Wimbo: Wanyonge
Toka kwa: Nikki Mbishi ft. Makamua
Mradi: Welcome To Gamboshi
Tarehe iliyotoka: 04.03.2022
Mtayarishaji: Kise P
Mixing & Mastering: Black Ninja
Studio: Boom Bap Clinic

Beti Ya Kwanza

Mnyonge mnyongeni haki yake mnyang’anyeni/
Na hata kama hajafanya kosa mkamateni/
Puuzeni matakwa yake mali zake gawaneni/
Mbambikieni kodi biashara zake fungeni/
Mpeni kesi za rushwa kutatakatisha fedha/
Uchochezi huani na jela mpelekeni/
Akipaza sauti kiherehere mtekeni/
Akipinga itikadi za chama pia mtengeni/
Au mfukuzeni na kwenye teuzi mpunguzeni/
Kuna bwege mmoja na mkosa sana bungeni/
Mtapigwa mabomu shauri yenu andamaneni/
Msigome matamko yakitoka nyi yafuateni/
Msijifanye Kigogo mkihujumiwa nyamazeni/
Msikosoea jambo mkikerwa kalaleni/
Isije tokea vita ya Kagera Magomeni/
Wana chuo nawasihi msiandamane kasomeni/
Mtachezea virungu nyi hayeni/
Wagogo mi hanyeni/
Hamuezi kuishi nchi hii hameni/
Ndivyo tunavyo ishi dunia imejaa watemi/
Wanao tia huruma kipindi cha kampeni/
Tukiwapa dhamana wanatuacha masingeni/
Usawa umetukaba makendeni/
Twendeni/
Ajira ku beti vijana gengeni na Singeli/
Nchi yangu tajiri alafu naitwa maskini kazi kweli/

Kiitikio

Hatuna haki hatuna sauti/
Hatuna machaguo wala maamuzi/ x2

Beti Ya Pili

Akitembeza karanga mzururaji/
Akiuza sigara mlanguzi/
Sasa ataishi vipi huyu mshkaji? /
Baadhi ya viongozi mwanzo hamkuwa na mitaji/
Zaidi ya porojo zenu na kujifanya wajuaji/
Tumewapa ajira leo mnatuita wanyonge/
Wanyama samaki na sijashtua kidaka tonge/
Mashavu yote ya Simba King Kiba na bwana Konde/
Tutapata Suluhu tukiacha Pombe tusonge/
Mnyang’anyeni ardhi huyo hawezi kuwekeza/
Na mikataba yenu ongezeni Kingereza/
Maskini tabula rasa asielewe akielekezwa/
Hana umuhimu zaidi ya miradi mnayotekeleza/
Msijali njaa zetu komaeni na miundombinu/
Nyie mnajua kila kitu sie wengine hatuna elimu/
Basi nitaitwa mchochezi na wenye akili finyu/
Mchi ni ule ule hata mkibadili kinu/
Nasema ninayoyaona mitaani na kupitia/
Wajukuu njaa bibi hana kuni za kupikia/
Majiko ya umeme na gesi hajawahi kuyaskia/
Na hata ukimpatia hatomudu kugharamia/
Uchumi wake duni umetekwa na maharamia/
Kama wazee flani wa bandari mabaharia/
Tuna njaa ya vitendo wanatulisha nadharia/
Wanaharakati bandia mkitishwa mnakimbia/

Kiitikio

Hatuna haki hatuna sauti/
Hatuna machaguo wala maamuzi/ x2