Wabibi Emcee

Mmoja wa ma emcee ambao nimekuwa nikiwafuatilia kwa ukaribu ni Wabibi Emcee kutoka Tanzania. Baada ya kupata nakala yangu ya Mixtape yake Misingi nimekua nikisubiria kwa hamu na gamu album yake ambayo ilidondoka mapema mwaka huu inayoitwa Moment Of Genius.

REKUSA ilipata fursa ya kufanya mahojiano na emcee huyu ili kuweza kumfahamu emcee huyu na harakati zake nyingine kando na mziki.

Karibuni.

  • MkoKeNya

*Rudisha Elimu kupitia Ujasiriamali na Sanaa Asilia

Tunaomba majina yako kamili ya kitaifa, na je unawakilisha kutokea wapi?

Kwa majina naitwa George Frank Mwenda.

Kwa nini Wabibi Emcee hii nickname yako inamaanisha nini?

Wabibi Emcee limetokana na kwamba mimi ni mtoto niliye lelewa na Bibi tangu mdogo mpaka ukubwani mwangu nilianza kujiita mtoto wa Bibi lakini nikaona kuna haja ya kulifupisha mpaka Wabibi Emcee.

Vipi kuhusu career yako ya muziki ilianzia wapi, lini, na ilikuwaje mpaka kujihusisha na Hip Hop na kwa nini Hip Hop sio zuku ama kwaya?

Safari yangu ya mziki ilianza nikiwa darasa la nne nakumbuka nikiwa Njombe nilikuwa napenda sana kuchana mistari ya wasanii hasa Wagosi Wa Kaya miaka hiyo ndio watu kwanza niliopata fursa  ya mwanzo kabisa kusikia kitu wanachofanya nikavutiwa mpaka nikapenda kufoka na kuanza kuufuatilia mziki wa kufoka.

Kuanzia hapa nyumbani mpaka ughaibuni ni watu gani walikushawishi kupenda Rap Game?

Nmekuwa mpenzi sana wa muziki kiasi kwamba napenda muziki kuliko hata wachanaji wenyewe kikubwa sipendi kuona kuna upotoshaji kwenye maudhui. Ninaowafuatilia sana ughaibuni ni KRS One ,the late Sean Price, 2pac na wengine wengi.

Kwa upande wa nyumbani ni Salute T, Adam Shule Kongwe na wengine wengi.

Una kazi ngapi mpaka sasa kuanzia

  1. Single track
  2. Min-album
  3. Albums
  4. Mixtape
  5. Min-Mixtape

Wabibi Emcee:

  1. Nyimbo ninazo tatu
  2. Min album sina
  3. Albam nimeshatoa moja, Moment Of Genius
  4. Kanda Mseto ninayo Moja, Misingi
  5. Min-Tape sina.

Kati ya vipengele nilivyotaja hapo juu ni kipi kilikutambulisha vyema kwa game?

Kanda mseto ya Misingi na ndio imenipa mwanga zaidi mpaka sasa.

Kati ya vipengele tajwa hapo juu kipi unahisi kina manufaa kwako?

Kwa sasa nafikiri album ndio kitu chenye manufaa zaidi kwa sababu kinabeba dhana pana.

I am the b-boy who destroys all negative circumstances every day spiritually.
I am the emcee who reaches above poverty skillfully.
I am the graffiti writer who thinks and grows spiritually; I draw peace, love, unity and joy.
I am the DJ who delivers justice while cuttin', mixin' and scratchin' with life.
I am the Beat Boxer whose body expresses art through sound; I play GOD's instrument.
I am the Fashion that uncovers the fear and shame hidden in oppressive nations.
I am the Language that loves and never gets understanding amongst grown-up educators; I am the utterance of my culture.
I am known as Knowledge; I build and destroy, heal and inspire with the right combination of words.
I am the entrepreneur who presents expert negotiating that repeatedly escapes poverty's routine experiences, never exploiting unlimited resources.

I AM HIP HOP! I am not just doing hip-hop, I am Hip Hop! I am the Watchman in the tower of Hip Hop's Inner City urging my people to turn from sickness, hatred, ignorance and poverty, and be restored to health, love, awareness and wealth.
Hii ni sehemu ya page katika kitabu cha teacha KRS ONE kinachoitwa The Gospel Of Hip Hop Instrumental One
Kutokea hapa katika hayo maandishi tunapata nguzo tisa za utamaduni wa Hip Hop.
First Of All tunaanza na zile nguzo mama ambazo zipo 5.

