Ponera MC "Safari"

Msanii: Ponera MC
Wimbo: Safari
Album: Single

Utangulizi

Ponera anasema “binadamu tumefungwa ufahamu wa yale yanayotokea au yatakayokuja kutokea baadae”na huo hasa ndio mzizi wa wimbo huu.  Ponera anatufungua ili tuone mfano wa yale yanayoweza kutokea baada ya maisha yetu ya hapa duniani. 

Lengo ni kutukumbusha ili tupate kujiandaa na kujiweka kwa nafasi nzuri tungalipo hai hapa duniani, kwani “hii ni safari ambayo kila mtu lazima aipite” kama asemavyo Ponera

Mwanzo

Siku imefika na roho inauacha mwili. Haitwi tena kwa jinale bali anaitwa marehemu,anajaribu kuongea lakini sauti haisikiki, anataka kuamka lakini mwili hauna ushirikiano na hatimaye anagundua yupo kwa ulimwengu mwingine na sio duniani tena,kwamba yeye ameshakufa. Marehemu huyu anashuhudia yatokeayo nyumbani kwake,msibani.

Picha ya kinachoendelea msibani inaelezewa na “marehemu” huyo ambaye kwa matukio yanayoendelea analalamika na ananasihi hasa kwa familia yake lakini yake ni sauti ya mtu alie nyikani hakuna anayeisikia.

Wimbo unajenga na kuunganisha picha ya ulimwengu wa watu na ulimwengu wa wafu, ubunifu huo wa kufikirika ndio utamu wenyewe wa wimbo huu na ubunifu huo ndio unafanya wimbo huu kuwa wa kipekee sana.

Uandaaji wa wimbo

Wimbo umerekodiwa na producer Tenth Wonder ambaye kwake na Ponera ni ndugu kwani urafiki wao umepitiliza. Producer aliandaa mdundo na kumsikilizisha Ponera, nae Ponera alipitisha hisia zake….kilichokuja kutokea ndio hicho, Msiba.

Kabla ya jina la Safari wimbo ulikuwa umebatizwa jina la “Muacheni Mke wangu” lakini title hiyo ikaonekana ndefu na ya wazi ndio sasa ikapendekezwa wimbo uitwe Safari. Mabadiliko ya jina hayakuhusisha mabadiliko ya mashairi kwani ingawaje wimbo unaelezea safari ya mwisho ya kila mwanadamu lakini muegamo ni kwa mwanamke anashughulishwa na kulaghaiwa kimapenzi baada ya mumewe kufariki.

Uandishi

Uandishi wa wimbo ulichukua muda wa wiki moja na wiki iliyofuata ilitosha kabisa kurekodi na kuweka sawa issue ndogo ndogo, wimbo ukawa umekamilika ukiwa na verse 2 tu. Ndipo Ponera na producer wake wakaona kuna sababu ya msingi kuongeza verse ya 3. So Project ikasogezwa mpaka baada ya siku 2 ndipo Ponera akaongezea verse ya 3. Kwa hiyo mzunguko mzima wa wimbo ukawa umetumia kama wiki mbili na ushee hivi

Sababu nyingine ya wimbo kuchukua muda huo ilikuwa ni muingiliano wa ratiba za studio, kwa maana kuna muda P ilibidi asubiri wasanii wengine nao wafanye project zao.

Changamoto

Changamoto kubwa kipindi wanarekodi wimbo huu ilikuwa ni kufutika futika kwa project hiyo pale studio hali iliyowalazimu kurudia kurekodi zaidi ya mara 4 hivi. Baada ya ukamilifu wake, kama alivyopata kuandika Producer Tenth Wonder kwamba yeye ndiye aliyependekeza wimbo huu utoke.

Ponera anaongezea hapo kwa kusema, kwake huu wimbo aliuona ni wa kawaida tu, hivyo alipendekeza uachiwe wimbo mwingine lakini kwa ushawishi wa Producer huu mkwaju ndio ukapata nafasi.

Kwa mshangao baada ya wimbo kutoka Ponera akawa bize, bize kupokea simu na kujibu message za kila aina ya pongezi kwa mkwaju huu, ilifika kipindi hata yeye akabaki anashangaa kwa jinsi wimbo ulivyopokelewa vizuri ni dhahiri kwamba ujumbe wake ulifika vizuri kwa hadhira, mapokeo yake yanathibitisha Hilo. Wimbo huu ulitoka rasmi tarehe 15/07/2017.

Ahsante.

Mcheki Ponera MC kupitia;

Facebook: Demetrius Hon
Instagram: ponera_mc
Twitter: PONERADEMETRIUS