Uchambuzi Wa Album: GUERILLA: dynasties vs the PEOPLE
Emcee: Nuffsed
Tarehe iliyotoka: 18.02.2022
Nyimbo: 19 (Pamoja na Intro, skits na interlude)
Mtayarishaji, Mixing & Mastering: Echochamber 

Nyimbo Nilizozipenda: Mzuka, Fire, Don’t You Ever Learn, Raw, Score, Nazidi, Real All The Way, Mware, State Capture + Hidden Track

Nuffsed

Jimbo la Nakuru linalopatikana kwenye bonde la ufa nchini Kenya, lina utajiri sana kwa sababu ya vitu kadhaa; Ziwa Nakuru, Ziwa Naivasha, Ziwa Elemtaita, Ziwa Bogoria, Ziwa Baringo pamoja Hifadhi ya Taifa ya Hell’s Gate.

Wasichokijua watu wengi wanapokwenda huko ni kuwa kwenye mazingira haya ya maziwa na hifadhi ya taifa kuna kundi flani la wachanaji waliojikita kule wanaojulikana kama 1183. Kundi hili limeweza kupatia wana Hip Hop wa Kenya ma emcee wenye uwezo mkubwa na wenye desturi ya kuachia miradi ya kiutu uzima.

Moja wa ma emcee hawa Nuffsed anayeiita Nakuru nyumbani alifanikiwa kuachia album yake ya kwanza mapema mwaka huu iendayo kwa jina GUERILLA: dynasties vs the PEOPLE. Kama ilivyo kawaida ya ma emcee wa 1186 miradi yao mingi huundwa na watayarishaji wanao patikana huko huko Nakuru na pia waliopo ndani ya kundi hilo la 1183.

Mradi huu wa Nuffsed umeundwa ki old school sio tu ki uchanaji bali hata ki midundo. Mwanzo mwisho midundo ni ya boombap na hata emcee mwenyewe anapochana utaona moja kwa moja yeye ni mwanafunzi wa old school boombap rap.

Single ya kwanza kuachiwa iliyotambulisha mradi ni Mzuka. Ngoma hii inakuonesha moja kwa moja ni nini utapa kwenye album hii; boombap beats na mistari ya kukuelimisha, kukuburudisha na majigambo kidogo hapa na pale.

Hata hivyo mradi baada ya kufunguliwa na Shout Outs_Intro unaanza na Mzuka moja kwa moja kabla ya kwenda kwa maigizo na kutufikisha kwa ngoma ya kuwasha moto speaker zako iitwayo Fire akiwa na dada Ash ambae uwezo wake wa kuimba tuliuona kwenye album ya memba mwingine wa 1183, Veryl Mkali Wao Shadow Of Death. Ngoma inatupeleka hadi kwenye wimbo Don’t You Ever Learn akiwa na emcee Romi Swahili ambaye naye anawaikilisha vyema 1183. Kama kawa nondo ni moto.

Moja ya ngoma iliyonasa maskio yangu ni Nazidi ambao kama kawaida ya ma emcee majigambo kuhusu uwezo wao lazima yawepo akisema Nuffsed,

“Na spark imagination na deeper meditation/
Guide your mental navigation leave you high like levitation/
No need for altercations so mzeiya ukini question/
Hip Hop ndio foundation I do this for my hood rats no doubt naleta mzuka/
Ndio maana nikiwa gusa jo wanapata goosebumps/
They wanna know now who’s that kwa block ni kama unga/
Patia dame yako lugha mpaka abuye kama dumba/
Ma rapper siku hizi Judas,street gospels waliruka,
Mashairi nikitunga utadhani ghost ya Tupac/
Hii doo nikitafuta kwenye bonde la ufa/
Life ya survivor hua kupata au kufa/
Walidhani sitakuja na sasa nimetua controversial shinda Huddah/
No shoul've coul've woul've,I drop the weight kushinda chuma/
Vituko ndo mnaduman,naristoza "Ki**ma"/
Wallah naskia ikiniuma ati wackness ndo inavumaaa!!/

Ngoma ambazo zimesimama kwenye mradi huu pia ni kama Real All The Way ambapo Nuffsed anaonesha uwezo wa kuimba pia kando na kuchana pamoja na Mware ambao ni wimbo shwanga sana unaompata emcee huyu akichana juu ya mpenzi wake.

Wimbo mwingine uliosimama kwenye mradi huu ambao pia ulikua kama single ya pili toka kwa mradi huu ni Raw.

Nuffsed ametupatia mradi kwa watu na ulioundwa na mtu wa watu, Guerilla: dynasties vs the PEOPLE.

Japokua mradi unaweza ununua pale tovuti ya Bandcamp unaweza mcheki mwana na ukualipia kwake. Mcheki kupiti;

Instagram: officialnuffsed
Facebook: Nuff Sed