Ollachuga - A Town

Ollachuga ni emcee chipukizi anae patikana pande za Arusha Tanzania. Ni mwanaharakati aliejikita kwenye mziki wa Hip Hop na anatumia mashairi na mziki wake kama silaha zake za kuelimisha na kukosoa jamii.

Tukisubiria uzinduzi wa Kandamseto yake ya kwanza rasmi tumepata fursa ya kufanya mahojiano nae ili kumtambua chali huyu wa Chuga na kufahamu ni nini tofauti anacho kileta juu ya meza takatifu ya Hip Hop.

Karibu sana.

Karibu sana Ollachuga. Kwanza kabisa tuanza kwa kufahamu Ollachuga ni nani, anatokea Wapi, kazaliwa wapi na lini?

Shukran sana Micshariki Africa kwa fursa hii.

Naitwa Olais maarufu kama Ollachuga ni msanii,ninaye fanya muziki aina ya rap/hip hop. Nimezaliwa na kukulia mitaa ya Oladadai Arusha Tanzania

Mbona unajiita Ollachuga ?

Niliamua kujiita Ollachuga kwa sababu jina langu halisi ni Ollais na mkoa wangu ni Arusha/Arachuga kwahiyo nikaamua kuchukua OLLA kwenye jina langu na CHUGA kwenye a.k.a ya mkoa wangu ndipo likapatikana jina langu la OLLACHUGA.

Nini kilicho kuskuma kuanza mziki, hususan Hip Hop?

Kiukweli nilianza kupenda miziki ya aina mbalimbali tokea nikiwa kinda kabisa baada tu ya kupata akili ila mapenzi yaliongezeka zaidi baada ya kuanza kusoma shule ya msingi pale Oldadai, nadhani kwanzia darasa la 3 /4 na nikavutiwa na muziki wa hiphop zaidi. Kadiri muda ulivyokua unaenda ndipo nikaanza kwa kurariri mashairi ya watu niliokua nawakubali zaidi kama Watengwa, Nako2Nako, Waturumbi, Ex-plastaz,Fid Q,Proffesor Jay na wengine wengi.

Wimbo wako wa kwanza uliutoa lini?

Wimbo wangu wa kwanza kabisa kurekodi niliutoa rasmi mwaka 2014 unaitwa Chalii Wa A Town (https://mdundo.com/song/44746). Ni wimbo flani ambao ni kama utambulisho wangu, yani ukiuskiza kama una maswali kadhaa kuhusu Ollachuga; ni nani, anafanya nini yani, ukimaliza tu kuusikiliza unakuacha na majibu ya maswali yako. Nakumbuka nilipewa nafasi ya kurekodi bure kabisa ndani ya studio ya 313 GREEN HOUSE UsaRiver Arusha na bwana Ricardo Locha na Br Marungi. Mwenyezi Mungu awabariki sana hawa jamaa kwakunifungulia njia. 

Umeshatoa nyimbo ngapi hadi sasa?

Mpaka sasa nimekwisha achia jumla nyimbo kadhaa zikiwemo;

(1)Chalii wa Atown((https://mdundo.com/song/44746)

(2)Aibu yao (https://mdundo.com/song/51842)

(3)MwachieMungu(https://mdundo.com/song/44741)

(4) Siombi pesa (https://www.youtube.com/watch?v=XFIl0imI86Y)

Umeshafanya kazi na ma emcee  na wapiga midundo(beat makers/producers) gani hadi sasa?

Watayarishaji niliofanikiwa kufanya nao kazi mpaka sasa ni Br Marungi, De La P, Brodmore na Dr. Luis.

Umeandalia mashabiki wako nini baadae, EP, kanda mseto (Mixtape), au album ?

Nimewaandalia KITU CHA ARUSHA  MIXTAPE kama zawadi yangu kwao ya kufungia mwaka  a imetoka rasmi mtaani tarehe 12/12/2021 na bei ni Tsh.7000/= kwa Hard Copy (CD) na Tsh.5000/= kwa Soft Copy (Whatsapp &Email)

Nani ana ku inspire hapa bongo kama emcee ukimuona anakupa hamasa yakushika kinasa?

Kusema kweli sina mmoja kama mmoja ila kuna wachache. Ninao wakubali zaidi ni Chindoman ,Jcb Watengwe,Fazza Nelly,Sugu, Fid Q na Professor Jay

Nini kinachokufanya uwe tofauti ki emcee na ma emcee waliopo kwa game kwa sasa?

Utofauti wangu na wengine kwanza naona ni katika uandishi maana kwangu mimi asilimia kubwa ya ninachokiimba ni uhalisia wa yale yalionitokea maishani mwangu au katika mazingira yanayonizunguka. Pili ni kwenye ufundi wa mitindo ya uwasilishaji huwa sikaririki naweza kote kwenye Boombap na Trap pia kwenye topic hua sirukiruki kama ma emcee wa sasa kila siku stori za uhuni wakati kuna mengi ya kuongelea kwenye jamii.

Una andika au kuandiwa mistari yako?

Mashairi ya nyimbo zangu hua naandika mwenyewe,sijawahi kuandikiwa wala sitarajii.

Ndoto yako ni kufanya kazi na wasanii au waunda midundo (producer) gani?

Nina mipango ya kufanya kazi na wasanii wengi sana waofanya Hip Hop na miziki aina nyingine baadhi yao ni kama Chindoman, Warriors from the East, Jcb Watengwa, Fid Q, Stopper, Salu Tee, Rama Dee, Lay Jaydee, Grace Matata na wengine wengii. Kwa upande wa watayarishaji ni ndoto za kufanya kazi na Duke Tachez, Dx, P Funk Majani, Daz Naledge, Abby Mp, Marco Chali, Palla Midundo na wengine wengi.

Tumuachie Mungu uliiunda lini, wapi na nani producer? Nini kilicho kusukuma kuandika wimbo huu? (https://mdundo.com/song/44741)

Mwachie Mungu niliachia mwaka 2016 chini ya Lost Poetry Production kwa producer De La P. Kilichonisukuma ni mambo tu ya kimaisha maana kwa wakati huo nilikua kwenye kipindi kigumu sana maana tayari nilikua na majukumu na ramani zilikua hazieleweki. Kwahiyo kama wimbo wenyewe ukiuskiliza unavyojipambanua kuanzia ubeti wa kwanza mpaka wa tatu ni kwamba nilikua naongea na Mungu wangu na nikaamua kumwachia yeye magumu yote yanyonisibu anifanyie njia nivuke, ndio maana nikauita “Mwachie Mungu”.

Nini hukuskuma kuandika mistari yako?

Mimi huwa sina formula kwakua naamini kua muziki ni hisia kwahiyo hata nikiwa njiani nikipata hisia za kuandika naandika tu mashairi.

Shukran sana Ollachuga kwa mda wako.

Asanteni sana Micshariki Africa.