Kama utani vile lakini ndio ukweli kwamba Mandojo hatupo nae duniani.
Kama utani vile enzi hizo Mandojo na wanae wa kwaya Mighty Melody wakicharaza sana magitaa.
Mandojo akawa anafanya kiutani utani tu kitu ya kuitwa banjo, huku kwaya huku pia anafanya na bongofleva.
Kama utani siku hiyo pande za Arusha, Mandojo anacharaza gitaa na Domokaya akafika pale, kama utani vile nae Domo akaanza kurap kwendana na mirindimo ya gitaa. Ukatokam uziki mtamu ile mbaya.
Kama utani vile wakaanzisha crew yao na vile kila mmoja alikuwa ashaanza muziki kitambo, wakaona waanzie hapo hapo na badala ya kuanzisha jina jipya la kundi wakaona waweke kiunganishi tu so kundi lao likaenda kwa jina la Mandojo NA Domokaya.
Kama utani vile zikatengenezwa nyimbo kadhaa na baadhi zikarekodiwa pande za Arusha ila hazikuwa released. Kama utani tu kwa enzi zile lakini wenyewe walipenda wangepata nafasi ya kurekodi kwa Pfunk pale Bongo Records.
Kama utani vile siku hiyo uso kwa uso na Pfunk pande za Arusha. Kama utani vile jamaa wakajaribu bahati yao, wakachek na Pfunk na wakamuonesha ujuzi wao, Pfunk kama utani akawaambia nimewaelewa na nikirejea Dar ntawachek na kama utani vile akawaambia "na kazi yenu ntawafanyia bure kabisa, mna kitu nyie jamaa"
Kama utani vile, jamaa hawakuamini. Kwa enzi hizo kupata nafasi kurekodi Bongo Records haikuwa kitu rahisi na tena mnaambiwa na kazi yenyewe mtafanyiwa bure!? Kama utani vile.
Kama utani vile simu inaita na Pfunk anawaambia njooni Dar tufanye kazi. Ilikuwa kama utani lakini ndio muda wao ulikua umefika, jamaa wakajipanga kwenda Dar ila changamoto ikawa nauli, si unajua enzi hizo machalii walikuwa madogo tu.
Kama utani vile washkaji waliokuwa shabiki zao pande za A town wakaanza kuwaungia nauli, ungaunga mwana hatimae kama utani vile ikagonga elfu 70..
Kama utani vile jamaa hao ndani ya ndinga na wakaja Dar na harakati za kurekodi zikaanza. Hapa na pale mara ‘Nikupe nini!’? Mara ‘Wanoknok’ mara ‘Niaje’ mara albamu ya ‘Taswira’ ikaingia mtaani na kama utani vile jamaa wakawa wasanii wakubwa Tanzania.
Kama utani vile, jumapili mchana naona habari kutoka kwa brother Soggy, kwamba Mandojo amefariki Dunia. Daaah! Pumzika kwa amani brother Mandojo, hakika kifo hakitakufika kwa mara ya pili.
Kama utani vile daaaaah!
√---------
0617933365