Uchambuzi Wa EP: For The Record II
Emcee: P-Tah
Tarehe iliyotoka: 04.06.2024
Nyimbo: 5
Midundo: Kunta Official Beats, Ransom Beats, Ares66, Sela Ninja
Mixing & Mastering: Aress 66
Studio: Big Beats Afriq, P-Mani Records, Truce Label

Nyimbo Nilizozipenda: Keep Moving Forward, Mwenda Pole, Decepticons,

P-Tah (Wa Furu) aka Tapi

EP kali art work kali na kazi zote mbili zinendelea kutoka For The Record (Tha Intro) hadi…. For The Record II, zicheki kwa makini….

Hapa ndipo nilipomalizia kwenye uchambuzi wa FTR (Tha Intro) na ndio tunavyoendelea kwenye FTR II…

‘Keep Moving Forward’ anashirikishwa underground emcee Adam Shule Kongwe kutoka Dom Down Click. Wanatutia moyo na kutuambia tuwe na shukrani kwenye jambo lolote lile tunalopitia maishani mwetu kwenye mgoma flani uliosukwa freshi na Kunta Official Beats kutoka Truce Label, Nairobi, Kenya.

Adam Shule Kongwe anakwambia,

Watu wa nyumbani kwenu wanasema unadose bure/
Ex girlfriend kutwa kusema ame dodge bullet/
Watu watasema, watu watacheka ila bro usinune/
Unapigika left right ila beba tu roho  kiume/
Haijalishi ka ulikwama na ulisha fanya vingi/
Haijalishi ka ulicheza na ulishazama kingi/
Haijalishi this haijalishi that
Saka ushindi/ usi wache past iku define/
We nenda kanyaga dingi/
Unastruggle unapelea fanya mambo we tembea/
Ni kweli muda unakimbia ila bado haujachelewa/
Piganisha,kuwa na imani piga misa/
Akili za kichopy na imani utashikanisha/
Usilale kumbuka dream usiwaze kuanguka chini/
Njoo na lemonade maisha yakifanya kukupa ndimu/
We usiogope ka si poa stress zote utazitoa/
Keep moving kama Rocky Balboa/”… 

P-Tah anaendelea kututia moyo akisema…

“That's how you triumph ukipitia trials/
Windows closing hapana gwaya/
Most high Sir ata sababisha ukibisha/
Kuanguka isiwa kutisha/
Been there got tha t-shirt/
See me trying coz trying is all you can do/
Extending upendo kwa wote siku zote/
Mantra ikiwa Ubuntu nikichorea comfort zone/
On my path trying inengi occupations/
Maisha ni jamo, siwezi kaa kwa jamo station/
Hata bila spare, mans never scared au ku-despair/
I hit rock bottom, I know how high I can get/
Never forget with a grateful heart/
Kuna mengi ya kuwa thankful for/
There is beauty in tha struggle, especially ukijiokoa/
Come on, failure si failure/
Come on, one more try/
One more try/”

‘Mwenda Pole’ anashirikishwa mtu mzima Sir-Bwoy. Hii ni mara ya pili kwa wawili hawa kufanya kazi pamoja toka washirikiane miaka kadhaa kule nyuma kwenye party banger lao ‘Serereka’. Hapa pia mwendo ni ule ule wa kula bata na kujirusha mdagi mdagi kwani hawakukosea wazee waliposema mwenda pole hajikwai.

‘Decepticons’ ni kama ngoma flani ya kinabii ambapo jamaa wanaongelea siasa za Kenya na ukiona vile mambo yalivyoenda hivi karibuni kwa majirani zetu utakubaliana nami. Ares66 ndo kapita na mdundo hapa ilhali Cafu Da Truth na P-Tah wanatuonesha vile wanasiasa ni waongo na vigeugeu ila ma emcee wetu washawasoma.

‘Apollo’ mdundo pia kaandaa Ares66, Boombap ndo msingi na nondo ndo uzito wa mistari ya majigambo kutoka kwa P-Tah. Jamaa akijisifia vile yeye ndo mbaya, wa kwanza, Apollo ki miungu wa kigiriki.

Sela Ninja na Old Skool Local, kutoka Kigambonino (Nino Nino), Dar Es Salaam, Tanzania na P-Tah akiwakilisha Buru (Buru Buru) Nairobi, Kenya akiwakilisha wanakwambia kuwa ‘Sio Kizembe’ kwenye mdundo wa Sela. Nilipenda vile P-Tah kama mwenyeji kwenye goma hili alivyokuwa anapokezana kinasa na wageni waalikwa.

Imeshaandikwa kuwa P-Tah anaendelea kujinoa ili awe emcee bora na hakuna njia nzuri ya kuweka kumbukumbu kama kutupatia miradi ya For The Record (The Intro) na For The Record II.

Kwa mawasiliano mcheki P-Tah kupitia

Facebook: P-Tah Wa Furu
Instagram: @p_tah
Twitter: @pmanirecords1