
Paul Prosper ni mchoraji mwenye style ya kipekee nchini Tanzania ambayo haifahamiki na watu wengi. Sanaa yake ya kubwa anayoifanya ni Scribble art ambayo kwa haraka unaweza kuiita kwa lugha ya Kiswahili kama mchoro bila mpangilio au naweza hata kuthubutu kusema machokoro ambayo mwisho wa kazi inakuwa mchoro wa kuvutia sana.
Kando na scribble art Paul pia anachora sanaa ya paintings pamoja ya uchoraji wa kidijitali yani digital art.
Leo tumepata fursa ya kumhoji ili kuweza kufahamiana naye na sanaa yake.
Karibuni.
Jina lako rasmi na unajishughulisha na nini kimaisha?
Jina langu ni Paul Prosper najishughulisha na uchoraji na ni mwalimu pia.
Tuambie kidogo kuhusu Poldrawingz umetokea wapi, ulikulia wapi, utoto wako ulikuaje na umesomea wapi na nini umefikia wapi hadi sasa?
Ni mzaliwa wa Mwanza Tanzania kabila Kerewe. Nimekulia kijiji cha Nyambiti kata ya Buzuruga wilaya ya Ilemela. Tangu niko mdogo nilikuwa napenda sana kuchora sikuwa interested sana na kile mwalimu anafundisha so mda mwingi nilikuwa nafanya yangu. Shule ya msingi niliyosoma ni Nyambiti na secondary ni Nyasaka zote za Mwanza Ilemela pia ni muhitimu wa chuo cha ualimu Bustani Kondoa mwaka 2019.
Unafanya art au sanaa ya aina gani?
Mtindo wa sanaa ninaotumia unaitwa scribble drawing.
Scribble art ni sanaa ya aina gani?
Scribble art ni michoro inayotungwa bila mpangilio(randomly) na kwa mistari dhahania(abstract lines) jumla bila kutoa dhana ya kuchorea(pen,pencil'spen) kwenye karatasi. The results are very loosely drawn. Sketchy artwork.
Kwenye shughuli hii ya scribble art ni kipi kimekugusa sana kwenye ujuzi wako wa kubuni?
Kilichonigusa ni kupenda kujaribu vitu tofauti japo naweza kufanya sanaa aina yoyote katika uchoraji
Ulijifunzaje hii sanaa ya scribble art?
Nimejifunza mtandaoni kupitia kwa mchoraji maarufu anayeitwa Vince low toka mwaka 2020
Poldrawingz, ni nini story ya nyuma kuhusu hili jina?
Poldrawingz ni jina la sanaa. Pol nimefupisha kutoka katika jina langu Paul alafu drawingz linawakilisha sanaa yangu ya uchoraji.
Tueleze kidogo kuhusu kazi yako, ni nini unahitajika kuwa nacho ili uweze kufanya hii kazi vizuri?
Kuna aina mbili za uchoraji; unaotumia karatasi na peni na digital. Mchoro wa karatasi unahitaji manila paper, pen(bic) na white pen pamoja na pen flani zinazokoza. Kwa upande wa digital kinahitajika computer na pad ya kuchorea au tablet.
Umekuzaje kipaji hiki hadi kimekupa ajira?
Mhhh, hasahasa ni mazoezi na ni nature, ni kipaji nimezaliwa nacho na tokea primary nimeanza kukifanyia mazoezi kwa sababu nakipenda, kwa hivyo mdogo mdogo nikiwa darasani hadi nilipo maliza shule nilikuwa nafanya mazoezi ya kutosha.
Nimejitahidi kufanya mazoezi hadi ku master hii na hivi majuzi nimeanza kujifunza styles za uchoraji tofauti kama vile painting, kuchora kwa penseli ile nime base na scribble art na sina mda mrefu na scribble art, nimeanza kuifanya 2020 na mpaka sasa hivi ndio zinaendesha maisha yangu kidogo, nashkuru Mungu.
Je unatafutaje fursa za kazi?
Asilimia kubwa ni mtandaoni; Instagram, Twitter pamoja na Facebook ndio sanasana natumia. Ila Instagram ndio inanipa asilimia kubwa ya kazi zangu. Huwa natangaza kwa ku post, ku share, ku sponsor na kadhalika.
