Toka kwa: Rap Poetic Grenades(RPGs) ft Nash Mc
Nyimbo: Ziwe Double
Album: Grenades From North
Producer: Dr. Louis - North Block Records

Verse 3: (J Yank Rpg)

Sasa kwanini mniandame/
Nikipita yote tisa haya kumi Mnitukane/
Na nikibisha mnaonya zisiumane/
Mna hila bila visa mnahakikisha Mi nikwame/
Aah!
Utata bado mtaka nidate/
Nachopata mnakata hata nisionje mkate/
Kila karata nnayocheza muikamate/
Rizki anatoa Mungu, vipi yangu muikumbate/
Hapana hiyo haifai/
Malipo ndivyo yalivyo dhamana hiyo haidai/
Ndo maana najichenga kivyangu sio majidai/
Yote mliyotenda kwangu kitambo nshayakinai, Naifuata ilipo Sinai/... Yeah!!!
Mniache nifanye kile nitakacho/
Nisikache nibane kila nipatacho/
Nizisake nikimbizane nikajichane Mi nitakavyo/
Nizidake msinibane nipigane niwezavyo/
Yeah!