Wimbo: NAAGNOOL
Emcees: Ngalah & MastaQuest ft. BananasOverdose
Mradi: The NAKALA Album
Tarehe iliyotoka: 01/12/2022
Mtayarishaji: Grand Master Teknixx
Mtayarishaji Mtendaji: Ngalah
Studio: Kubwa Studios
Verse 1 (Ngalah)
Sema na mimi, sema na mimi/
Walibobea Mashariki Afrika mabinti/
Saad Binti, Kidude B, siti ya mziki/
Tumehitaji miaka mingi kuwashabiki/
Na hayaishi na mashairi/
Queen Nzinga hakutishika alijitahidi/
Mekatilili na Rukiya Malkia Amini/
Mwana Mkisi atupatia story za miji/
Na Na wanawake wanatende, wakitenda wanatemwa/
Wanawake wanasema, wakisema wanalengwa/
Wanawake wanatenda, wametengwa Bogi Benda/
Wamejengwa body better, sio mimi tu nateta/
Ni stori mingi munaleta (stori mingi munaleta)/
Verse 2 (MastaQuest)
Zalisha nyonyesha fundisha komesha/
Mapishi nonesha ulizwa onyesha/
Tuliza ponesha mwanamke ni backbone ya kila Nation/
Kichwa kabeba maji, mgongo kabeba kuni/
Ni Rais wa Nchi na maneja wa kampuni/
Mpe silaha atapigana na madume/
Eh leo waongo midomo watafunga/
The oldest profession sio ya malaya ni ya wakunga/
Maze heshimu kina dada paradise iko chini ya miguu ya mama/
Zalisha nyonyesha fundisha komesha/
Mapishi nonesha ulizwa onyesha/
Tuliz ponesha mwanamke ni backbone ya kila Nation/