
Zee Maya: "Kioo"
Msanii: Zee Maya ft. Jossian
Wimbo: Kioo
Album: Single
Utangulizi
Anaitwa Umaya Twaha ukipenda muite Zee Maya, na leo yupo nasi kwa NyP na wimbo wake wa “Kioo”.
Kioo imefanyika katika studio za Mowton Records na Producer Dullah ndio alisimamia mpango mzima.
Kwa mara ya kwanza ni ngumu kwa msikilizaji kung’amua wimbo huu wa “Kioo” unazungumzia nini na hii ni moja ya sababu ya NyP kuteta na Maya ili kupata mawili matatu kuhusiana na kazi hii.
Wazo
Zee Maya anasema katika ujenzi wa idea hii hakuwa na chanzo husika na wala hakupata wazo kutoka kwa mtu wa pembeni bali alichofanya ni kuvaa kiatu cha mtu aliyepoteza kitu hasa kilichokuwa kinampa status kubwa, hapo ndipo akaona mengi ya kuyajadili ndani yake.
Ujumbe
Maya anasema “Nilipanga nijenge picha kuonesha jinsi nilivyoumia mara baada ya mtu niliyekuwa namtazama kama kioo (role model) kukengeuka"
Uandishi
Zee Maya anasema “Mi huwa natumia mda mwingi kwenye hatua ya mwanzo ya kuandaa wimbo, nikimaanisha uandishi na kwa wimbo huu nilitumia mwezi na wiki mbili ila beat, vocal na mixing na mastering vilichukua wiki mbili tu, so ni miezi miwili kwa ujumla.”
Aina ya uandishi na namna alivyoifunga hiyo message yake Zee Maya anasema “Lengo langu ni kila mtu aguswe kivyake; hapo aliyepoteza nguo, aliyeachwa na mke/dem, aliyesuswa na ndugu wote wataguswa kwa namna zao”
Malengo
Zee Maya anasema “licha ya kuongea na watu wenye influence kubwa katika jamii akiwanasihi watunze dignity zao kwani wanapoharibu wafuasi wao wanaumia, lakini pia nimewaambia watu wathamini vitu vinavyowazunguka kwa kuvi treat kama vile inavyotakikana”
Changamoto
Zee Maya anasema changamoto aliyokutana nayo ni kumpata mtu wa kufanya chorus, hili lilimsumbua sana hata kujaribu kufanya kwa namna nyingine. But kuna siku akiwa kwenye tamasha flani hivi, akamuona mwamba anaimba cover za wasanii mbalimbali…akamuelewa uimbaji wake na bahati nzuri alivyomfata ikawa barida tu. Zee Maya anakubali kwamba “Kioo” imepata mapokeo kuzidi ngoma yake ilyotangulia na hii kwa kweli imempa sana moyo.
---
Siku zimeenda sasa tangu utoke wimbo huu lakini bado Zee Maya anaikumbuka ile siku, ile ile siku wanatoka kufanya chorus ya wimbo huo wa “Kioo”, siku hiyo akiwa njiani simu yake ilidondoka na “Kioo” kuvunjika hii ilimfikirisha sana…ilimfikirisha mno!
--
Kwa hayo machache nikushukuru msomaji wa NyP na tukutane tena kwa makala nyingine hapa hapa kwa Micshariki Africa.
Mcheki Zee Maya kupitia;
Facebook: Zee Maya
Instagram: zee_maya
Twitter:IamZeeMaya
Pia mcheki Iddy Mwanaharamu mwandishi wa makala haya kupitia;
Facebook: Iddy Mwanaharamu