha kuwaambia waalimu?

“Unajiona ukuta, unahisi una nyufa/
Waalimu wakishika fimbo, wanajiona wao ni Musa!/"

Masista do nao walipewa neno kwa njia la fumbo,

“Mchumba uto ishi kwenye mwezi/
Utaingia na kutoka, kisha utanikuta geto nime kumiss ile kilofa!/ ”

Nala anatema madini kibao yakutuelekeza jinsi tunaeza na tunapaswa kuishi kwenye nyakati hizi ngumu.

3. Party Ya Ghetto

Maisha ni sherehe na Nala kwenye wimbo huu anatukaribisha kwenye party kwenye Ghetto lake. Huu wimbo unakumbushia nyimbo zingine za awali za “Party After Party” kama vile “Kimya Kimya” wa Jay Moe na marehemu Ngwair au “Mikasi” ya marehemu Ngair pia.

“Kwanza una anzaje kununa/
Na umekuja mwenyewe bwana, hakuna alie kutuma/
Leo furaha na kicheko, karibu ghetto/
Tunafurahi,hatujui utarabi wa kesho/”

Kwenye party hii kuna kila aina ya msosi na tungi,

“Nimetulia na wanangu, freshi bila woga/
Oya changa jero jero kwanza tukadake mboga/
Shtua walio nje waje tukae kikao/
Gengeni kuna dagaa, pale pale kuna limao/
Wanasema tununue unga, wengine mchele/
Mara kuna jamaa, ame miss matembele/
Mwengine hataki kula, kwanza anataka ‘nyagi/
Sio mbaya, mzingatieni pia mshkaji!/
Leo tutakula hadi kitabaki/

Mpishi hana mikwara, kwanza amevua shati/
Tunaishi mara moja, kwa upendo wa dhati/
Asante Mungu unae zidi kutupa nafasi!/”

Je watu wa betting wapo kundini? Ndio wame wakilisha,

“Wana wana piga stori za ku beti/
Hela zenyewe za kibubu, sio benki!/ ”

Maisha ni sherehe, muunge Nala mkono anapo tuhimiza tu Ishi.

Nala Mzalendo