Toka kwa: Rabi James
Nyimbo: Nyumba ya kupanga
Album: Single
Producer: Ringle Beats
Mchanganyaji sauti: John Bleized
Tarehe iliyo toka: 08.11.2019
Baada ya miaka mingi nyumbani
kuishi na baba
Nikatamani kuhama na mimi niende kupanga
Si unajua maisha ya home
Nikahisi nakosa uhuru
nikichelewa kurudi nyumbani
Dingi anabwata
Ndipo nilipo msaka dalali mzee kusaga
Nikapatachumba cha nje mtaa wa saba
Kodi yangu miezi 6 yanini sikuzembea
bora niwe huru maana maisha kujitegemea
Sasa nipo kwangu so naishi navyotaka
Hakuna wakunichunga, naruka na kula bata
Narudi usiku wa manane nipo tungi nimelewa
Nikihamua nakesha disco vumbi na masela
Ajabu kwamba ulipopita mwezi mmoja
Chumba nilichopanga ni vitimbwi na vioja
Ndani hakulaliki mauza uza mtindo mmoja
ndipo nilipohisi labda mchizi nimerogwa
Picha linaanza yapata usiku saa 9
naota majoka joka nakimbizwa kwenye nyika
Naota ajali mala gali imepinduka
Na mm ndo deleva watu shazi wamekufa
Nilipo amka nikagundua kumbe ndoto ni msala
Ila chakushangaza sakafuni nimelala
Miguu imejaa matope halafu nina ndala
Nimenyolewa nywele kichwani bonge la para
Hofu ikatanda na moyo kwenda kasi
Kijasho chembamba nikapigwa na bumbuwazi
Natazama kitandani kwa woga na papara
Nagundua kuna mtu kama mimi amelala
mala sauti za mapaka wanalia
Zinasikika ngoma na watu wanaitikia
Wakitaja jina langu kwa sauti za kugumia
Mwili ukakosa nguvu nilipowaza kukimbia
Ndipo nilipo amnini uchawi upo duniani
Ukiona mti unateleza jua siki ya kufa nyani
Mwili ukasimka kwa hofu isiyo kifani
Baada ya kuona vivuli vya watu kiwambazani
Mala mchanga kwenye bati
vishindo kwenye dali
Nikaanza kupiga mayowe
Nakuita majilani
Ghafla watu wakajaa
Ndipo nilipo ponea
Hodi wakanigongea kujua kilichonitokea
Namshukuru mungu kanihepusha na majanga
Wengi wakanishauri nikajikinge kwa waganga
Wengine wakanidokeza mama mwenye nyumba mwanga
Tangu hapo sitamani kuishi nyumba ya kupanga
Asubuhi sikutaka kuvunga
Nikafungasha vilago na kukihama chumba
Nikasamehe kodi nawala sikuiwaza
Nikarudi nyumbani nilipo chungwa na baba.
https://www.youtube.com/channel/UCG6cO3JCtvO0oB66D9xw3YQ
http://mdundo.com/a/6179
https://audiomack.com/song/rabi-james/nyumba-ya-kupanga