Toka kwa: Pizzo Madawa
Nyimbo: Vita ya kale
Album: Panga Mbili
Beat Producer: Wise Geniuz WG

Toka kwa vesi la kwanza (Verse 1)

Omukama Kasagama,Maleale wa Malangu
Bwana Heri na Chagama, upendo kijiji changu
Sarange chief Machemba,Hip Hop naishi ki Bantu
Unguja Visiwa Pemba,mi Menelik wa tatu
Nawatuma vibaraka, ni Akida Na Jumbe
Afrika sina mipaka, chora ramani nitimbe
Mifumo ki Ubugabire,naishi ki Nyarubanja
Hili pori Tarangire,rafiki sungura mjanja
Ukoo wa Chief Merere,mtawala wa bonde la Usangu
Skia sauti ya kengele,usiogope ni ujio wangu
Kiongozi Olaiboni, ishara tosha mi Mmasai
Kwa michoro ya mapangoni,nawapa historia hai
Jaja wa Opobo, napiga Vita Koi Koi
Sitaki urafiki wa Ndorobo,mwaisha mwanga wa koroboi
Nimetimba Sundiata, Chaka la Mansa Musa
Ile Pwani ya Mombasa, Kona utamu wa sambusa
Wapi Dedan Kimathi,mi Mashona na Ndebele
Mirambo kichwa Cha kazi,chunguza ubongo wa Nyegele
Watoto nyungu ya mawe, Ni Nama na Maherero
Dingi swayo usipagawe,Mi nasifa ya ukachero