Toka kwa: Plate MdaiJasho akiwa na Jaheem Massacre
Nyimbo: Mpwa
EP: TuTaLeTa EP Vol 1
Tarehe iliyotoka: 20.02.2021
Muunda mdundo: Mwamba Mgumu (Sima on the Map)
Studio: Nexus Studios
*Beti ya 1*
Mafanikio si lelemama/
Jitoe sadaka ili uweze kusisimama/
Usiwe mtu wa kulalama/
Acha lawama Mungu kakupa karama/
We ni hero sio zero pambana inawezekana/
Kwenye tatizo ndo kunamafanikio/
Suluhisho kwako fursa na msaada kwa wenzio/
Jichange change tu upate kianzio/
Jichanganye kwenye watu kisha tega sikio/
Sikiliza mawazo ya wenzako/
Story zikuonyeshe mwanzo/
Pata ushauri kwa watu wakaribu yako/
Wakupe maoni chanya yawe ni nguzo kwako/
Sio wote watakao kuelewa/
Wapo watakaokupuuza kaza bado hujachelewa/
Wakikufukuza muda unawapotezea/
Waombee maisha marefu waje kujionea/
*Chorus*(Jaheem Massacre)
Mpwa nakueleza kwa uwazi/
Epuka papala acha masihara Dunia Kitanzi/
Nenda kasi Usichelewe/
Mingi Mikakati inakutazama wewe/
*Beti la 2*
Malengo yako sio ya kupuuzia/
Utatusua kama kweli unayo nia/
Ukipania kuwa utakuwa/
Ukisikilizia utakuwa unazingua/
Siku zinakimbia,tengeneza njia/
Ili ziweze kupitia,zikwachie japo mia/
Yakutumia uache kutumikia/
Mabwanyenye, mapepari wa hili soko huria/
Bora ugali bila masimango/
Kuliko wali na kuku huku unapigwa mabango/
Weka mpango endelevu/
Usiombe hela omba hekima na werevu/
Uoga huo uoga huo/
Ukatae, upinge/
Kwenye kusaka maisha hofu ishinde/
Ukipata kidogo haitakiwa ulinge/
Jikinge,jishike,jiongeze/
Chamtu mavi kisifanye ujikweze/
Ongeza ukakamavu mpwa usijilegeze nakupa makavu uwe shupavu nikupongeze/
*Chorus*(Jaheem Massacre)
Mpwa nakueleza kwa uwazi/
Epuka papala acha masihara Dunia Kitanzi/
Nenda kasi Usichelewe/
Mingi Mikakati inakutazama wewe/