Patrino ni mmoja wa watayarishaji wa Hip Hop wanaopatikana handakini mwa Tanzania aliejikita kwa midundo ya Hip Hop. Mtayarishaji huyu ambae ana taaluma yake ya mambo ya fedha (banker) amejulikana sana kutokana na midundo yake yenye ubunifu na utubhutu. Leo tumepata fursa ya kupiga gumzo na kaka Patrick aka Patrino (On The Beat!).
Karibu sana Micshariki Africa kaka Patrino. Kwanza kabisa tuanze kwa kufahamu majina yako rasmi na unajihusisha na mishe gani?
Asante sana. Kwa majina naitwa Patrick Kapongwa a.k.a Patrino, mimi ni banker nafanya kazi katika benki moja hapa Sumbawanga Manispaa pia ni producer na beat maker!
Tueleze kuhusu historia yako ya kimaisha, ulizaliwa wapi, ulisomea wapi na kimasomo umefika hadi wapi? Kifamili mpo wangapi na maisha yako ya utotoni hadi ujanani yalikuaje?
Nimezaliwa Sumbawanga,nikasoma elimu ya msingi Jangwani Primary School na sekondari St.Maurus secondary school hapa Sumbawanga,then A-level nkasoma Sangu High School jijini Mbeya, then nikagraduate degree Dodoma University(UDOM) 2012 katika familia yetu tupo watoto sita ambapo wa kiume ni watatu na wa kike ni watatu pia. Mimi ni mtoto wa nne kuzaliwa.
Maisha yangu toka utoto mpaka ujanani yalikuwa kawaida maana tumelelewa katika misingi ya kumcha Mungu na wazazi wangu walikuwa watumishi then baba akawa mfanyabiashara (R.I.P).
Tueleze kuhusu historia yako ya kuwa mtayarishaji, ulianzaje hii safari hadi hapa sasa umekuwa mtayarishaji anayeaminiwa kutokana na ubora wa kazi unazozifanya?
Nilianza kujifunza utayarishaji wa muziki nilipokuwa Chuo UDOM mwaka wa kwanza na nikiwa na jamaa yangu CRUNK (Frank Nolasco) ambaye alinikutanisha na LUIS wa north block record Arusha ambapo nilianza kupenda production hasa kutengeneza beats wakati tupo UDOM pia Hans Q wa Dar Es Salaam ambapo walikuwa wanatufundisha jinsi ya kucompose beats kwenye FL Studio.
Jina lako la kazi Patrino lilikujaje na linamaanisha nini?
Jina langu la kwanza ni Patrick, jina la Patrino lilitokana na kupenda sana majina ya Latin America ambayo mengi yalikuwa yanaishia na herufi no,kwa hiyo katika kucheza la maneno nikaona Patrino itakuwa identity yangu na ndipo ilipoanzia hapo.
Vipi mapokezi ya wazee wako ulipojitosa kwenye shughuli hizi za muziki na utayarishaji, je walikubali na kusapoti uamuzi wako?
Mama yangu ndiye mzazi aliyebaki na mze wangu alifariki wakati nipo form five sijaanza hata beat making na production kwa ujumla,ila mama alikuja kujua wakati naporudi likizo nilikuwa nagonga beats sebuleni kwa hiyo akaambiwa nina make beats, hakupinga zaidi alinisapoti na akanipromise nikimaliza chuo atanifungulia studio.
Inapokuja kwenye utayarishaji vitendea kazi vyako ni vipi kwa upande wa vyombo vya muziki, hardware na software?
Kwa sasa sina studio zaidi huwa na compose beats nyumbani kwangu then naenda studio kwa jamaa zangu kwa ajili ya mixing na mastering (Finalizing), software natumia FL Studio na hardware natumia AKAI MPD na MPC.
Najua umepiga kazi na wasanii tofauti tofauti. Ni nani baadhi ya wasanii uliopiga nao kazi? Ni miradi gani uliohusika kuiandaa au unaimiliki kama yako iwe ni mixtape, album au EP? Je umeshafanya kazi na wasanii nje ya Tanzania?
