Uchambuzi Wa EP: DTP (Deliver The Package) NO EXCUSES EP
Msanii: Oksyde
Tarehe iliyotoka: 30.04.2021
Nyimbo: 7
Ma Producer na Wapiga Midundo: Mxshu, W4nj4u(Wanjau), Day Dro, Boomba Ye
Mchanganya Sauti na Midundo: Ndovu Kuu, W4Nj4u
Studio: Feel Hood Est
2001 ndio mwaka niliotoka kwetu Mombasa na kusafiri kilomita 1000 hadi Eldoret kwenda chuo kusoma. Mwaka huu ndio ilikua mara yangu ya kwanza kupitia vitu kadhaa maishani mwangu kwa mara ya kwanza; ilikua mara yangu ya kwanza kulala selo ya polisi (hadithi ya siku nyingine), mara yangu ya kwanza kuishi mbali na wazazi wangu, mara yangu ya kwanza kuiona Nairobi moja kwa moja na mara yangu ya kwanza kukutana na mwanangu Brian toka Nairobi kule chuoni, Eldoret. Hapa mwana Hip Hop toka Mombasa alikutana na mwana Hip Hop toka Nairobi.Brian ndio alianza kunipatia shule ya lugha ya Sheng kando na sisi kujengana ki mawazo juu ya mziki wa Hip Hop ambao ulikua msingi mzuri ulionisaidia mimi kuelewa mashairi ya ma emcee wa Nairobi.
Miaka 10 baadaye (2021) ndio pia nikaweza kupata fursa ya kumskia emcee Oksyde toka Kenya na kuweza kununua mradi wake wa 9. Wimbo wa kwanza wa mradi huu DTP (Deliver The Package) toka kwa Oksyde ndio umenipatia kumbukumbu niliyoitoa hapo juu kwani kwenye mradi huu emcee huyu ana mzigo muhimu sana ambao anataka usafirishwe toka Nairobi hadi La Costa (Mombasa inavyoitwa na watu toka Nairobi). Kwenye mdundo mzuka sana wa Drill ulioundwa na Boomba Ye, Okysde anatukaribisha kwenye mradi na kupitia mashairi yake anatueleza kua tunapaswa kuhakikisha tunafanikisha mipango yetu bila ya sababu yoyote. Anasema hivi Oksyde,
“No excuses this your calling don’t refuse it/
Eeh see mine is music that’s my drug I use it mix it fuse/
Kila tune ni bop in nigga really dope uki bump you can’t refuse/
Tick Tock bout to blow wana sema I’m the bomb you can’t defuse it/
Naleta nare Mwaki zaidi shinda vibiriti vifaru/
We are in the building mrazi yuko nje ananyongwa na waru/
Wachana na yee fala mang’aa bado yuwasha kinyaru/
Wachana na yee fala ni rat ye huchekeshwa na mambaru/
Wordsmith mdeadly very lethal na ka biro/
I don’t need hizo kiki ati G ni go viral/
Chunga ma Iscariot wako fogo hii kanairo/
Mjini ni gleasy serious tings we una jokes za Kajairo/
Wanariadhi wao hutuita mbogi ya nduki/
Eh, peng ni rider ye hu fly na squad ya nduthi/
She there on duty mzeya she a cutie/
Half Kenyan Half UG/
Ni mgenge but boogie/”
Wimbo huu una ubeti mmoja ambao unaweka msingi na kukuonesha ni nini ukitarajie ndani ya EP hii; mashairi ya kiujanja, sheng kwa wingi na Drill ya kumwaga.
Kwenye wimbo wa pili She Call Me Daddy mashairi ni ya kiutukutu ambapo Okysde anaelezea kuhusu mahusiano yake na peng-ting wake kabla ya kutupeleka kwa Rungu Kwa Mkono akiwa na Jovie Jov ambao ni wa bata flani ila Parental Advisory zinahusika kwa sana hapa.
Mbleina Akimblein ni wimbo flani wa tahadhari kwa wabaya wake ambapo Oksyde anawaonya watu wanaotaka kumletea ujinga watapigwa na chain. Mdundo wa wimbo huu umeundwa na Ndovu Kuu na uko bouncing flani ila ni mzuka sana kama we ni shabiki wa midundo dizaini hii.
Kwenye Tajua Hujui akiwa na Liquid Flowz Oksyde anaonesha mistari ya kiujanja anapotupa mistari kama, “Tempting/Natema vichafu utadhani mistari zi huandikiwaga kwa septic”. Nyimbo ya ubaya hii. Kwenye Kubaff akiwa na Abbas Kubaff wawili hawa wanapita na mdundo mzuka sana na legend Abbas anatukumbushia kua bado yupo makini na mashairi yake bado.
Wimbo wa mwisho ni kama kongamano la ma emcee kwani Trabolee, H.R The Messenger, Cafu Da Truth, Muddah na Liquid Flowz wanampiga support Oksyde kwenye Tuko Macho ambao ni wimbo kuhusu maisha ya utafutaji wakituambia kwenye kiitikio,
“Juu ya hussle tuko macho/
Tumemwaga damu machozi na pia jasho/
From the underground tuna mwok na vibasho/
Jiji ndani kugeuza scene ya commercial/
Ma tools zimesundwa kwa vibegi na zingine kwa kinena zimenasho/
Snitch aki chati chati mouth ana tresiwa gizani askumiwe kahasho/”
Kama vile Brian alivyonifundisha maneno kadhaa ya sheng wakati nilipokua nae chuo ambayo nimeyaskia ndani ya mradi huu kama vile; Uweri(Ushamba), Mboi/Imbo(Fake) na Woyes(Maji), Waru(wivu) basi Oksyde nae kaendeleza shule kwani kuna maneno kibao kusema kweli yamenipita kichwani ila ni fursa ya kuyafanyia utafiti ili kuelewa maana yake.
Mradi umeniwezesha nimfahamu Oksyde na mtindo wa kazi zake kwani ndio mradi wake wa kwanza niliopata kuuskia mwanzo mwisho. Oksyde amejitahidi ku Deliver The Package kwa hiyo na wewe nenda ukauskilize aidha kwa streaming apps au kwa kununua nakala ili umpe support mwenzetu, No Excuses.
Wasiliana na Oksyde kupitia mitandao ya kijamii;
Instagram: Oksyde