Wengi watakuwa wameskia mdundo wa HHC Rap Challenge – Sawa ya Kaa La Moto ila huenda wakawa hawamfahamu producer aliyehusika na kuunda mdundo huo. Huyu si mwingine bali ni NJE Pro ambaye ni producer anayefanya kazi zake ughaibuni kwa sasa ila chimbuko lake ni Mombasa, Kenya.

Leo tumepata fursa ya kukaa naye ili kuweza kumfahamu vizuri. Je uko tayari kwa gumzo letu na NJE Pro?
Sawa, Twenzetu!

N.J.E Pro ni nani,kazaliwa wapi na anatokea/kupatikana wapi?

Nje Pro ni msanii, music producer, audio engineer, Mc, Radio Host na shughuli nyingi za kisanii.

Jina lako la rasmi ni nani?

Kwa majina rasmi ni Fredrick Kiama

Kwanini uliamua kujiita N.J.E Pro? Jina lilikujaje na linamaanisha nini?

Najiita N.J.E Pro sababu Nje ni jina la kupewa tangu utotoni kisha likazoeleka kama kijana wa kwanza wa kivulana (toka kwa familia yetu).
Pro ni ufupi wa jina producer.

We ni mpiga Midundo tu/beat maker au producer au hata emcee pia?

Mi ni mpiga midundo, full audio and video producer, mwandishi, mtunzi wa nyimbo na pia ni emcee.

Historia yako ki mziki ikoje ?

Historia yangu ya kimziki ni ndefu sana,mwanzoni nilianza kama msanii pekee,kisha baadaye nikaanza kutengeza midundo. Nimefanya kazi na wasanii wengi nchini Kenya/Tanzania na hata nchi za nje.

Ulianzaje shughuli za music production na ni kipi kilichokupatia motisha kuendelea na production?

Kilichonipa motisha kuwa producer ni wakati tulipata shida tukiwa wasanii kwa kundi letu moja mimi na mchizi wangu tukijiita G.O.B.

Ukiangali hawa ma producer waliopo kwenye game ya Hip Hop Kenya na duniani ni nini kilicho kufanya uamini utafanikiwa kama producer ?

Ilikuwa ngumu sana ku record mziki na pia ma producer walikuwa wanaringa sana na walikuwa wachache,so nikashikwa na hasira sana ndipo nikajitosa na kujifunza kutengeneza midundo, nia yangu ilikuwa kuwapatia wasanii nafasi ya ku record na wajiweke huru.

Mimi nilikuwa na ndoto toka nikiwa mdogo na ninavyokua nilikuwa natamani sana nifike matawi ya juu, yani nipate fursa ya kufanya kazi katika mazingira ya hali ya juu, kama vile nilikua nikitizama ma movie na ma video naona vyombo na vitu ambavyo sikudhania nitavipata,nilikuwa ni mtu  mwenye  ndoto za juu na nilitaka niwe kivyangu nisifanane na mtu mwingine.

Je unatengeneza aina gani ya miziki?

Mimi natengeza sana Hip Hop, Underground, Boombap, sometimes natengeza mziki wa aina yeyote bora mziki tu. But sana sana napenda kukaa katika conscious Hip Hop yaani mziki wowote ambao ni wa kudumu.

Ulishawahi kuwaza huenda ukafanikiwa au usifanikiwe kwenye shughuli ya kuzalisha muziki?

Sijawahi kuwa na shaka sababu hii ni ndoto ambayo nilijua siku moja itatimia.

Ni kipi kilichokufanya usiache fani hii ?

Kilichoniskuma nisiwache fani ni mapenzi makubwa na hope kwani nilijua hii ndio njia yangu. So, nilikuwa naifanya kwa moyo na nikitarajia malipo baadaye.

Watu walimtambua Nje kama producer baada ya muda gani tangu aanze kugusa instruments?

Haikunichukua muda mrefu,sababu watu walikuwa wananitambua kama msanii na nilikuwa na connection nyingi, ya mtu wa watu,so watu walivyoskia nafanya production,ikawa rahisi kwangu.

Je ma producer wa Mombasa wanakubalika kama wenzao toka Nairobi?

Ma producer wa mombasa wanakubalika, shida ni toka kitambo ilikuwa ngumu kutoboa mpaka watu waende Nairobi,na fedha pia ma producer wetu wa Mombasa hawawekezi kwenye mziki,ndio maana imekuwa ngumu kiasi.

Marketing pia iko chini sababu hamna support na mafunzo.

Unapataje wateja?

Wateja wangu wapo online. Kuna sehemu nyingi tu natoa huduma zangu, ukinihitaji ukiwa pande yoyote ya dunia. Social media, sio lazma tukutane uso kwa uso, pia kuna face time tunawezafanya kazi tu.

Ungepewa nafasi, Ungetoa ushauri gani kwa yoyote anayetaka kufuata nyayo zako?

Kuwa mvumilivu, heshima, na fanya kazi kwa bidii. Hakuna kinachokuja kwa urahisi,usitarajie kupanda mbegu leo uvune kesho,kila hatua ipo na utaratibu na hakuna short cut ya maisha.

Ushawahi kupata kazi kutoka wasanii wa nchi za nje?

Ndio… nafanya na wasanii wa nje sana.

Hip Hop ya Marekani na  Ulaya  na hii ya East Africa ina tofauti? tunaweza kujifunza toka kwao au wao kujifunza nini kwetu?