Nimefanya kazi nyingi na Momumo, Wabibi Mc, Obby Mjuzi, Swanga The Conscious, MaKaNTa kwa ujumla na wengine wengi nimewasahau. Pia kuna jamaa wa nje ya Tanzania alifanya ngoma na Lugombo na Obby Mjuzi sikumbuki ni wapi ila ni Africa magharibi.
Kando na hizi mbanga za utayarishaji huwa unapiga shughuli gani za kukupatia kipato?
Mbali na utayarishaji mimi ni Banker nafanya kazi Tanzania Commercial Bank ambayo zamani ilikuwa ikiitwa Posta Bank au TPB bank.
Ni manufaa gani umeyapata mpaka sasa kupitia shughuli hii ya utayarishaji?
Mafanikio niliyoyapata zaidi ni kufahamika na kufahamina na watu wengi....I just do it for the Kulture!
Moja ya midundo yako ulitumika kuandaa promo za TMT. Unajiskiaje kuona kuwa kazi yako imebarikiwa na mashairi ya ma emcee kibao?
Hii kitu ilinifanya nikapata nguvu kubwa ya kucompose more beats mpaka leo na imenifanya kufahamiana na watu wengi sana katika utamaduni wetu wa Hip Hop.
Jingle yako "Patrino On The Beat" ilikujaje?
Hii jingle aliitengeneza mwanangu mmoja yuko Iyunga Mbeya anaitwa Step Father(Mike Sangu) ni producer pia Ila mimi ndiye niliyeweka sauti yangu na nyingine ile ya "Patrinoooo" ni mimi niliweka sauti ila alimix Shabba tune ambaye ni producer yupo Sumbawanga.
Je wewe Patrino unamiliki studio yako mwenyewe?
Kwa sasa nipo na home studio ambayo natumia kucompose beats only!
Muziki wa Hip Hop ugumu wake kwenye soko letu la Africa Mashariki ni kuwa haliuzi sana kama waimbaji kwa mfano wa Bongo Flava. Nini kifanyike ili tuweze kuwafikia mashabiki zaidi?
Mziki wetu wa Hip Hop tukiamua kuuza tunaweza zaidi ni kuimarisha katika platform zetu na wasanii kujielewa, hatuwekezi nguvu nyingi kwenye kuuandaa zaidi tunaishia kuskiza geto tu! Pia media zetu nyingi wanatuweka kando sana ni kama hatuna presenters wenye uwelewa na utamaduni wetu (Big up kwa Jabir Saleh EFM!)
Una ushauri gani kwa ma emcee na watayarishaji chipukizi?
Ushauri wangu ni kwamba real recognize real. Emcee na producer tunategemeana kwa kila mmoja tukishirikiana tutafanya kazi nzuri!
Gharama zako za kazi zikoje na je mtu anayetaka kupiga kazi na mtu akitaka kukucheki atakupata vipi?
Gharama zangu ni maelewano tu, sina fixed costs zaidi tunatofautiana kipato na mi nafanya for the kulture kwa hiyo ni maelewano na Emcee na napatikana kwa namba: (+255)717696875 na (+255)736696875 au
Facebook: Kanyuka Patrino Kapongwa
Instagram: patrino_anno_domino
Changamoto unazokabiliana nazo kama mtayarishaji ni zipi?
Changamoto ni watu kuchukulia poa kazi tunazofanya wengine wanajua ni rahisi tu...jibu ni kwamba kama rahisi wanavyochukulia wafanye wao basi…over!
Je wewe unachana na pia unapiga vyombo gani vya muziki?
Nilikuwa nachana wakati nipo O-Level na A-Level ila kwa sasa sichani kabisa ila nafundisha jinsi ya kuchana tu the extent.
Ni kipi cha mwisho ungependa kutuambia ambacho sijakuuliza?
Mengi umeniuliza mkuu...ila nachopenda kusema nashukuru kwa kunipa nafasi hii na kutambua mchango wangu,sikujua kama watu wanafahamu hiki kidogo nachodeliver kuwa ni kikubwa zaidi...be blessed sana!
Asante sana!