Uchambuzi Wa EP: On My Case 2 (OMC2)
Emcee: P-Tah (Wa Furu)
Tarehe iliyotoka: 17.07.2022
Nyimbo: 8
Watayarishaji: Ares 66, Evano, Ransom Beatz, Afrvka, Kunta Official Beats, Alex Vice
Mixing & Mastering: Ares 66
Studio: P-Mani Records
Nyimbo Nilizozipenda: Misunderstood, Freedom Of Expression, Vices, Wealth Generational, Great, Turn Off The Light
P-Tah (Wa Furu)
P-Tah (Wa Furu) ni jina la kisanii la Peter Mutisya ambaye ni rapper anayetokea kule Buru Buru, Nairobi Kenya. Emcee huyu ambaye nilianza kumfahamu mwaka jana alipotoa EP yake ya 5 jina On My Case 1 pia tulifanikiwa kumhoji ili kuweza kumfahamu zaidi.
Emcee huyu aliyeanza kughani miaka miwili iliyopita wakati wa janga la Uviko 19 amejitahidi kujinoa ukizingatia alijifunza kuchana akiwa chumbani kwake akiwa lockdown kule London ambapo ni makazi yake. Baada ya kununua vifaa flani ili kuweza kujinoa, emcee huyu alianza kuandika na kujirekodi mwenyewe juu ya midundo ya watayarishaji tofauti kama njia ya kuondoa kuboeka na kujiweka busy akiwa lockdown.
Mwaka huu baada ya kushiriki kwenye Door Knockers Cyphers 1 emcee huyu aliingia studio na kuanza kutuandalia mradi wake wake wa 6 On My Case 2. Emcee huyu aliachia single ya kwanza, Freedom Of Expression mwezi wa nne. Ngoma hii ambayo ilitayarishwa na Ares 66. Ngoma hii inamkuta emcee huyu akiangusha nondo mwanzo mwisho bila kiitikio inamkuta emcee huyu akiongelea uhuru wa kuongea na pia anakuwa huru kuongea na anafunguka kuhusu maisha yake kidogo na changamoto alizopitia akisema,
“Koma to KDO, dry spells filled my heart with fury/
Can’t lie man never missed meals/
Au lacked fees nashukuru wazazi/
My struggles were mental/
Convinced my existence ilikua accidental, by my own mental/
Begging to fit in, gravitating to repellents/
Nikidhani watanipenda, bila guidance/
Dress code ilikuwa barmy was not cool like them/
No matter what I spend, nikitaka to end it all/
Low moods had to climb tall trees macho Chinese/
Umri mdogo juu ya mitungi niko deep end/
Paranoia but nagwaya kumeet shei-to/
Suicidal thoughts, what kinda talk is that? /
Hii ni afrika we don’t tolerate weak minds, ndio echo za society/”
Baada ya Intro (Money, Power, Respect) kufungua mradi huu rasmi emcee huyu anafunguka kuhusu changamoto za kuwa Misunderstood kwenye ngoma iliyosimamiwa na mtayarishaji Kunta Official Beats aliyetumia sampuli ya mwimbaji gwiji toka Marekani, Nina Simone akisema kuwa Nina kamuwezesha ku See More.
Alex Vice anachukua doria kwenye kwenye Vices akiongelea maovu yalivyojaa kwenye jamii yake pamoja kabla ya kushirikiana na Brima Maovete kwenye Wealth Generational, wimbo unaotuhamasisha kujenga urithi kwa ajili ya vizazi vyetu vya baadae. Ma emcee hawa wawili wanashirikiana vizuri kutueleza ndoto zao za kuomoka akisema P-Tah,
“Kutofautisha investments na savings/
Nikafunge ka Jay au ‘Ye/
Hey a few billi’ mbona ni Kim Ye?”
Kando na emcee Brima aliempa support kaka P-Tah, emcee huyu amemshirikisha mwimbaji Dyana Cods wa River Lake Nilote kwenye wimbo flani mzuka sana wa ki utu uzima, Turn Off The Lights. P-Tah anampa dada huyu nyama ya ulimi yenye uwezo wa kumtoa nyoka pangoni akisema,
“We ndio my eyes zina see mama/
For you always nita see mama/”
Mashairi ndani ya mashairi.
Kwa mtu ambaye alianza kujifunza kuchana kama njia ya kujitibu kutoka kwa madhara ya lockdown emcee huyu amepiga hatua ki mada ila naona anaweza kuboresha uwasilishaji wa mashairi yake ili askike vizuri zaidi. Tenje yangu itapiga On My Case 2 kwa muda.
Mcheki P-Tah kwenye mitandao ya kijamii;
Facebook: P-Tah Wa Furu
Instagram: p_tah