Toka kwa: Pizzo Madawa
Wimbo: Sigara
Albam: Panga Mbili
Tarehe iliyotoka: 01.11.2020
Muunda Mdundo: Wise Genius
Studio: AMG Records

Beti ya kwanza

Wengi wananichukia,nakusema mi m-baya/
Harufu ninayo nuukia ni chafu zaidi ya malaya/
Japo majina mengi,kizungu na kienyeji/
Wengine wanaiita fegi,nikiwashusha na kinywaji/
Wanatabasamu,ile koo naisuza vyema/
Ni kitabu cha ufahamu, huwezi juwa ninachosema/
Hatari kwa afya yako,dogo soma haya maandishi/
Wajuze na wenzako,mi na cancer hatarishi/
Wapo niliowatoboa, maini na mapafu/
Japo wengi nimewatoa, duniani na sasa wafu/
Nauzwa Bei nafuu,kwa Wakushi bati mbili/
Chanzo kifua kikuu,tena nadhoofisha mwili/
Kama pato la taifa,nabeba huu uchumi/
Ni janga la maafa,ninayetamba bila uvumi/
Wananita Marlboro/
Ama Sweet Ice Berg/
Hawavuti Kama ugoro,sina stimu kama geji/
Mangi washa poti/
Embassy ama Master/
Baridi sina koti,na hisi ngiri nitapata/
Japo navunja heshima,ya mtu kwenye jamii/
Wa kinenge ntawanyima,mnao gongea bila utii/

Beti ya pili

Kaka huwezi amini, sigara waumini wengi/
Wengi ni miaka ishirini,kuacha bado hawapendi/
Mapenzi matamu,Moshi ulale kifuani/
Hata mangi anafahamu,ndilo deni kwa jirani/
Rafiki wa vijana,anayeuwa taifa la kesho/
Bado kifua nabana,pumzi inakata michosho/
Voko inaharibika,kisa moshi kwenye koo/
Sauti mbaya kuskika,stegi ni mvivu flow/
Sijatunza silesile,zote nanunua sigara/
Vipisi Kama mchele,wana wameshiba madhara/
Sijabadilika ,ila mwili umekonda sana/
Ninavyo taabika,mapafu yalidanja jana/
Dogo acha sigara, ulimwengu unakudanganya/
Hujajua Kuna hasara,wazazi utawa changanya/
Uvutaji wa sigara/
Ndo alama za shetani/
Hakuna tiba m badala,ni uamuzi tu kichwani/
Fundi chonga jeneza,ukishindwa kuacha sigara/
Shtuka machale yanacheza,hii kitu kina madhara/
Waache wajichinje wenyewe,maana sanda shuka lao/
Afya ujilinde mwenyewe, uvutaji karaga baho/