Msanii: Ricky Remy
Wimbo: Bado
Tarehe: 02.07.2021
Mdundo: 9th Wonder
Studio: Kiri Records, Bjsound
Mixing: Bea (Kiri Records)
Mastering: Stuta (Bjsound)

Ricky Remy akiwa na video producer wa Bado, Lowkey Picasso

Utangulizi

(Hook) Life is a gamble when you win or lose/

Beti Ya Kwanza

Bado nipo hai ingawa wengi Bado wamekufa.../
Ingali naishi kwenye nchi ya kusadikika.../
Bado ni Africa maisha magumu ndani ya gurudumu ila viongozi ndio wanaotajirika......./
Sera ya kilimo kwanza imefunikwa na kubet.../
Nchi ya viwanda na umeme umesanda uwanda bridge..../
Bado hali duni maisha ya mtanzania na ndio utamaduni elfu10 wiki nzima unaiskia/
Bado elimu hakuna ishu watoto wanapotoshwa.../
Na huku walimu hawana kitu tangu uhuru ulipotoka.../
Because life like a gamble knife like Rambo.../
Don't make happy for children this life like Rango../
Bado wasomi hawana ajira Bado sikomi maana simuoni wakuonyesha dira..../
Ndani ya torati ya mtaa Bado yupo chindo.../
Mtu anandoa ukimuliza jibu Bado yupo single…/
Bado Afrika Tanzania ni maskini hofu inanishika mbona inasifika tuna madini..../
Mungu atupe nini gas, milima, bahari, mito, mbuga na vitu kibao nchini…/
Hatuna vita tunapokaa ni balaa mvua ikinyesha hutopita..../
Tembea mwisho saa sita wakikukuta ni msala kinachofwata we utajuta.../

Kiiikio

Tuna freedom lakini kuwa free Bado/
Tuna Kingdom lakini kuwa ma king Bado/
Mambo yaishe wala usiulize Rado/
Hapa tuna mishe mishe so tuko busy Bado. X2/

Beti Ya Pili

Bado ujinga na maradhi maadui zetu sote.../
Nishacheza sana kwetu na sijatunzwa chochote.../
Ndio chama chetu tupo nacho miaka yote..../
This world is not my home sito ishi siku zote.../
Bongo Bado sio matibabu bei ghali.../
Viongozi wakiugua ni ndege hawapandi gari../
Si mabwege tukiugua madokta hawatujali.../
Tunakufa wodini na madokta hawana habari.../
Bongo Bado majanga timu Simba na Yanga.../
Mpira sioni chochote wachezani ndumba na wanga../
Bado shirika moja na umeme haueleweki.../
Bea tayali washazima Tanesco kudadadeki..../
Usiombee nyumba iungue alafu uwapigie fire.../
Yaani mpaka wakishakuja iyo nyumba imeisha expire…/
Siyafumbii macho kwakuwa nayaona haya../
Kila Raisi anaekuja wanasema Bora Jakaya.../
Bado watakuja Tena karibu na uchaguzi.../
Wataleta mipila kofia kanga na jezi.../
Nasi tutawapokea kwa shangwe tulivyo wapuuzi.../
Yaani mambo yaleyale alishasema ganzi kuzi.../
Kivipi maskini watapata nafuu vijana wanakua mapema hivi nitapata mjukuu..../
Sinaga makuu seduce me sinaga tattoo/
Wanangu chini ya dola moja tunajiruzukuu/

Kiitikio

Tuna freedom lakini kuwa free Bado
Tuna Kingdom lakini kuwa ma king Bado
Mambo yaishe wala usiulize Rado
Hapa tuna mishe mishe so tuko busy Bado. X2