  1. Emceeing (Emcee)
  2. Deejaying (DJ)
  3. Beat Boxing
  4. Graffiti
  5. B. Boy & B. Girl

Baadaye KRS ONE akatuongezea nguzo nyingine nne na kufanya idadi yake kufikia tisa

  1. Knowledge (Street Knowledge)
  2. Hip Hop Fashion (Street Fashion)
  3. Hip Hop Language (Street Language)
  4. Entrepreneurship (Street Entrepreneurship)

Huku bongo tukiwa katika mijadala isiyo na faida kuhusu nguzo za Hip Hop (Hip Hop Elements)

wenzetu huko ughaibuni tayari wameongeza nguzo ya kumi ambayo inajulikana kama

  1. Health and Wellness

Pia kutoka katika huo ukurasa hapo juu unakutana na Hip Hop Principles (Misingi ya Hip Hop) ambazo zipo nne

  1. Love (Upendo)
  2. Peace (Amani)
  3. Joy (Furaha)
  4. Unity (Umoja)

Pia hapo mwisho anasisitiza kwa kusema, “I am Hip Hop! I am not just doing hip-hop.”

Kupitia andiko hili ukiachilia mbali ya kuwa emcee ni vitu gani unahamasisha kati ya hizo nguzo 10?

Entrepreneurship sababu ni kitu pekee naamini kinachoweza kunifanya huru kwa sababu ujasiriamali unahitaji zaidi mpangilio wa muda sio kupangiwa muda.

Tujikite  zaidi katika Album yako mpya inaitwaje? Jina la album linasadifu nini?

Kuna nyimbo ngapi katika hiyo album? Guest Emcees katika album yako wako wangapi?

Na watayarishaji wangapi wamehusika? Imetoka au itatoka lini?.

Albam inaitwa The Moment Of Genius....ina nyimbo kumi

The Moment Of Genius imesadifu kwa maana kila binadamu ana kipaji chake alichopewa na Mungu na anahitaji kujitafuta ili kujua wapi kipaji chake kilipo binafsi naamini nitashindwa vyote ila ikija nafasi ya kuchana hakika na mimi nitaonesha Ugenius wangu. Kwa upande wa guest emcees wako sita.

Watayarishaji waliohusika ni wa nne Burnbob Wa Kitaa (R.I.P), Black Magician, Black Ninja na Patrino. Album ilitoka tarehe 05.06.2022

Burnbob ametangulia mbele ya haki, unamuongeleaje huyu jamaa kwa kazi ulizofanya nae?

Nimemzungumzia sana lakini kikubwa kuna session kwenye albam kwa ajili yake tu.

Tunaweza pata list ya track zilizopo katika Album yako mpya au bado ni confidential?

The Moment Of Genius Album Track List

  1. Introduction
  2. Moment of Genius
  3. Tumeishi Sana
  4. Ujamaa na Hip hop ft TK Nandeze
  5. Am feel Blessed ft T Breaker
  6. Kwa Masela
  7. Free Life

RIP: Burnbob wa Kitaa Special Session

  1. Kwako Baba ft Em One
  2. Medani ya Ushairi ft Nguti & Isanga Native
  3. Upendo ni Gharama ft Lastie Born
  4. Hip hop for Everybody ft Spy Emcee
  5. Autro

Kuna vitu ambavyo vinakuvutia katika game yetu ya Hip Hop? Je ni vipi? Je vipo ambavyo huvipendi? Je ni vipi?

Vinavyonivutia ni vingi; kwanza mitambao na midondoko kuna emcees wakali sana mpaka naogopa...Lakini pia sipendi upotoshaji wa kukusudia.

Kuna ngoma katoa Lugombo MaKaNTa kuhusu watu waliobobea wa Mbeya. Mimi nilikuwa makini sana kuhusu wachanaji waliotajwa pale. Kwa nini Mbeya imefanikiwa kutupatia ma emcee wazuri kila kukicha?

Nafikiri kaka zetu wametujenga na kutuwekea misingi ambayo inatufanya wengi kupita katika njia sahihi labda ni kitu ambacho wengine wamekosa fursa hiyo.

Wabibi kuna hii harakati yenu ya kutembelea wafungwa na wagonjwa kama sijakosea. Tueleze mlianzaje na nia na malengo ya mnachofanya ni nini ?

Harakati inajulikana kama TaLaNTa Ya MTaa Ibiza ina maana ya kila mtu kwa kipawa chake akitumie kuwatia moyo watu kwenye makundi mbali mbali yaliyotengwa katika jamii kama tunawatembelea wafungwa magereza, watoto yatima, wagonjwa na watoto ambao hawana wazazi lakini wameshindwa kuwasomesha kutokana na ugumu wa maisha tunachangishana na kufanikisha kadri ya uwezo wetu....ilianza miaka minne sasa ipo kwenye msimu wa tano lengo ni kuwaamsha watu kutambua sisi kama waafrika tunahitaji kuinuana kwa hali na mali.

Thanks buddah kwa ushirikiano wako naamini tukiunganisha dots tutapata makala bora toka kwako... Karibu tena.

Barikiwa sana…pamoja sana peace family

© REKUSA

Mfuatilie Wabibi ili kusapoti kazi na harakati zake kupitia mitandao ya kijamii;

Facebook: Wabibi Emcee
Instagram: wabibiemcee