
Formula
Msanii: Formula ft. Dully Sykes
Wimbo: Namba Ya Simu
Album: Single
Kipindi flani pale kati zilifanywa nyimbo nyingi sana zihusuzo simu, pamoja nazo kuna wimbo wa kuitwa “Namba ya Simu” uliofanywa na jamaa wa kuitwa Formula, hii naweza kusema ndio hasa ilifungua njia ya nyimbo nyingi za aina hiyo.
Leo Segment hii imeona sio kesi ikabonga machache na Formula kuhusiana na wimbo huo na mengine mengi.
Kwanza kabisa bro, kwa nini Namba Ya Simu?
Yap yap, kama unakumbuka nyimbo nyingi enzi hizo zilikuwa zinatoa hitimisho. Nikataka nije na story ambayo itawaacha wasikilizaji njia panda ndio nikaja na Namba Ya Simu. Naamini utakubaliana na mimi kama hii ndio ngoma ya kwanza ya kibongo kutokuwa na hitimisho.
Idea ilikubalika maana track haikupata airtime kivile so hii ikafanya wasanii kadhaa wai copy idea. Ukianza na Wrong Number ya Sna Lee na story ya Soggy Kibanda Cha Simu. Ikumbukwe Namba Ya Simu imerekodiwa December 2002 baada ya kupata pesa ya vitabu chuo na kutumia kurekodi huo wimbo.
Hivi yule dada aliyechagiza katika wimbo (Angel) ni nani hasa?
Yule ni msanii nilimkuta MJ kaja kurecord akijulikana kama Colour Gift ndio nikamuomba aingize zile sauti.
Nafasi ya kurekodi kwa Comorien ilipatikanaje? Na kwa nini iwe yeye na sio wengine hasa Miika Mwamba aliyekuwa karibu sana na Dully? Na vipi ushirikiano wa Comorien ulikuwaje kwa kipindi kile?
Kama nilivyokueleza kwamba, mimi ni muasisi wa Manyema Family ambao walikuja kushiriki shindano lililowaibua UVC, Neck Breakers hivyo kupata nafasi ya kurekodi kwa MJ (Records).
Nami nilipowapa wazo la kutaka kurekodi single yangu walinambia tukafanyie MJ. Mwanzo nilitaka Q Chief asimame kwenye chorus tukaenda maskani yake enzi hizo Zero Brain tukamkosa hivyo likaja wazo la kumfuata Dully. Dully alifurahi sana kufanya kazi na member wa Manyema Family kwa heshima ya rafiki yake aliyekuwa mmanyema aliyepoteza maisha huko Kigoma na ambaye kuna wimbo kwenye album yake amemuimbia (Haji Sadi).
Sikufanikiwa kwenda nae studio. Mi niliingiza vocal zangu kisha yeye akaenda kuingiza chorus.
Dully alinipa ushirikiano mkubwa na nakumbuka alisema nafanya hili kwa heshima ya rafiki yangu. Kwa jinsi alivyokamua katika Chorus ya Namba Ya Simu hadi Comorien akampa ofa ya kufanya wimbo wa bure. (Ladies Free)
Uandishi wa huu wimbo ulikuwaje? One take au uliandika kwa kadri mawazo yalivyokujia?
Mi ni storyteller mzuri sana. Baada ya kupata idea nilimaliza mara moja. Zipo tracks za story nyingi ambazo nimewahi kutunga japo hazikwenda studio.
Kufanana kwa idea za nyimbo za simu ulikuchukuliaje?
Kama nilivyosema huu wimbo umerekodiwa 2002 nikiwa mwaka wa kwanza pale Mlimani, fuatilia hizo nyingine zimerekodiwa lini kisha utajua nani ka copy kwa nani. Nadhani wakati hao wanarekodi hata Comorien alikuwa kashaondoka nchini.
Kuna changamoto ya kupotea nyimbo zikiwa studio kama ulivyonidokeza, unaweza kututajia kwa majina nyimbo hizo?
Kuna “Guitar Linasema Sorry” na “Box La Kadi” nilofanya na K. Basil. Hizi kwa kuwa sikuziachia naona inakuwa ngumu kuzipata. Box la Kadi ulifanywa na Marco Chali enzi hizo yuko Nash Records.
Unakumbuka mapokeo yalikuwaje baada ya kuachiwa kwa wimbo huu?
Kwanza huu wimbo ulichelewa kuachiwa. Ulikuja kuachiwa kwenye mwezi wa sita 2003 kipindi hicho mimi niko field Uvinza, Kigoma na hakukuwa na hizo radio za FM zikisikika kule hivyo walivyoona mwenye wimbo hatokei wakauweka kapuni. Hii ilinikatisha tamaa sana na muziki wa kibongo unaohitaji kunyenyekeana hivyo nikaongeza juhudi kwenye masomo yangu tu.
Zaidi ya Namba Ya Simu ni ipi ngoma yako ambayo unaikubali zaidi?
Mwaka 2007 nilikutana na Chege pande za Mwanza alipokuja Fiesta akataka tufanye wimbo mmoja unaitwa Introduction yaani kama ananitambulisha ila tulipofika kwa Q Mo Records ikaonekana kama chorus ya Chege inafanana na wimbo mmoja wa TMK ikabidi nifanye nae track nyingine inaitwa Guitar Linasema Sorry feat Chege & Geez Mabovu. Hii ilikuwa true story dedicated to my girlfriend. Bonge la track. Chege alitamani sana niiachie maana alikamua mbaya. Naikubali sana hii kitu bro.
Shukran kwa ushirikiano bro.
Pamoja bro.
Pia mcheki Iddy Mwanaharamu mwandishi wa makala haya kupitia;
Facebook: Iddy Mwanaharamu