Tofauti ipo kubwa sana! Kwanza mamtoni soko lao liko imara. Muziki huku upo na utaratibu kuanzia uandishi mpaka packaging. Kila mtu ambaye amehusika katika kuandaa  mziki anahusishwa mpaka kwenye biashara,na anajua mapato yake kabla ya  kufanya kazi.

Pia kuna utaratibu wa mikataba ambayo inarahisisha kazi. Ukipewa deal ya album tayari ushapewa budget yako,so we ni ku deliver. Hapo ni kama umesainishwa na record deal. Kuna endorsements nyingi kutoka  kwa makampuni tofauti.

Kuna elimu ya watu kufahamu biashara inavyokwenda na wasanii wengi wako na management team ya kusaidia kuskuma kazi.

Umeshafanya kazi na ma emcee gani na kwa miradi gani hivi karibuni?

Nimefanya nyimbo kadhaa lakini sijawachilia sababu ya biashara,lakini mwaka huu nitaachia kazi nyingi.

Je, upo chini ya mtu au una miliki studio zako mwenyewe? Pia tueleze kidogo kuhusu historia ya Ufuoni records

Mimi nipo America Seattle kwa sasa,na namiliki studio yangu mwenyewe.

Ufuoni Records ilianza kama mwaka 2000 hapo na kufunguliwa rasmi 2002 Mombasa, kisha nikahama kuja hapa Amerika 2013.

Je unaelezeaje mtindo wako wa kufanya kazi na msanii ?

Mimi kabla nifanye kazi na msanii yoyote inakuwa natural lazma nikufeel na uwe katika levels za mziki ninaoufanya mimi.

Lazima miaka yetu iwe sawa.

Ni wimbo gani au mradi gani unaoupenda sana ambao uliufanya?

Nipo na nyimbo nyingi nyingine hazijatoka,ni ngumu kuchagua moja.

Lakini album ya Kaa La Moto Kesi.

Sawa beat, unainzungumziaje? Unajiskiaje kuwa Sawa upo kila mahali sasa?

Sawa beat yani ilikuja natural. Katika hali zangu za ma beat tulikuwa na mazungumzo sana na Kaa La Moto, na hii beat nilitengeza haswa kwa minajili ya kumpa Kaa La Moto motisha baada ya kuangalia industry yetu ya mziki ilivyozembea, yani ilikuwa beat ya uchungu tu. Kisha Kaa La Moto aliitendea haki kwa mashairi kama inavyotakiwa.

Ujumbe ndio ulikuwa muhimu uwafikie ndipo sasa kukawa na Sawa Challenge.

Yani kuskia mtu yoyote yule ameutambalia ni baraka sana.

Gharama zako kwa kazi hii ni bei gani?

Gharama inategemea na mtu,siwezi weka bei moja.

Unasikiliza nini na kumsikiliza nani sana hivi karibuni ?

Naskia kiasi mitindo tofauti ila hainifurahishi sababu mimi ni shabiki wa hardcore Hip Hop,but najaribu kufuatilia.

Je, ni kitu gani ambacho unakizingatia kila uki produce ili kuhakikisha kazi inatoka kali?

Kuwa tofauti na wenzio na kujipa changamoto kwa kila kazi ninayofanya,saa zingine naweza tengeza beat nzuri na nikaifuta sababu sijaifeel!.

Ni nani mtayarishaji wako bora wa muziki unayemkubali sana?

Wapo watayarishaji wengi  na naona wanafanya vizuri tu! Japokuwa kuna kazi zingine naziskia lakini sijui majina ya ma producer waliohusika.

Nje ya muziki N.J.E Pro hujishughulisha na nini?

Nje ya mziki nafanya biashara tofauti,napenda kucheza mpira wa miguu,safari na kujiburudisha na marafiki.

Nipe mawili matatu juu ya game ya underground hip hop toka Kenya na Africa Mashariki..

Game bado haijachangamka vilivyo,sababu mitindo ya underground haijapewa kipaumbele, kuna mitindo mingine imetangulia na kushikilia soko,ila pande za Tanzania naona wanajikwamua sababu soko lao lipo juu kiasi.

Ila kuna watu wachache wanafanya vizuri

Nadhani underground soko lake bado halijafunguka,ila linajulikana lipo.

Unazungumziaje rap game iliopo sasa ya Trap, Shrap na mumble rap?

Mziki ni mziki sababu hao wa trap,shrap na mumble wametafuta soko lao, so kila mziki una soko lake sioni haja ya kukashifu mziki ambao siuskizi! Kila mtu ashike analofanya na atafute soko lake, muda umebadilika na watu wanakuja na idea tofauti.

Je ni masomo gani muhimu ambayo umejifunza juu ya kutengeneza midundo ambayo ma producer pamoja na wasanii chipukizi wanaweza kujifunza?

Siku hizi mambo yamekuwa rahisi, elimu ipo ya bure, ukienda online utapata mafunzo unayotaka. Imekuwa rahisi ma producer wakubwa wako na programs zao na wanakupa siri zote za kufanikiwa kimziki.

Una miradi yako binafsi iwe ni EP, mixtape and albam ambayo ulishawahi iachia sokoni?

Nipo na album (Game Ngumu)iko sokoni online na pia zipo singles, Itunes,  Amazon nakadhalika.

Tutegemee nini toka kwa NJE Pro hivi karibuni au hata baadaye?

Naangusha album mpya soon na pia video zipo njiani zinamaliziwa kazi.

Wasiliana na Nje Pro kupitia:

Facebook: Nje Pro
Instagram: Nje Pro
Twitter: Nje Pro
YouTube: Nje Pro
Tovuti: www.ufuonirecords.com