Toka kwa: Nikki Wa Pili ft G Nako, Ben Pol
Wimbo: Staki Kazi
Albam: Singo
Tarehe iliyo toka: 13.05.2014
Muunda Mdundo: Nahreel
Studio: The Industry Studios

Vesi ya kwanza

Uko na wasiwasi mtu bila nafsi/
Umeajiriwa shirika la mtu binafsi/
Sina wasiwasi mtu mwenyewe nafsi
Sijaajiriwa nime ajiri yangu nafsi/
Biashara imejaa makato/
Biashara mjini ndio zimejaa mapato/
Ajira itakulinda toa vyeti/
Sihitaji kulindwa mi sio mtoto wa geti,
Kazi ni mpaka wa akili yako/
Mpaka ufukuzwe kazi ndio ugundue kipaji chako/
Ajira ya mkeo chini ya boss/
Wee ni house geli pekee nchi anakuita boss/
Mi si vai tai si kataii/
Utamaduni wangu ni kuuliza why? /
Elimu bongo imekosa plan ya pili/
Kosa la pili haufundishwi kua tajiri/

Vesi ya pili

Wanasema hizi singo na jingo mzee/
Naelekea kua bosi ki Rozzay/
Nikki nina binti mzuri nikuoze? /
Mi bado siko vizuri nipozee/
Nakuza network najuana na watu/
Nakuza yangu keki napunguza za watu/
Keki, baada ya Mungu ni mzungu alafu mimi (obvious)/
Unataka mtoto mwenye akili (serious)/
Fanyafanya uzai na Nikki Wa Pili (genius)/
Sitafuti kazi nataka nitafutwe na wanao tafuta kazi/
Kuimba mziki kazi ya Mungu/
Staki kazi ya mtu aki ya Mungu/
Aah kazi ni kipimo cha mtu/
Amka umekunja sura kipimo cha mtu/