Kazi zako hupatikana kwa bei gani?
Inategemeana na size ya picture na pia kama kazi ni soft copy au hard copy. Kwa soft copy kazi nafanya kwa Tshs 40,000.00 ila mtu akitaka na frame, printed (A4 size) Tshs 65,000.00 na A3 Tshs 100,000.00 na kuendelea.
Umeshawafanyia kazi na wasanii wa mziki hususan wa Hip Hop?
Ndio nimeshafanya kazi nje ya Tanzania na wateja wawili; mmoja ni mtu wa Nigeria na wa pili ni wa kutoka Marekani anaitwa Danny Breezy. Pia nishafanya kazi na Rapcha
Ilikuaje ukaamua kumchora Rapcha?
Rapcha ni mmoja kati ya wanamziki ninaowapenda pia ana ni inspire kwa kuwa ni rika langu.
Tofauti yako na hawa wachoraji wengine ni nini? Ni nini mtu akiona kazi yako atajua moja kwa moja hapa Poldrawingz kahusika?
Tofauti yangu na wengine ni style yangu ya mistari, scribble art ambayo sio wengi huifanya.
Muziki na uchoraji je vinaendana? We huskiliza mziki gani? Una miradi gani ya wasanii iliyotoka 2021 ambayo unapenda kuiskiliza mara kwa mara?
Ndio unaendana kwa sababu vyote vinatumika kama njia ya kuelimisha jamii kwani vyote vinaburudisha na kufurahisha.
Sana sana mie hupenda kuskiza nyimbo za Rapcha.
Mziki ninaopenda kuskiza ni Hip Hop na bongo flava.
Siku yako huanzaje?
Mara nyingi nikiamka asubuhi nasali, najinyosha kwa kufanya mazoezi na kucheza mpira.
Wewe unapenda nini sana kuhusu kuwa mchoraji na je ni kitu uliwahi waza kwamba utakuja fanya?
Napenda kuwa mchoraji kwa sababu ni mojawapo ya channel ya kuelimisha jamii, kuburudisha, kukosoa na vingine vingi.
Pia napenda kushirikiana na wasanii wenzangu hasa hasa bongo na kitu ambacho ningependa kukifanya ni kushirikiana na wasanii wa nchi nyingine pia.
Je kuna design au kazi ulioifanya ambayo unajivunia zaidi? Waweza nitumia picha/ mchoro wenyewe kama upo?
Mchoro niliojivunia sana ni wa Burna Boy pamoja na Wurld.
Kando na shughuli hii ya ku design una vipaji au talanta gani nyingine? Pia unafanya kazi gani nyingine tofauti na digital art?
Ni football freestyle, napiga sana football freestyle. Pia ni mwalimu, nimesomea ualimu ila sijaanza kufanya kazi.
Pia nachora kwa kutumia pencil, carry pencil, painting styles za acrylic art, pencil, kama style nne tofauti.
Je ni changamoto gani wewe huzipitia kwenye hii sanaa yako?
Changomoto kubwa kwangu ni vifaa kwani vina gharama kubwa sana, kwa vifaa professional sio chini ya Tshs 1,000,000.00, vina cost sana.
Una ushauri gani kwa artist yoyote anaeanza kwenye fani hii?
Ningewashauri wafanye zoezi sana, wajitahidi kuangalia tutorials
Mapokezi ya hii sanaa yako ya scribble art yakoje? Je watu wamekuelewa au wanaona machokoro kibao tu?
Sio wote wanaoielewa ila wachache wenye jicho la utofauti na wanaopenda vitu tofauti na kawaida ndio wanavutiwa sana na kitu ninachofanya.
Je unaushauri gani kwa yoyote anaeanza kwenye fani hii?
Nawashauri wafanye mazoezi kwa sana na wajitahidi kununua vifaa sahihi na kuangalia turotials zaidi, reference na anaweza pate reference kibao zipo za kuchora.

Mpate Paul kupitia mitandao ya kijamii:
Facebook: Poldrawingz arts
Instagram:poldrawingz
Twitter:poldrawingz