Uchambuzi Wa EP: Enzi Zetu
Emcee: Nevo
Tarehe iliyotoka: 06.08.2022
Nyimbo: 6
Mtayarishaji Mtendaji: Neville Mulama
Midundo, Mixing & Mastering: Lil’ Datchy, Yung Lawd, Jimmy The Beatmaker

Nyimbo Nilizozipenda: Acha Mdomo, Wapi Challenge, Punde, Wanabonga

Nevo

Nevo amekuwa kwenye radar yangu kwa muda sana. Hii EP nilikuwa niichambue mwaka mmoja uliopita ila kutokana na mambo tofauti tofauti kuingilia ratiba zangu ilibidi mradi wake ‘Enzi Zetu’. Mradi huu ndio mradi ambao ulinifanya nitulie niskie na nimuelewe kaka Nevo na mashairi yake.

Ndani ya mradi huu midundo ya drill ndio imepigwa sana chini ya watayarishaji Lil Datchy, Yung Lawd pamoja na Jimmy The Beatmaker. Kuna ngoma mbili ambazo zimetumia mdundo mmoja kwenye mradi ‘Wapi Challenge’ ambapo Nevo yupo man solo alafu kwenye ‘LLT’ yupo Trigger Wes mwenyewe pia.

Kwenye ‘Wanabonga’ ambao umeundwa na Lil Datchy emcee huyu anatanua misuli ya uchanaji wake akitumia nondo zake za kujigamba akitaka kuonesha vile watu wanaongea sana ilhali yeye anapiga kazi tu freshi akijenga maisha yake mdogo mdogo.

Mradi huu unabidi uwe na kamusi ya sheng kwani binafsi maneno mengi waliyochana humu yamenipita juu ya upara wangu japokuwa nime enjoy ngoma kadhaa hapa. Nevo bado ni "yanki" ila ndio ameanza kuwacha historia yake kwenye rap game ya Kenya. Siku moja atakaa na wajuu wake aanze kuwasimulia…”Nikiwa kijana, ‘Enzi Zetu’ nilidondosha EP yangu ya kwanza…”