Msanii: Rap Poetic Grenades (RPGs)
Album: Grenades From North
Tarehe iliyo toka: 01.07.2020
Nyimbo: 12
Beats: Dels Beats, Joe Mic, Slimsal
Mixing and Mastering: Dr. Louis Markos (Louis), North Block Records

Joe Mic - J Yank - SlaiYank

Bomu la kurusha roketi yaani Rocket Propelled Grenades (mara nyingi hufupishwa RPG) ni silaha ya kombora inayo wekwa begani ambayo hurusha makombora yaliyo na kichwa cha vita cha kulipuka. Kule kaskazini mwa Tanzania, Arusha panapo mbuga na asili endelevu za utamaduni wa Hip Hop kuna aina tofauti ya RPG; kundi la ma emcee watatu wanaoitwa Rap Poetic Grenades (RPGs).

Silaha kuu ya vijana hawa ni mashairi, kinasa na midundo ambayo yote kwa pamoja ni silaha Tatu Za Moto.Waliomo kwenye jeshi hili shupavu ni Slai Yank (Apolinary Olomi), J Yank (Joseph Msechu) na Joe Mic(Joseph Michael). Vichwa hivi vitatu vina malengo ya kusaidia jamii kunyanyavua fikra, kujadili hisia, kuzungumza vitu kwa uhalisia wake, kuitisha hoja, kupinga, kuonya, kurekebisha na kuzindua vipawa vinavyo ishi.

RPGs ambao awali walikua wanajulikana kama QB walianza kuchana mnamo 2008 na walishawai kutoa album yao ya kwanza kwa jina Kilicho Bora ambayo iliundwa pale studio za NoizMakeh Arachuga 2011. Baada ya album hii ilifuatia mixtape iliyoitwa Madini Ya Handaki.

Mwaka wa 2020 RPGs waliibuka tena na album yao ya kwanza baada ya mda mrefu; Grenades From North. Album hii iliundwa pale studio ya North Block Records chini ya usimamizi wa Dr. Louis. Album waliita Grenades From North ili kuwakilisha North/Kaskaziki mwa Tanzania wanamotokea ma emcee hawa na pia North/Kaskazini jina la studio walipo undia album hii. Album hii imejaa makombora ambayo yanaelekezwa pakubwa kwa adui ujinga. Ma emcee hawa lengo lao kubwa likiwa ni kuamsha fikra zilizolala kwasababu ya adui huyu kwa kupitia mashairi yao.

Mradi huu uliwashirikisha ma emcee tofauti kama Nash Mc kwenye wimbo wa Ziwe Double kwenye mdundo uliyoundwa na SlimSal na pia Adam Shule Kongwe, Fred Lou na Neno Wa kwanza kwenye wimbo Twenzetu.

Makombora ya ushauri yapo kede wa kede kwenye album hii kama vile Wekeza ambapo majemedari hawa wanatushauri tuwe makina kwa vitu tunavyo wekeza akisema J Yank

“Acha upuuzi weka Kazi mbele/
Fanya ujuzi tenga Cash Daily/
Jenga ubuni acha uhuni tenda utashi tele/
Lenga Ukwasi Wewe/
Bidii kipaji acha ganzi twende/
Miliki taji hamna daz kwenye/
Hii Miradi yenye__Mitikasi, nyingi pasi zenye/
itikadi si ilimradi iende/

na pia kwenya Ghala ambapo wasanii hao wanajisema kua ni maghala ya ushauri na maarifa akisema SlaiYank,

“Leo nashona walipo chana/
Skia ladha/
Tega skio kwa kina ulishwe mada/
Ujue North kiundani skia ala/
Hizi zama/
Wee funga, nafungua mjadala huu/
Mii ni ghala ninaewalisha wale wajanja tuu/
Ujinga gharama tu/
Maarifa ndio mtindo huu/”

Pia nyimbo nyingine iliosimama ni Dau La Juu ilio undwa na Dels Beats.

Album hii ni kama bonge la movie ambapo ma Starring hawa watatu J, Slai na Joe wapo vitani dhidi ya muovu ujinga na wao wanasilaha za moto zakupanua wigo wa mawazo. Japokua mistari ni ya juu changamoto niliyo pata nikutofautisha sauti za majemedari hawa watatu kwani huu ndio ulikua mradi wa kwanza toka kwao kuuskia. Ila hili pia lilisaidi kutozingatia ni nani kasema nini sana badala ya nini kilichosemwa.

Kupata mradi huu wasiliana na RPG's kupitia

Facebook: Rap Poetic Grenades (RPG)
Instagram: rappoeticgrenades
WhatsApp: +255689459128