Toka kwa: Papaa Frege
Wimbo: Moyo Na Akili
Albam: Single
Tarehe iliyotoka: 05.02.2021
Mtayarishaji: Ghost Kifaa
Mixing & Mastering: Ghost Kifaa
Studio: Action Records
Beti Ya Kwanza
Kama unavofahamu, binadamu tumeumbwa kwa udongo/
So niko hapa kutoa tofauti ya Moyo na Ubongo/
Jua ubongo ndo unaokupa we akili ili upate fikiri/
Ila Moyo hauna akili wenyewe unadeal na mwili/
Kufanya upumue uonekane kiumbe mahiri/
So nashangaa unavochanganya kazi ya Moyo na Akili/
Jambazi akiua utasikia ana Moyo mgumu/
Sa Moyo unahusika vipi.?. Hiyo ni Akili ngumu/
Mtoto akikataa Shule hana Moyo wa Kusoma/
Sio kwamba hana Moyo wa kusoma, ni akili imegoma/
Usijipe Moyo, we utakuwa na Mioyo miwili?/
Cha msingi stay positive yaani itune akili/
Kila unachofanya, fanya akili yako iwe chanya/
Ukiamini ya kwamba Maulana inawezekana akakupa/
Jua akili haiwezi kufanya Moyo wako ukasimama ila Moyo wako ukisimama na akili imekufa/
Kiitikio
Tunatofautisha, Moyo na Akili si Sawa/
Usije fananisha Moyo na Akili si sawa/
Basi feel hii ndo difference/
Njoo feel hii ndo difference/
Basi feel hii ndo difference/
Njoo feel hii ndo difference, difference (Heee)
Beti Ya Pili
Ukisema mapenzi yapo Moyoni me nakataa/
Jiulize kwa nini mapenzi hayapo kwa Kichaa/
Si ana Moyo hapo ndo ujue mapenzi ni akili na sio Moyo kama wengi wao wanavyofikiri/
Eti nampenda mpenzi wangu kwa Moyo wangu wote/
Hiyo sio kweli sema nampenda kwa akili zangu zote,/ maana akili ndo inayokufanya uamue,/ Kwenye mapenzi Moyo unakuwepo kufanya upumue/
Ujue hatufanyi kazi kwa Moyo bali juhudi/
Na juhudi ni baada ya akili kufanya maamuzi/
Ila Moyo unakuwepo pale kwa makusudi/
Baada ya akili kuamua wenyewe kuhusika na pumzi/
Kila unachofanya, fanya akili yako iwe chanya/
Ukiamini ya kwamba Maulana inawezekana akakupa/
Jua akili haiwezi kufanya Moyo wako ukasimama ila Moyo wako ukisimama na akili imekufa/
Kiitikio
Tunatofautisha, Moyo na Akili si Sawa/
Usije fananisha Moyo na Akili si sawa/
Basi feel hii ndo difference/
Njoo feel hii ndo difference/
Basi feel hii ndo difference/
Njoo feel hii ndo difference, difference (Heee)/
Beti Ya Tatu
Mbele ya kipaza Mic check One Two/
Kazi ya Moyo ni kusukuma Damu tu/
Kama kupenda hiyo ni kazi ya Akili/
Kwanza mnaupakaziaga Moyo hauna siri/
Ukiwa na Moyo mkubwa maishani ni kitu hatari/
Ila ukiwa na Akili kubwa maishani we ndo hatari/
Pia unaweza ukaishi bila kuwa na Akili/
Ila bila Moyo (mmh) nadhan una jibu la hili/
Moyo hudhurika wa pili baada ya Akili kuteswa/
Akili ikiwaza sana mzunguko wa damu unaongezeka/
Ukiongezeka hapo ni Moyo unateswa/
Na so soon jiandae Moyo kupandwa na Pressure/
So, ifanye Akili iongoze Akili iongoze Moyo uongoze Mwili/
Badili mawazo ambayo ni batili/
Ukishakiri kwa Akili na Moyo ndo unasubiri/
Kupokea taarifa utitiri ambazo unafikiri/
Kiitikio
Tunatofautisha, Moyo na Akili si Sawa/
Usije fananisha Moyo na Akili si sawa/
Basi feel hii ndo difference/
Njoo feel hii ndo difference/
Basi feel hii ndo difference/
Njoo feel hii ndo difference, difference (Heee)/